Hapana Mbowe hawezi kujipeleka mwenyewe Mahakamani, Mwenye Mamlaka ya kufanyia kazi hizo tuhuma ni vyombo vya dola na kumkamata Mbowe mara moja ili achukuliwe hatua.
 
Uchunguzi si bado unaendelea,ukweli utajulikana tu na siku baada ya siku tunaanza kupata ukweli na huenda pia ni chanzo cha baadhi ya wanachama kukihama chama ila ukweli utakuja tu
 
mods wa siku hiz wa JF nao ni vichekesho,eti hii nayo ni "News Alert"
 
Amani kwenu ndugu zangu!! Ngoja tu nianze na hili swali kuntu..... 'Baada ya lissu na dereva wake kugundua kwamba kuna watu wanawafuatilia,ni nani baina yao(lissu/dereva wake) aliyeshauri au kuamua waelekee kule tukio lilipofanyika?(Area D)" swali hili linakuja kutokana na maswali makuu mawili ambayo yamakuwa yakijitokeza kila kunapokuwa na mjadala kuhusiana na hili sakata la lissu.
(1) kwanini walinzi wa sehemu husika(Area D) waliondolewa siku ya tukio ama siku chache kabla ya tukio?
(2) kwanini cctv camera ziliondolewa siku ya tukio ama siku chache kabla ya tukio?
Hivyo basi hapa tunaona kwamba ,waliofanya tukio lile walijua mapema kuwa lissu atakwenda area D baada ya kutoka bungeni ndio maana wakaondoa aina zote za ushahidi katika maeneo yale.
Swali linakuja ....
Yeyote aliyehusika (Wasiojulikana,Serikali au wabaya wa serikali) aliwezaje kuyajua maamuzi ya lissu na dereva wake ya kuamua kwenda kule ambapo wao (wasiojulikana,Serikali,wabaya wa serikali) wanataka? ...ikizingatiwa kuwa lissu na dereva wake walishagundua wanafuatiliwa tangu wakiwa kwenye maeneo ya bunge,kwanini hawakuamua kurudi bungeni?kwanini hawakwenda kituo cha polisi?kwanini walikwenda kule kule mtegoni?
Hapa inaweza ikaletwa hoja kuwa ; lissu na dereva wake waliamua kwenda Area D....
Kwa sababu waliamini watakuwa salama zaidi kwa kuzingatia kwamba
-yale ni makazi ya lissu mwenyewe
-yale ni makazi ya viongozi wengi wa serikali na bunge
-katika eneo lile kuna ulinzi wa uhakika
Lakini bado hayo yote hayafuti hili swali ;wahusika wa tukio lile waliwezaje kuwa na uhakika wa 100% kuwa lissu na dereva wake wataelekea Area D mpaka wakaamua kupasafisha kabisa? Na hapo ndipo lile swali nililoanza nalo kwenye bandiko hili linapojitokeza.ni nani kati ya lissu na dereva wake aliyetoa ushauri au kuamua waelekee Area D?
Je serikali inahusika,jumba bovu kwa serikali au tunachezewa akili?
Kwanini kuna uwezekano tunachezewa akili? Siku nafasi ikipatikana nitajaribu kuelezea tena.
 
Jibu ni kuwa hao watu hawakuanza siku hiyo kumfuatilia Lissu kwana hata hapa Dra es Salaam walikuwa wanamfuatlia kila siku na aliwahi kulizungumzia hili hadharani. Nia ya kumfuatilia kwa muda mrefu hivyo ni kujua nyendo zake ili iwe rahisi wao kujua sehemu muafaka kufanya shambulio lao, na ni dhahiri kuwa hata kipindi yuko Dodoma kwenye kikao cha bunge walishajua ratiba yake kuwa mchana huwa anakwenda nyumbani kwake.
 
Watanzania wanaendelea kuchapa kazi Kama kawaida, issue ya Lissu imebaki Kama story Za Kikombe Cha Babu

K
 
Unaongelea nafasi? Umezuiwa Mkuu au ndo propaganda? Hivi angefanyiwa mbunge WA ccm hali ingekua hivi
 
Hakuna haja ya kulizungumzia sana hii issue kwani wahusika waliishajulikana long time hata watoto wa chekechea wanalifahamu hili.

The answer is simple, just wear a T.shirt with inscriptions "Pray for Tundu Lissu" and you will know who the suspects are and that's all.
 
Mkuu, tukio kama hilo ni kama wizi wa gari, linachukua muda kupangwa, huenda hata waliashajaribu baadhi ya siku wakamkosa. Hakuna mwizi wa gari anayekutana na gari siku hiyo hiyo na kuliiba.
 
Watanzania wenzangu ningeomba tujadili kidogo ili kupanua ufahamu wetu na kutoa hoja zenye mashiko ili kutetea kile tunachokiamini.

Kumekuwa na msigano mkubwa wa watu kuwa na mitazamo tofauti kutokana na shambulio la ndugu yetu Lissu. Sasa nimuombe kila mmoja anayechangia ajaribu kueleza sababu ya yeye kuamini kuwa lilipangwa na vigogo wa chama chake na angalau atoe kiashirio kimoja cha kutetea hoja yake.

Pili wale wote wanaoamini ni serikali iliyofanya shambulio hilo basi toeni vielelezo vya kutetea hoja.

Swali moja la kuanza nalo kama ni vigogo wa chama chake, hivi ndio walioweza kushawishi walinzi wote wanaolinda nyumba za viongozi wa serikali ikiwemo nyumba ya naibu spika? je serikali imewaacha hao viongozi ambao wamesababisha nchi kuchafuliwa kimataifa kuhusu shambulio la Lissu?

Je hao viongozi wameweza kuishawishi serikali iondoe kamera zote zilizokuwa kwenye compound hiyo?

Toa mawazo yako siyo matusi, tuwe wastarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…