Ni mstari gani kwenye biblia unautumia sana upitiapo nyakati ngumu katika Maisha

1. Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake.


2. Usihukumu nawe utahukumiwa.
Kuna watu wanapenda kukosoa sana wenzao kama vile wao ni watakatifu

3.Mimi ndimi njia ya kweli na uzima mtu hawezi kwenda kwa Baba bila kupitia kwangu
 
Zaburi ya 23
 
Zaburi 23
BWANA ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza
Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
5Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika.
6 Hakika wema na fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Hiyo hapo
 
Hoses 4: 6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
[emoji106]
 
Zaburi:23
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…