Ma
Mahaba yamekuharibia FOCUS, ulianza vizuri sana but umeshindwa kuficha unachokipenda.
 
Kwanza I declare interest sipo katika mlengo wowote wa chama chochote cha siasa hivyo bandiko langu halina uhusiano na political interests zozote.

Naomba kujuzwa inawezekanaje mtu risasi ikapiga upande wa kushoto wa gari ila muhanga akajeruhiwa mguu wa kulia kama inavyoonekana kwenye picha na dereva akasalimika.

Nimeweka picha apo chini kusindikiza uzi wangu.
 
Mimi huwa najiuliza mpaka ilikuwaje dereva hata asipapaswe na risasi ?
 
Wahusika wangefanya uchunguzi (kwa weledi)kila kitu kingejulikana.
 
Jitahidi japo Mara chache utazame movie za kihidi,jibu utalipata 99% ni uongo
 
Turudi kwenye hoja yangu unamanisha haiwezekani
Huamini? hata Mimi hivyo hivyo siamini
Kwa hivyo hata kwa lissu hata ni movie ilichezwa na washamburiaji walikuwa mahiri sana kama walivyoelekezwa
 
Risasi zilipopigwa dereva wake alishusha kiti chake lisu then akalala wakati wa Hilo shambulio lisu pia alifanikiwa kugeuka akalalia tumbo hivyo mguu uliokuwa kushoto automatically unakuwa upande wa kulia na dereva wake alifanikiwa kushuka bila kudhurika na yeye hakuwa Target hivyo hawakudili nae.
 
Hiyo haiwezekani kwa maisha ya kawaida labda kwenye movie tu. Naomba tukutane kesho
 

Namkubali sana Tundu Lissu na nilisikitika mno kwa Kilichomtokea ila hadi Leo hii najiuliza kwanini Risasi zote zimpate tu Yeye na si Dereva wake? Kwa kutaka Kujiridhisha zaidi juu ya hili nililazimika kuwatafuta baadhi ya Marafiki zangu ambao ni wana Medani ( Wanajeshi ) na Mmoja wao ni wa Kikosi Maalum kabisa Wazee wa Sanga Sanga wanielimishe zaidi juu ya Masuala haya.

Elimu ya awali niliyoipata kutoka Kwao ni kwamba kwa aina ya Bunduki iliyotumika katika Tukio ikitoa Risasi yake basi ina uwezo wa Kusafiri kwa Kasi ya kuanzia mita 50 hadi 75 na ikiwezekana hata 100. Pia wakasema hata iweje Risasi za aina ya Bunduki iliyotumika kwa jinsi ilivyo mkiwa mmekaa Watu Wawili pamoja inaweza ikapenya kutoka kwa Mmoja hadi kwa mwingine kulingana na Mazingira waliopo hao Wawili.

Gari inayoonekana hapa Pichani tunaona jinsi ilivyokoga Risasi nyingi tu na wakati zinapigwa nakumbuka Dereva alisema alikuwemo ndani yake na alikuwa amelala ila baadae kidogo akafungua Mlango na Kushuka kisha akajificha chini. Kinachonichanganya na Kuniumiza Kichwa imekuwaje Yeye hakuna hata Moja iliyomgusa na zote zikamiminika tu Kwake Tundu Lissu wakati walikuwemo wote ndani ya Gari hiyo?

Na hapa ndipo Mzukulu Mimi nakumbuka mno maneno ya Mzee wa Busara Mmoja aliponiambia kuwa kuna ninayoyajua na pia nisiyoyajua kabisa.
 
Kwa kuongezea ni kwamba Lisu pamoja na dreva wake walikuwa wameshashtuka kuhusu gari inayowafuatilia na ndo maana walipoingia parking hawakushuka wakawa wanaangalia ni nini kitafuatia

Na ndo maana hawakufanikisha hadhima yao kwa Lisu

Mungu ni mkubwa....[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Na ku Na kutokushuka kulisaidia Sana maana wangeshuka wangepigwa za kichwa au kifua na biashara ikaishia hapo. Gari ilisaidia Sana kuweka shield.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…