Huyu mtu amesema wazi kabisa kuwa ukiwa msaliti huwezi ku-survive. Maana halisi ni kuwa atakuua. Lakini ni nani anayeamua kuwa fulani ni msaliti na mwingine ni mzalendo? Msaliti ni mtu gani? Ni yule anayehoji maamuzi mabaya? Ni yule anayekataa maamuzi ya kijinga? Au ni yule ambaye anaimba nyimbo za kusifu hata pale ambapo kuna uwongo na hadaa za kisiasa zilizo mbali na ukweli? Ni yule anayesema hewala kwa kila analotamka mkubwa hata kama siyo sahihi?
Leo hii, mimi kama raia nikikwaruzana na jirani yangu halafu nikimwambia kuwa nitakumaliza, kesho yake ikatokea jirani yangu amevamiwa, kwa uhakika kabisa, mimi nitakuwa mtuhumiwa wa kwanza. Kwenye hili, hivi tuna shaka lolote la mtuhumiwa mkuu kwa tukio la TL?