Ni msanii gani wa Comedy unaona kabisa hamnaga kazi ila ndo hivyo tu

Ni msanii gani wa Comedy unaona kabisa hamnaga kazi ila ndo hivyo tu

Mtu ambaye akisimama jukwaani huwa nacheka ni mandevu tu kwa sasa ila wengine ni wanatafuta ugali tu.

Kuna mtu anayejiita mzee shayo ndio sijawahi kumuelewa kabisa kila nikijitahidi kumfuatilia sijui anachokifanya kabisa
 
Kuna huyu Eliud nilimuona Arusha juzi kwenye standup comedy ya Churchill ya wakenya aliua vizuri tu ila Eric omondi alikuwa wa Kawahida Sana pale jukwani
Ila yote kwa yote kuchekesha kazi Sana Kuna jamaa wale wa Moshi wapo wawili walipanda duh aibu nikawa Naona Mimi mtazamaji
 
Binafsi, kuna huyu wa kujiita Shafii Comedy. In short hakuna anachofurahisha. Ni kama alilazimusha tu kuwepo huko, na watu ambao wameamua kumpiga tafu tu, Hakuna kitu kabisa aisee

View attachment 3188397
Kwako ni yupi unaona kabisa hamna kazi
kuna kile kifupi sijui kinaitwa Anko Nzala nacho chenga
 
Chukua list yote ya Cheka Tu & Watu Baki, watoe TX Dullah, Madevu: hawa wanafanya vizuri kotekote kwenye kuigiza (skit) na stand-up comedy, wana story na punchline zitakazokufanya ucheke.

Wapo wengi wanajitahidi ila kwenye angle ya uigizaji zaidi kuliko stand-up comedy:

1. Eliud: yupo vizuri sana kwenye uigizaji kuliko stand-up comedy ila bado anaweza kujiboresha zaidi.

2. Jol Master: tatizo lake kubwa ana mapepe sana awapo jukwaani na maudhui yake kwa asilimia kubwa ni ngono na ndiyo tasnia nzima ya comedy imelalia upande huo, mpaka wakina TX Dullah wanaanza kupita na huo upepo kwenye skit zao. Wengine kwenye skit zao wanahamasisha mpaka ubakaji kwa kigezo cha uchekeshaji bila kujua.

***Leonardo: kipindi anaanza alikuwa anafanya vizuri sana kwenye stand-up comedy, sasa hivi itakuwa kashalewa sifa. Kwenye uigizaji (skit) uhusika wake ni kama anafanya maudhui kwaajili ya watoto.

***Kipotoshi pale Watu Baki naye anajitahidi sana kusukuma gurudumu yupo na dogo mwingine akipanda jukwaani unatamani asishuke.

Wanaobaki: Coy Mzungu, Ndaro, Steve Mweusi, Madirisha (huyu hajui kuchekesha wala kuingiza, anabebwa kishkaji), Mtumishi Obama, Shafii Brand (sharobaro), Mr. Black, MC Kisoli (aweke nguvu kwenye utangazaji na ushereheshaji tu), Chard Talent (muigizaji mzuri ila siyo uchekeshaji), Deo (kelele nyingi tu, kwenye uigizaji anaweza aweke nguvu huko) hawa wangetafuta shughuli nyingine za kufanya, angalau mwenzao Coy Mzungu kajipata. List ni ndefu sana, wapo wanaojitahidi ila wengine ni wasindikizaji tu.

Cha msingi watu wapambane tu wapige madusko yao, muhimu mkate/ugali ukae mezani. Kwa hapa bongo watapiga pesa tu maana tasnia yetu ya sanaa hadhira imeshazoea kupokea kazi mbovu, kuanzia muziki, filamu, uchekeshaji n.k.
 
Yaani umetoka huko kuja kumfungulia sledi mwanaume anaefaiti kupata riziki. Dada usidharau kazi ya mtu yeyote. Asiefanya kazi na asile. Kama hakufurahishi pita mbali.

Yaani nifungue genge la nyanya halafu uje useme biashara yangu haikufurahishi?! acha umama
 
Back
Top Bottom