Ni muda Cheo cha Makamu wa Rais kifutwe Tanzania

Ni sawa na Nafasi ya Dc ni kupoteza pesa tu iyo kazi afanye DED , nafasi ya ma naibu waziri izo wake makatibu wa wizara
 

Nadhani hujanielewa. Mimi nashauri kiondolewe kisiwepo maana kwa Sasa hakuna impact yoyote. Ukisoma andiko langu, nimeweza kushauri ni wapi Mazingira na Muungano vipelekwe. Tubaki na Rais na Waziri Mkuu.

Halafu kwa Tanzania Rais ana mamlaka yote, hivyo anaweza kufanya kazi bila umakamu wa Rais. Kama kukaimu anaweza kumkaimisha hata Waziri Mkuu au Waziri yeyote.
 

Pia tujiulize, ukimtoa Makamu wa Rais Leo, Kuna madhara gani yatatokea?. Nini kitapungua?.
 

Kweli kabisa mkuu.
 
Watanzania wengi tumepagawa,imagine mtu anataka makamu wa rais afutwe ,waziri mkuu afutwe 😁😁

Nimesema Makamu wa Rais, Kama nafasi sio mtu. Hii itapunguza gharama na mabajeti yasiyokuwa na maana. Halafu sijamzungumzia Waziri Mkuu labda Kama unamnukuu mtu mwingine.
 

Nimekuelewa mkuu
 
Kwa Tanzania, cheo ambacho hakitakiwi ni Cha Waziri Mkuu. Waziri Mkuu HANA KAZI yoyote ingawa inaonekana anayo. Mfano, wewe umesema ana uwezo kumfukuza kazi MTUMISHI; sio kweli.

Ila Makamu wa Rais cheo chake ni kikubwa zaidi ya tunavyokiona. Sana sana tu labda cheo chake kiongezewe majukumu ya Waziri Mkuu kikae sawa.
 

Umeongea Jambo la msingi sana. Tubadilishe katiba ili tuweke mfumo mzuri wa kumkaimu Rais.
 
WAKO WAPI WA JARIBIO LA UTEKAJI WA DEO BONGE
 
Kwa maoni yangu,
nadhani kile cheo cha makamu mwenyekiti wa chadema taifa ndicho hasa hakina maana wala umuhimu, na kilichopoteza uelekeo kabisa, na kwakweli kinachochochea uhasama na kuzidisha mpasuko na mgawanyiko chadema, ndicho haswaaa cha kufutilia mbali...

kuhusu kwingineko,
nadhani kuna tatizo la uelewa na ufahamu tu, juu ya umuhimu na maana ya makamu au naibu rais. Ukijua malego na madhumuni yake licha ya gharama yake, kamwe huwezi kufikiri wala kusema ulichokiandika. Akina Aristotle na Plato hawakua na ufinyu wa fikra kama huo wa kwenye hoja ya msingi, ndiyo maana wakabuni na kuweka nafasi hiyo.

Na kwa binadamu alivyo,
mpaka kwanza apate tatizo ndipo aone umuhimu wa jambo alilokua akilidharau au haelewi wala kuona umuhimu wake.

Nachelea kusema,
kama kuna nafasi muhimu, nzito na ya maana sana ambayo kamwe haistahili hata mjadala wa kuwepo kwake basi ni nafasi ya Makamu au naibu wa rais.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…