Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Kila tukio likitokea, CDM hutafuta "huruma ya wananchi" kisaikolojia...

Screenshot_20170910-073340.png

Wakati ule kibiti watu kibao wamekufa kwa kumwaga damu, ckusikia kuchangia damu "sbb ya damu ya watanzania inayomwagika"....

Dah!

CHADEMA kutoa damu nchi nzima | East Africa Television

<> semper fi <>
 
Kila tukio likitokea, CDM hutafuta "huruma ya wananchi" kisaikolojia...

View attachment 585485

Wakati ule kibiti watu kibao wamekufa kwa kumwaga damu, ckusikia kuchangia damu "sbb ya damu ya watanzania inayomwagika"....

Dah!

CHADEMA kutoa damu nchi nzima | East Africa Television

<> semper fi <>
Huko kibiti si kuna Mbunge mbona hakupigwa Risasi? Tambua kuwa chadema hawakujua Lisu mnataka kuja kumuua njama zenu zilikuwa siri na hakuna mwana chadema anasaka huruma zenu bali wameamua kutoa Damu kwa uchungu halisi.
 
Anhaaa... Sasa nimeelewa, kumbe tunaoneana uchungu, SI KWA UTANZANIA WETU, BALI KWA MISIMAMO YETU YA KISIASA...

Hapa mimi ambaye sina uanachama wa chama chochote niko na wakati mgumu zaidi, sbb nahc hakutokuwa na wa kunionea uchungu hata kidogo!

<> semper fi <>
 
Hoja zipo nyingi na si nyepesi hivyo labda ujibu kwa kudhani unavyofikiri ndilo jibu, Zipo wapi zile bilion 251 zilipotea wizara ya ujenzi kwa kuwalipa makandarasi hewa?
Kuna kamati za bunge zinazosimamia mambo haya. Afuate taratibu kupitia bunge na atapata jibu. Kuhoji hili jukwaani ni upuuzi. Unataka serikali iingie mitandaoni kukujibu. Mnatumiaje nafasi zenu za ubunge? Kuna njia kupitia kamati za bunge za kuhoji na kupata majibu. Sio majukwaani.

Vipo wapi vyeti vya Bashite mshauri mkuu wa Mtukufu?
Raisi anaweza kuteua msaidizi wake yoyote hata kama hajaingia hata darasa moja ilimradi anaridhika na utendaji wake. Una mashaka na utendaji wa Mh. Makonda?

Nakuhakikishia kuna maprofesa wenye maPh.D wasioweza kufanya anachofanya Makonda.

Makonda aliingilia biashara zenu za unga ndio maana mkamjengea chuki. Acheni upuuzi huu.

Yupo wapi Ben sanane aliyehoji PhD feki ya mtukufu, ?
Hii ni kazi ya vyombo vya usalama. Kuna kesi chungu tele hazijatatuliwa. Ya Ben Saa Nane ni mojawapo tu.

Shinikizo la Ph.D fake ni kashifa tu za CDM. Magufuli amesomea UDSM, maprofesa wake wapo, kwa nini msiangalie records zao kama aliipata digrii yake kihalali. Kwanza mshukuru haamui kuwashitaki kwa kumchafulia jina lake.

Ujenzi wa uwanja wa ndege chato,
Kwani Chato sio sehemu ya TZ?

ununuzi wa ndege kwa cash vilibalikiwa na Bunge?
Kuna kitu kinaitwa Executive Decision. Hii ni power alionayo rais kufanya maamuzi mengine bila kutaka ushauri wa bunge.

Tenda za ununuzi na ujenzi zilitangazwa wapi? Na bei ya ndege ni bei halisi?
Bunge lina uwezo, kupitia kamati zake kuhoji haya na sio kupayuka majukwaani tu ili mpate umaarufu. Fuateni sheria na kanuni za kuhoji na mtapata majibu. Lakini CDM mnatumia kila mwanya kusimama majukwaani na mitandaoni kuhoji vitu mnavyoweza kupata majibu yake kirahisi. Serikali haiwezi kufuata mbinu zenu nayo ijibu mitandaoni hizi hoja.

Zipo wapi zile nyumba za serikali alizojiuzia Mtukufu akagawa kwa mdogo wake na ingine kwa hawala yake ambao hawakuwa watumishi wa umma?
Aliekuwa Rais kipindi hicho alikuwa Mh. Kikwete. Magufuli alikuwa waziri akitimiza maagizo ya bosi wake. Kamuulizeni Rais Kikwete kuhusu hili. Don't sweat Magufuli.

Nakupa hayo machche kwanza maana Hoja ni nyingi na maswali ni mengi sana.
Umeona ilivyokuwa rahisi kuzijibu hoja zenu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.

1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.
Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.

==============================
Baada ya michango mingi iliyowekwa hapa kuna dhana niliyoigusia tu (Internal politics within CDM) na wengi kuuliza kwa nini sikuifafanua. Hapa chini naiongeza ingawaje mwanzoni sikuipa kipaumbele.

Dhana ya 5.
Maadui wa ndani wa CDM walitaka kumuua Lissu ili watimize malengo 3 yafuatayo.

1. Lissu aondoe ushindani katika uchaguzi ujao wa mwenyekiti.

2. Lissu aondoe ushindani katika uteuzi ujao wa mgombea uraisi ifikapo 2020.

3. Lissu atumiwe kama kafara ili kuipa CDM mvuto wa kuonewa huruma na kuichukia serikali katika uchaguzi wa 2020.
wangekuwa watu wa kawaida wangekamatwa siku hiyohiyo ??hayo ni maeneo ya makazi ya waeshimiwa yanalindwa si bure???hakuna namna sie tunasema tu hii sio tanzania yetu..tulizoea kusikia siasa za mauaji kule rwanda na burundi!!
uijaribu kuhamisha ukweli mungu ataumbua watu tu!!!kwa kuogopa basi tuseme ni dhana ya 5 hapo juu ili tusimiminiwe risasi 32

Tuzidi kumuombea tundu lisu apone haraka;;lisu ni hazina kubwa ya taifa ..atatusaidia sheria za kimataifa juzi hapa aliweza kuwaonesha wabunje jinsi walivyotengua sheria walioitunga kwa mbwembwe za makanikia mwez july!!

kupiga kele ya makanikia billa kuondoa kinga ya wahalifu wakuu ktk katiba ni kupoteza muda ...unajua kwann aliyehongwa alimasi hatajwi???ikiwa mwendo huu tutaenda hivhiv sahau maendeleo!!!!uwajibikaji hauletwi na maneno unaletwa na mifumo inayotoa adhabu kwa wahalifu wakuu..
mzalendo wa kweli ni yule atakaye tuletea katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi
 
tokea 1998 lisu alipiga kelele juu ya mikataba mibovu ya uwekaji na Mtukufu alikuwa waziri kipindi hicho na wabunge wa CCM wakapitisha mikataba hiyo leo hii Mtukufu anajidai kupiga kelele kana kwamba hakuwa sehemu ya waliopitisha mikataba mibovu.
Hii ndiyo inayodhihirisha kuwa CDM mmekuwa muflisi kifikra. Ni kweli hapo nyuma serikali za CCM ziliweka sheria mbovu na kusaini mikataba mibovu ya madini wakati Magufuli akiwa waziri. Hakuna utata hapa.

Sasa hivi Magufuli ni Rais na ameamua kwa dhati kurekebisha hii kasoro na wewe mwenyewe unaona matokeo yake. Shutuma hapa ipo wapi kwa serikali hii?

Hapa ndipo mnaponikasirisha. Tumepata mtu anaetatua matatizo ya nyuma yaliyopigiwa kelele nyingi na upinzani lakini bado hamridhiki. Mnataka Magufuli afanye nini ili mridhike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuripoti tishio la kuuawa hawawezi kuripoti BAVICHA; anaripoti mhusika. Kila ukiripoti ni lazima polisi wakuulize unamtilia shaka nani? BAVICHA hawawezi kujibu hilo swali itakuwa ni heresay. Je, kwa nini Lissu mwenyewe hakuripoti?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata jirani anaruhusiwa kiripoti kama fulani anawindwa siyo lazima uripoti mwenyewe na polisi wanatakiwa walichukulie uzito. Polisi kazi yao siyo kukaa ofisini kusubiri watu waje waripoti matukio hapana. Ndiyo maana kuna doria na ndiyo maana wanawahoji hata raia wakisikia tetesi ambayo wanazitilia mashaka.
Polisi hawatakiwi kuchagua nani ameripoti tikio ndio tulishughulikie. Hata kama nimesikia wewe uko kwenye target labda ya kuuliwa na wewe unajua lakini umeanza kukaa kimya au kwa kudharau au kwa woga Mimi nikiripoti polisi wanatakiwa walifanyie kazi maana hiyo ni moja ya kazi zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sina chama bali ninaunga mkono juhudi za serikali hii. Hapo nyuma nilimshambulia sana Lissu kwa hoja zake potofu dhidi ya serikali hii. Hoja zote za Lissu dhidi ya serikali hii ni nyepesi sana na zinajibika kirahisi. Serikali haina haja ya kumuua kwa sababu hana hoja nzito. Nitarudia tena hapa:

Lete hoja yoyote ile ya Lissu dhidi ya serikali hii na nitaijibu hapa, sasa hivi.

Na kwa taarifa yako mimi sio msemaji au muajiriwa wa serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ya Bombadier ambayo tulifichwa yeye kaibua kwanza imezuiliwa mpaka tulipe deni imejibika ki urahisi sana kwamba ni uongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ya Bombadier ambayo tulifichwa yeye kaibua kwanza imezuiliwa mpaka tulipe deni imejibika ki urahisi sana kwamba ni uongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiki ni kitu cha wazi lakini serikali iliamua kulitatua hili tatizo kimya kimya. Lissu na Zitto wakaamua kuidhalilisha serikali hadharani.

Fikiria:
Baba nyumbani anaweza kuwa na madeni mengi tu kufikia kuweka baskeli yake rehani.

Sasa wewe kama mtoto pale nyumbani ukaenda kijiweni na kuutangazia mtaa mzima kuwa baba ana madeni kibao na kuwa Mangi mwenye duka anashikilia baskeli yenu. Hii itakusaidia nini wewe?

Hivi kama baba akijua ulichofanya unafikiri utakula ugali nyumbani jioni ile?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila tukio likitokea, CDM hutafuta "huruma ya wananchi" kisaikolojia...

View attachment 585485

Wakati ule kibiti watu kibao wamekufa kwa kumwaga damu, ckusikia kuchangia damu "sbb ya damu ya watanzania inayomwagika"....

Dah!

CHADEMA kutoa damu nchi nzima | East Africa Television

<> semper fi <>
Kila mtu ana familia yake na kila familia ina mpango wake.
Wale wa kibiti walikuwa viongozi wa CCM kwani CCM walikatazwa kufanya kama wenzao wanavyotaka kufanya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki ni kitu cha wazi lakini serikali iliamua kulitatua hili tatizo kimya kimya. Lissu na Zitto wakaamua kuidhalilisha serikali hadharani.

Fikiria:
Baba nyumbani anaweza kuwa na madeni mengi tu kufikia kuweka baskeli yake rehani.

Sasa wewe kama mtoto pale nyumbani ukaenda kijiweni na kuutangazia mtaa mzima kuwa baba ana madeni kibao na kuwa Mangi mwenye duka anashikilia baskeli yenu. Hii itakusaidia nini wewe?

Hivi kama baba akijua ulichofanya unafikiri utakula ugali nyumbani jioni ile?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ile press conference ilikuwa ya kiswahili na pia aliwaambia Watanzania siyo watu wa nje kwa hiyo ametufahamisha kuwa kodi zetu safari hii zitalipa deni njaa.
Mbona Nyerere baada ya vita ya Uganda alitueleza kwanza hali ni mbaya tufunge mikanda miezi 18 tulikasirika lakini tulimuelewa. Hayo ndiyo madhara ya kuficha maradhi

Unafikiri Kiswahili kinaeleweka katika mipaka ya Tanzania pekee?

Halafu baada ya wewe, kama mlipa kodi, kujua hadharani kuwa tunadaiwa, hii imekusaidia nini. Hutalipa kodi tena? Deni letu litafutika, au nini, zaidi ya kuidhalilisha serikali hii. Na kwa faida ya nani?

Ndio maana niliutilia shaka uzalendo wake. Mke na mume wakigombana ndani si busara mmoja wao kuwaeleza majirani wote ugomvi wao. Hii haimdhalilishi mwenzie tu bali familia nzima.

Nitalipa lakini nitaelewa nitajipanga nijue naishi vipi kuliko kukaa kulaumu ooh hakuna sawa kumbe pesa zimelipa deni Mimi sijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi binafsi sijapenda alichofanyiwa mbunge na mwanasheria machachari mheshimiwa Tundu lisu ,lakini kitu ambacho watu hawajui ni kwamba kuna uwezekano Mheshimiwa rais hajui au anajua kuna wanasiasa wanataka kumfurahisha wakijua watapewa vyeo kwa kuwafanyia vitendo vya ukatili viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani,(hapa wenye ufahamu mmenielewa) .Upande wa pili ni ndani ya CHADEMA huenda mbowe hajui au anajua kuna wanasiasa ndani ya chama chake hawampendi lisu na wanamwona kama mwiba kwenye uchaguzi ndani ya chama,na wamechukua advantage ya ugomvi wa lisu na serikali kufanya yao ili mtuhumiwa aonekane ni yule alikua anagombana naye,mimi sijui bado giza kwangu sijui wadau mnasemaje na nyie
 
Nitalipa lakini nitaelewa nitajipanga nijue naishi vipi kuliko kukaa kulaumu ooh hakuna sawa kumbe pesa zimelipa deni Mimi sijui

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa.

Lakini hii imetufahamisha dhamira za wenzetu. Sio kuishauri serikali bali kutumia siri za serikali kuiumbua.

Unafikiri watu kama hawa ni wa kuwajumuisha au kuwataka ushauri kwenye mambo nyeti ya nchi? Mtaishia nje ya mageti kwa kukosa uaminifu.

Msilie kuwa serikali hii haitaki ushauri. Nyie, kwa hulka zenu kama hizi hampaswi kufahamishwa chochote mpaka kitakapotokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafikiri Kiswahili kinaeleweka katika mipaka ya Tanzania pekee?

Halafu baada ya wewe, kama mlipa kodi, kujua hadharani kuwa tunadaiwa, hii imekusaidia nini. Hutalipa kodi tena? Deni letu litafutika, au nini, zaidi ya kuidhalilisha serikali hii. Na kwa faida ya nani?

Ndio maana niliutilia shaka uzalendo wake. Mke na mume wakigombana ndani si busara mmoja wao kuwaeleza majirani wote ugomvi wao. Hii haimdhalilishi mwenzie tu bali familia nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaap, mke na mume wakigombana ni siri yao huko ndani, lkn serikali ikidaiwa lazima tujue coz kodi zetu ndo zinazoenda kulipa hilo deni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi binafsi sijapenda alichofanyiwa mbunge na mwanasheria machachari mheshimiwa Tundu lisu ,lakini kitu ambacho watu hawajui ni kwamba kuna uwezekano Mheshimiwa rais hajui au anajua kuna wanasiasa wanataka kumfurahisha wakijua watapewa vyeo kwa kuwafanyia vitendo vya ukatili viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani,(hapa wenye ufahamu mmenielewa) .Upande wa pili ni ndani ya CHADEMA huenda mbowe hajui au anajua kuna wanasiasa ndani ya chama chake hawampendi lisu na wanamwona kama mwiba kwenye uchaguzi ndani ya chama,na wamechukua advantage ya ugomvi wa lisu na serikali kufanya yao ili mtuhumiwa aonekane ni yule alikua anagombana naye,mimi sijui bado giza kwangu sijui wadau mnasemaje na nyie
Mtarimbo kila siku tunasema usitutoe kwenye reli hilo la Lisu lina sura moja tu.mkubwa anapenda sifa sana bila kukosolewa anapenda aonekane malaika mbele ya watanzania sasa makombora yanayorushwa na lisu ambayo yana ukweli mtupu yameendelea kumuudhi mkumbwa ndo maana hata mahita alipohojiwa majuzi alisema waziwazi kuwa wamezungumza na kutoa ushauri juu ya kuwakabili wanasiasa.nani asiyemjua mahita ?roho yake ?wenye akili tumeishajua mbili +mbili ni nne.(hesabu ndogo tu inakushinda?)Mwenyezi Mungu amependa kuwaumbua na story itasimuliwa na watanzania watajulishwa mchezo wote ameisha tweet baada ya kuzinduka labda mtume tena wauaji
 
Back
Top Bottom