Ni muda Cheo cha Makamu wa Rais kifutwe Tanzania

Ni muda Cheo cha Makamu wa Rais kifutwe Tanzania

Ni sawa na Nafasi ya Dc ni kupoteza pesa tu iyo kazi afanye DED , nafasi ya ma naibu waziri izo wake makatibu wa wizara
 
Logics zinakataa Boss, lakini pia angalia best practice duniani, nchi nyingi zenye Rais Mtendaji huwa Zina Makamu wa Rais ambaye ni Running mate, maana yake amepewa nguvu na watu.

Lakini pia ili kumfanya Makamu awe na kazi ya kufanya day in day out kuna baadhi ya nchi Makamu wa Rais Anapewa Wizara fulani fulani, Mfano hapa kwetu ni Mazingira na Muungano; maana yake sio kweli kwamba Hana kazi za kufanya.

Changamoto kwenye andiko lako nadhani unataka kumuona Makamu Yuko on per na Boss wake, hili nafikiri haliwezekani, refer case ya juzi ya Gachagua/Ruto.

Nadhani hujanielewa. Mimi nashauri kiondolewe kisiwepo maana kwa Sasa hakuna impact yoyote. Ukisoma andiko langu, nimeweza kushauri ni wapi Mazingira na Muungano vipelekwe. Tubaki na Rais na Waziri Mkuu.

Halafu kwa Tanzania Rais ana mamlaka yote, hivyo anaweza kufanya kazi bila umakamu wa Rais. Kama kukaimu anaweza kumkaimisha hata Waziri Mkuu au Waziri yeyote.
 
Logics zinakataa Boss, lakini pia angalia best practice duniani, nchi nyingi zenye Rais Mtendaji huwa Zina Makamu wa Rais ambaye ni Running mate, maana yake amepewa nguvu na watu.

Lakini pia ili kumfanya Makamu awe na kazi ya kufanya day in day out kuna baadhi ya nchi Makamu wa Rais Anapewa Wizara fulani fulani, Mfano hapa kwetu ni Mazingira na Muungano; maana yake sio kweli kwamba Hana kazi za kufanya.

Changamoto kwenye andiko lako nadhani unataka kumuona Makamu Yuko on per na Boss wake, hili nafikiri haliwezekani, refer case ya juzi ya Gachagua/Ruto.

Pia tujiulize, ukimtoa Makamu wa Rais Leo, Kuna madhara gani yatatokea?. Nini kitapungua?.
 
Uko sahihi kabisa.nafasi ya makamu haina tija zaidi ya kuongeza gharama zisizo na tija.Na katiba ibadilike ili ikitokea rais amefariki basi waziri mkuu akaimu Kwa muda wa miezi sita au mwaka mmoja na kuitisha uchaguzi upya ili kuondoa muserereko wa mtu kupata nafasi ya urais chumbani kwake.

Kweli kabisa mkuu.
 
Watanzania wengi tumepagawa,imagine mtu anataka makamu wa rais afutwe ,waziri mkuu afutwe 😁😁

Nimesema Makamu wa Rais, Kama nafasi sio mtu. Hii itapunguza gharama na mabajeti yasiyokuwa na maana. Halafu sijamzungumzia Waziri Mkuu labda Kama unamnukuu mtu mwingine.
 
Kwa sasa usimlaumu sana makamo wa raisi sababu kwa awamu hii ndani ya serikali kuna serikali nyingine tusiyoijua na yenye nguvu kuliko serikali tunayoijua.

Mfano Abdul wa mama Abdul ana madaraka na kauli kuliko hata Waziri Mkuu.

Hii nchi imekuwa mateka ya wapumbavu. Tunatawalia na wapumbavu na kwa vile kabla ya hapo sisi wenyewe ni wapumbavu wakubwa zaidi basi imekuwa ni balanced equation ya upumbavu.

Nimekuelewa mkuu
 
Kwa Sasa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania inatakiwa kupitiwa upya, na kuondoa cheo Cha Makamu wa Rais. Cheo hili hakina tija kinaongeza tu mlundikano wa vyeo visivyokuwa na maana.

Makamu wa Rais Hana mamlaka Kama aliyonayo Waziri Mkuu, ndio maana Waziri Mkuu anaweza kumfukuza au kumsimamisha kazi Mtumishi ila sio Makamu wa Rais.

Nafasi ya Makamu wa Rais imekuwa ceremonial tu. Makamu wa Rais anaweza kupotea hata miezi SITA na wananchi wasishangae au Makamu wa Rais ataonekana Sana kwenye ufunguzi wa warsha na makongamano.

Ni kweli Makamu wa Rais yupo kwaajili ya kukaimu nafasi ya urais Rais anapokuwa nje ya nchi, ila sio lazima yeye akaimu , Rais anaweza kumkaimisha yeyote madaraka ya Urais akiwa nje.

Nashauri baadala ya kutumia pesa nyingi kumuhudumia Makamu wa Rais na watu wake, ni bora kuondoa hicho cheo na Mazingira pamoja na Muungano vikaunganishwa kwenye Wizara ya mambo ya ndani .
Kwa Tanzania, cheo ambacho hakitakiwi ni Cha Waziri Mkuu. Waziri Mkuu HANA KAZI yoyote ingawa inaonekana anayo. Mfano, wewe umesema ana uwezo kumfukuza kazi MTUMISHI; sio kweli.

Ila Makamu wa Rais cheo chake ni kikubwa zaidi ya tunavyokiona. Sana sana tu labda cheo chake kiongezewe majukumu ya Waziri Mkuu kikae sawa.
 
Cheo Cha makumu wa raisi kimewekwa ili kuwaridhisha wazanzibari wajione nao ni watawala kwenye muungano.
Ikiwa raisi ni mtanganyika

Sasa kibao kimegeuka raisi ni mzanzibar Makamu wa raisi ni redundunt

Tumeishashauri sana juu ya mabadiliko ya katiba mpya hawatusikilizi

Umeongea Jambo la msingi sana. Tubadilishe katiba ili tuweke mfumo mzuri wa kumkaimu Rais.
 
1. Mmiliki wa Jengo yupo wapi?
NANI NI MMILIKI WAJENGO.
2. Ramani za jengo ziko wapi??
Uokozi bila Ramani.

3. Ghorofa nne watu wanaokolewa siku nne na sio moja. TAIFA LIMEOZA.

4. Selikali ipo Radhi kununua Mabomu, magali ya Jeshi nk kuizuia CHADEMA na Inashindwa KUNUNUA VIFAA VYA UOKOAJI kwa Raia wake.

5. Niffer amejipeleka Kituoni, Yuko wapi mmliki wa Jengo.

6. Je ni nani aliyetoa vibali vya kujenga na kubomoa anakamatwa Niffer.
TANZANIA YANGU MASIKINI

ZIMA MOTO NA UOKOAJI NI SAWA NA HAKUNA KITU ZERO KABISA.
JESHI LIVUNJWE HARAKA

MAJENGO MENGI KARIAKOO YAMEOZA
WAKO WAPI WA JARIBIO LA UTEKAJI WA DEO BONGE
 
Kwa Sasa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania inatakiwa kupitiwa upya, na kuondoa cheo Cha Makamu wa Rais. Cheo hili hakina tija kinaongeza tu mlundikano wa vyeo visivyokuwa na maana.

Makamu wa Rais Hana mamlaka Kama aliyonayo Waziri Mkuu, ndio maana Waziri Mkuu anaweza kumfukuza au kumsimamisha kazi Mtumishi ila sio Makamu wa Rais.

Nafasi ya Makamu wa Rais imekuwa ceremonial tu. Makamu wa Rais anaweza kupotea hata miezi SITA na wananchi wasishangae au Makamu wa Rais ataonekana Sana kwenye ufunguzi wa warsha na makongamano.

Ni kweli Makamu wa Rais yupo kwaajili ya kukaimu nafasi ya urais Rais anapokuwa nje ya nchi, ila sio lazima yeye akaimu , Rais anaweza kumkaimisha yeyote madaraka ya Urais akiwa nje.

Nashauri baadala ya kutumia pesa nyingi kumuhudumia Makamu wa Rais na watu wake, ni bora kuondoa hicho cheo na Mazingira pamoja na Muungano vikaunganishwa kwenye Wizara ya mambo ya ndani .
Kwa maoni yangu,
nadhani kile cheo cha makamu mwenyekiti wa chadema taifa ndicho hasa hakina maana wala umuhimu, na kilichopoteza uelekeo kabisa, na kwakweli kinachochochea uhasama na kuzidisha mpasuko na mgawanyiko chadema, ndicho haswaaa cha kufutilia mbali...

kuhusu kwingineko,
nadhani kuna tatizo la uelewa na ufahamu tu, juu ya umuhimu na maana ya makamu au naibu rais. Ukijua malego na madhumuni yake licha ya gharama yake, kamwe huwezi kufikiri wala kusema ulichokiandika. Akina Aristotle na Plato hawakua na ufinyu wa fikra kama huo wa kwenye hoja ya msingi, ndiyo maana wakabuni na kuweka nafasi hiyo.

Na kwa binadamu alivyo,
mpaka kwanza apate tatizo ndipo aone umuhimu wa jambo alilokua akilidharau au haelewi wala kuona umuhimu wake.

Nachelea kusema,
kama kuna nafasi muhimu, nzito na ya maana sana ambayo kamwe haistahili hata mjadala wa kuwepo kwake basi ni nafasi ya Makamu au naibu wa rais.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom