Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ulitaka iwejeHizo syndicate achana nazo
Kwahiyo katibu mkuu wa wizara ya Afya ni upuuzi kumbeShati linapakwa damu na anahongwa daktari anatoa taharifa msisogelee ICU
Sawa Dada maana walimu wengi wa Kiswahili ni madada ma nguinUkiweza kuimudu lugha yako naimani hata akili yako itawaza vitu vyenye manufaa na vyenye tija lugha huiwezi vipi vitu ambavyo vinahitaji fikra pana?
Umeielewa thread??? Rudia tena comment bila muhemkoWamechanganyikiwa, sasa hivi wanaandika tu kama vichaa.
Ninao ushahidi kutoka kwa wafanyakazi wenzake mbeya kuwa dr mpoki ni kada kindaki ndaki wa CHADEMA...... Nilipo ambiwa hili nikawaza sana kama tukio hili limetokea ama ni lakutengenezwa kisayansiHumuamini hata katibu mkuu wako wa wizara ya afya ambae waziri wako Ummy alitutangazia kuwa ni miongoni mwa madaktari waliomuhudumia Dodoma?
Ujinga ukizidi ubinadamu unapungua sana.
Hivi jiulize ukimya wa mtu anayeonekana kutetea kwa nguvu nafasi yake ndani ya chama mpaka waanze kuhoji?
Yule mzee Edward Ana hela kwanini hakutaka kuchangia ndege mpaka wadhaminiwe usafiri wa ndege ,? Ina maana marafiki wa lowassa ni kwa ajiri ya ikulu tu?
La kutengenezaNinao ushahidi kutoka kwa wafanyakazi wenzake mbeya kuwa dr mpoki ni kada kindaki ndaki wa CHADEMA...... Nilipo ambiwa hili nikawaza sana kama tukio hili limetokea ama ni lakutengenezwa kisayansi
Acha mapovu kijanaMods sitaki kuwafundisha kazi, lakini kuna thread nyingi sana za watu wa CCM kukejeli shambulizi la kinyama alilofanyiwa Tundu Lissu kana kwamba yule ni mnyama na si binadamu. Kuendelea kuziacha nyuzi hizo ni kukaribisha lugha za kuudhi na matusi hivyo kushusha hadhi ya jukwaa letu.
Anacho maanisha angetafta hawa wa kuwadhamini hiyo helaina maana lowassa siku hizi ana miliki ndege? ile ni ndege ya Flying doctors(AMREF) so ina kila accessory ya kumhudumoia mgonjwa kule ndani... kuliko kupandishwa kwenye ndege ya kwaida ambayo haijawa installed na vitu vya medical care
Baadhi ya mambo yanayoendelea yananifanya nisiamini kwamba lissu alishambuliwa na watu wa mbali naye, unaweza kuwa mpango tu endelevu wa kukusanya hela au ya kutafuta huruma kisiasa, maana wanaweza wakamdhuru lissu kwa nia ya kupata sifa zaid na wakafanya hivyo kwa kumficha lissu ukweli,
Hivi jiulize ukimya wa mtu anayeonekana kutetea kwa nguvu nafasi yake ndani ya chama mpaka waanze kuhoji?
Yule mzee Edward Ana hela kwanini hakutaka kuchangia ndege mpaka wadhaminiwe usafiri wa ndege ,? Ina maana marafiki wa lowassa ni kwa ajiri ya ikulu tu?
NANI mpaka sasa ameenda Nairobi kumuona akiruhusiwa kama si nyalandu na mpango wao wa kutafta huruma ya wananchi kugombea arusha mjini?
Tutajua mengi hebu tuendelee
Nyingine ukipitia uzi huu waweza pata picha halisi ya nini chafanyika
Wanachokitengeneza CHADEMA ni siasa za "Appeal to Fear"
Pili kwanini mpaka sasa familia haiwekwi karibu na tukio zima, yaan ni Jambo la kushangaza, ni dili imepangwa kahusishwa mke tu??
Mbali na mke, kuna mwanafamilia mwingine aliyemtembelea Lissu Nairobi?
Muda mwingine najiuliza hivi hawa watu vipi mbona michango imekithiri isije kuwa lengo lao
OK tuendelee au yaweza kuwa kwa ajili ya kujisafisha na accacia??
Kutokana na tuhuma nyingi dhidi ya kupokea rushwa yaweza kuwa njia ya kuwaaminisha watu kuwa hakupokea maana hata hela ya ndege iliwakosa si angetumia hizo?
Kuko wapi Kuhongwa kwa Lissu na Acacia?
Na kama kashambuliwa kweli basi ni ndani ya chama chake wanaosaka nafasi za juu
Swali:Je inawezekana mlemavu ama ukilema wa kufanyiwa au wa kuzaliwa nao,Tanzania akagombea nafasi ya juu akashinda?
Kupitia hayo tu naona sintofahamu Nyingi tu, ngoja tusubiri,
Mungu ameekupa akili uzitumie, siyo kusema kama mtu mpumbavu. Ukiona maisha yako yanatishiwa unaenda kuripoti polisi, unatoa maelezo, wanatafuta jinsi ya kukusaidi. Kuitisha press conference siyo kuripoti polisi. Changanya na zako.Hukumpa ulinzi kisa unasema kwa ujinga wako anabwabwaja, sasa njia ya kuzuia kubwabwaja ni kuuwa? Mbona huko CCM mnabwabwaja ni wengi sana je? na nyie mpigwe Risasi?
Mawazo yanayotokana na ubongo wa matope, Mahakama peke yake ndiyo yenye kuhitimisha kuwa walompiga risasi Lisu walikusudia kumuua. Siyo wewe mjinga mjinga usiyejua hata chembe ya sheria. Nenda shule kwanza.Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.
Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.
Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.
Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.
Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.
Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:
1. Vichaa fulani tu. (Random act)
2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
3. Serikali yenyewe
4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.
1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.
2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.
Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.
Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.
3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.
Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.
Kwa hiyo dhana hii ni potofu
4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.
Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.
Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.
Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.
Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?
Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.
Please tell me I am not crazy.
==============================
Baada ya michango mingi iliyowekwa hapa kuna dhana niliyoigusia tu (Internal politics within CHADEMA) na wengi kuuliza kwa nini sikuifafanua. Hapa chini naiongeza ingawaje mwanzoni sikuipa kipaumbele.
Dhana ya 5.
Maadui wa ndani wa CHADEMA walitaka kumuua Lissu ili watimize malengo 3 yafuatayo.
1. Lissu aondoe ushindani katika uchaguzi ujao wa Uenyekiti.
2. Lissu aondoe ushindani katika uteuzi ujao wa mgombea urais ifikapo 2020.
3. Lissu atumiwe kama kafara ili kuipa CHADEMA mvuto na kuonewa huruma na kuichukia serikali katika uchaguzi wa 2020.