Ni msanii gani wa muziki Bongo ambaye tangu uanze kumsikia hujawahi muelewa kabisa?

Ni msanii gani wa muziki Bongo ambaye tangu uanze kumsikia hujawahi muelewa kabisa?

Yes swadakta,hiyo ni miongoni mwa hizo nyimbo zilizokuwa zinanichekesha hasa ikifika kwenye ule mstari unaosema"aliyekuja na ngedere amtoe out maana humu ndani anazua varangati"😃😃😃😃
"Ndani kuna mabuzi, muhogo mchungu anacheza na mbuzi"
Halafu kuna kidemu mle kinarusha kiuno kiselasela na khanga yake
 
UVC T-shirt na Jeans yalikuwaga mabenga
Mabaga Fresh wazee wa kutaabika.....Enzi hizo husikii biti ya mapiano.
Hiyo T-shirt na jeans ni balaa na nusu
Halafu kuna vumilia walioimba na feruz
 
Uko sahihi vijana wa siku hizi wameacha kabisa kuangalia contents za msanii wanachoangalia ni mafanikio ya msanii na jinsi anavyotrend mitandaoni yaani hata kama anaimba matusi tu basi huyo ni muimbaji mzuri kwao.
Kwa mfano kwa sasa msanii akijiunga tu na Wasafi basi huyo anaonekana ni mwimbaji bora hata kama anachoimba ni utopolo
Amini mkuu
Hivi kina Chino sijui chinawaman, jaiva, mabantu wanaimba nn
Ukisikiliza nyimbo zao hakuna rhymes, hakuna rhythm ,hakuna ujumbe
 
Kazi kuvua mashati kwenye video zake
Yaani Jux akichora tatoo mpya tu shida na akihudhuria Gym week nzima anafosi atoe nyimbo mpya ili aoneshe alivyogain muscles ndani ya hiyo week
Ila mnawavyoakanda
Kama wanapita kusoma humu basi watakua wanatukana sana
 
Amini mkuu
Hivi kina Chino sijui chinawaman, jaiva, mabantu wanaimba nn
Ukisikiliza nyimbo zao hakuna rhymes, hakuna rhythm ,hakuna ujumbe
Yeah wanaiga tu beat kali za Amapiano ila kinachoimbwa cha maana hakuna.
Washabiki wanashangilia wanamvimbisha kichwa kujiona bonge la msanii.
 
Dully syks nyimbo zake hazieleweki kabisa.yaani anaimba maneno mengine hata yeye hayajui.mfano Kuna wimbo siufahamu anaimba Njagara Njagara ooh ooh.
Aisee nimecheka na hiyo njagara njagara
 
N'jomba Nchumali aka Harmonize sijawahi elewa kabisa uyu Mmakonde
 
Kuna watu Kanda ya ziwa wakiskia unasema hivyo wanakuona wewe ndio una matatizo huyo ni kama diamond kwenye chaka to chaka na ana mpunga mrefu uliotokana na muziki binafsi napenda Ngoma zake kama Khadija, maisha ni utata
Best naso hapana kwakweli, hizo hela anapeleka studio bora angekua anakula nyama choma ajenge shavu
 
Kwenye hip hop wako wengi ila Gaidi la rap King Izzy, Joh makini, Fid Q, Darrasa, FA naomba wasiguswe waachwe na muziki wao.
Kuna huyo kwa dp yako ni kichwa kinoma, niki wa pili
 
Back
Top Bottom