Chukua list yote ya Cheka Tu & Watu Baki, watoe TX Dullah, Madevu: hawa wanafanya vizuri kotekote kwenye kuigiza (skit) na stand-up comedy, wana story na punchline zitakazokufanya ucheke.
Wapo wengi wanajitahidi ila kwenye angle ya uigizaji zaidi kuliko stand-up comedy:
1. Eliud: yupo vizuri sana kwenye uigizaji kuliko stand-up comedy ila bado anaweza kujiboresha zaidi.
2. Jol Master: tatizo lake kubwa ana mapepe sana awapo jukwaani na maudhui yake kwa asilimia kubwa ni ngono na ndiyo tasnia nzima ya comedy imelalia upande huo, mpaka wakina TX Dullah wanaanza kupita na huo upepo kwenye skit zao. Wengine kwenye skit zao wanahamasisha mpaka ubakaji kwa kigezo cha uchekeshaji bila kujua.
***Leonardo: kipindi anaanza alikuwa anafanya vizuri sana kwenye stand-up comedy, sasa hivi itakuwa kashalewa sifa. Kwenye uigizaji (skit) uhusika wake ni kama anafanya maudhui kwaajili ya watoto.
***Kipotoshi pale Watu Baki naye anajitahidi sana kusukuma gurudumu yupo na dogo mwingine akipanda jukwaani unatamani asishuke.
Wanaobaki: Coy Mzungu, Ndaro, Steve Mweusi, Madirisha (huyu hajui kuchekesha wala kuingiza, anabebwa kishkaji), Mtumishi Obama, Shafii Brand (sharobaro), Mr. Black, MC Kisoli (aweke nguvu kwenye utangazaji na ushereheshaji tu), Chard Talent (muigizaji mzuri ila siyo uchekeshaji), Deo (kelele nyingi tu, kwenye uigizaji anaweza aweke nguvu huko) hawa wangetafuta shughuli nyingine za kufanya, angalau mwenzao Coy Mzungu kajipata. List ni ndefu sana, wapo wanaojitahidi ila wengine ni wasindikizaji tu.
Cha msingi watu wapambane tu wapige madusko yao, muhimu mkate/ugali ukae mezani. Kwa hapa bongo watapiga pesa tu maana tasnia yetu ya sanaa hadhira imeshazoea kupokea kazi mbovu, kuanzia muziki, filamu, uchekeshaji n.k.