Ni muda sasa sijawahi kumbuka ndoto yoyote niliyoota

Ni muda sasa sijawahi kumbuka ndoto yoyote niliyoota

Chukua chumvi ya mawe kiganja kimoja tia kwenye ndio ya maji kaoge kabla ya kulala usiku
Mwisho utamwambia achukue pande la Mkaa aweke Chini ya Mto wa kulalia kichwani
 
Ombea ufahamu wako.. wa mwilini na rohoni...
Ndoto ni jambo la muhimu sana zipo taarifa unapewa kwa njia ya ndoto hivyo adui akikuwahi anakusahaulisha. Ombea ufahamu hivyo tu
 
Ni serious Comedy SIO Comedy
Mkuu unaharibu uzi, Hii dunia ni kubwa na bado tunaendelea kujifunza ili tuijue zaidi... Kuna ndoto zina maana kubwa sana katika maisha yetu.... Nikupe tafakuri kidogo, Hivi unahisi ni kwanini Nikola Tesla alikuwa akizunguka nyumba mara tatu kabla ya kuingia ndani? Bado hatujafahamu formula za ulimwengu. Ila tukija kuzingundua maisha yatakuwa mepesi sana
 
Ombea ufahamu wako.. wa mwilini na rohoni...
Ndoto ni jambo la muhimu sana zipo taarifa unapewa kwa njia ya ndoto hivyo adui akikuwahi anakusahaulisha. Ombea ufahamu hivyo tu
Sawa kabisa, kweli napaswa kufanya maombi juu ya hali hii, inanifanya nakosa amani.
 
Mkuu unaharibu uzi, Hii dunia ni kubwa na bado tunaendelea kujifunza ili tuijue zaidi... Kuna ndoto zina maana kubwa sana katika maisha yetu.... Nikupe tafakuri kidogo, Hivi unahisi ni kwanini Nikola Tesla alikuwa akizunguka nyumba mara tatu kabla ya kuingia ndani? Bado hatujafahamu formula za ulimwengu. Ila tukija kuzingundua maisha yatakuwa mepesi sana
Nikwambie kitu mkuu, HUKO kwenye Mambo hayo ya mauzauza nilishatokaga zamani the more you go the more you get the more you give, tell me Nikola Tesla alikufaje? Km kweli umemsoma na kumjua niambie alikufaje Kifo chake kilikuaje kuaje?
 
Mie naota halafu zinakua na maana kabisa, yani nnayoyaota yanatokea....

Nilishajifunza kitambo huwa sipuuzii ndoto zangu kabisa. Kuna siku niliota ugomvi yani kila nilichokiota kesho yake kilikua kama nilivoona ndotoni.
Hii hali hunitokea sana mimi pia, sometimes inaniogopesha though on other side namshukuru Mungu kwasababu huwa nachukua hatua mapema
 
JApo ningetaman unisaidie kufafanu zaid, lakin usimacho kinaweza kikawa kwel, maana siku ya 3 yake, nikashtuka tena usiku moyo/roho inauma sanaa, kesho yake ikatokea ile ajali ya mbeya (hii ya juzi hapa) and my blood brother alikua mmoja wapo wa waliokuwepo kwenye ajali ile, hali yake badi si nzuri yuko icu mpaka sasa.
Sina uhakika kama kuna connection na those 3 days of dreaming
Fanya sana Ibada, badili mfumo wa maisha na utoe sana Sadaka na Zaka.

Usirudie makosa yaliyopita ingawa kukosea ni kawaida na huwezi kuishi Bila ya kutenda dhambi. Ila kuna jambo/mambo hayako sawa. Zingatia
 
Mie naota halafu zinakua na maana kabisa, yani nnayoyaota yanatokea....

Nilishajifunza kitambo huwa sipuuzii ndoto zangu kabisa. Kuna siku niliota ugomvi yani kila nilichokiota kesho yake kilikua kama nilivoona ndotoni.
Yesss! Wapo wa design hiyo... Kwakweli hasa wanawake.

Aliwahi kunieleza mtu mzima mmoja mwenye hekima, kwamba ukiwa mmojawapo ni dalili za kuwa na kiumbe mzuri, wengi huingia kwenye uganga mbeleni. Ana ushawishi huo sana! Na washirikina wakikujua unae wanakuchezea kukuharibia memory yako.
 
Ndoto ni namna mojawapo ya MUNGU kuwasiliana na wanadamu.Kupitia ndoto,MUNGU anatupa maonyo kuhusu yaliyopita na kutupa ushauri wa namna ya kubadilika for our own good.Kupitia ndoto,anatutabiria yajayo,yawe mazuri au mabaya.
Ukiona umeacha kuzikumbuka ndoto zako,basi jua kwamba umefungwa kiroho ili usiweze kuwasiliana na MUNGU.
Kama kuna maovu unayafanya,jaribu kufanya toba na jitahidi kujuta na kuachana kabisa na hayo maovu.Ukifanya haya,njoo utupe mrejesho nini kimetokea.
Nimewahi kupitia hali kama yako,ila nilijichunguza na nikajirekebisha kasoro zangu na hali ikarudi kama mwanzo.Japokuwa hizi ndoto tunazoziota huwa hazinaga maana ya moja kwa moja vile ulivyoiota,hivyo unahitaji mtaalam wa kukutafsiria,usije ukaota msiba ukadhani ni msiba kweli!
 
Job 33:14-15​

14 For God does speak—now one way, now another— though no one perceives it.
15 In a dream, in a vision of the night, when deep sleep falls on people as they slumber in their beds.
 
Back
Top Bottom