Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
UNAUSHAHIDI GANI KAMA NDIYE ALIYETOA AMRI YA KUMPIGA LISU ACHA UCHONGANISHI
 
Njoni na mpango wa kulipiza kisasi kwa wahusika maana Kama mnaushahidi juu yao. Mpaka Sasa ni propaganda tu ambazo hazina mashiko
 
Jamani tulizeni mzuka.. Suala la Tundu Lissu wala halihitaji nguvu nyingi sana kulisemea..
Damu ya Binadamu haipotei hivi hivi..
Kidogo kidogo wale waliohusika watazidi kuchanganyikiwa, kuropoka ovyo na kudhoofu miili yao mmoja baada ya mwingine..!!
Mwisho wa siku watakufa kabla hata ya huyo Tundu Lissu waliyetaka kudhulumu uhai wake..!!
 
Alifanya kosa sana kutaka kumfunga kinywa Lisu kwa kudhamiria kumuua.
Jiwe miezi yake inahesabika ataondolewa kwenye ulingo wa siasa.
Anachokifanya kama kumpigia mbuzi gitaa,kama kweli nguli wa sheria na ana concrete evidence kwanini asiende mahakamani kuliko kupiga kelele?

Mwanaume asili yake sio kulia lia kama mtoto wa kike,kama ana ubavu amkabili sio kuweka mafumbo mafumbo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alieendesha shambulio ni Ndugai narudia Ndugai narudia Ndugai.
Hapo sisi hatumo kabisa, ila ungepeleka ushahidi polisi ungesaidia kuweka wazi uropokaji wa Lissu. Maana hata mi nasimama kwa Magu yupo Bold lakin asingewez kumfanyia hiyo na bado akaishia kupigwa mguu! ana watu wa kiulinzi halafu aishie kwa mtu asiyejua shabaha na mipango kama mimi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

Hii dhana ni sahihi kabisa! Na tumeshuhudia baadhi ya watu kama Bashite, Kibajaji, Jerry Muro n.k ambao wapo tayari kufanya lolote ili tu kumfurahisha bosi wao.. Kuna kipindi walikuwa (na nahisi bado hali iko hivyo) wanachukizwa na ukosoaji wa aina yoyote unaofanywa dhidi ya bosi wao..!!
So circumstantial evidences zinaonesha kuwa either expressly or impliedly or both hoja yako ni sahihi!!
Swali la kujiuliza ni je, wanaweza kutekeleza zoezi zito kama hili la Tundu Lissu ndani ya eneo ambalo ulinzi wake upo juu kwa asilimia zaidi ya 80% na wakatokomea kusikojulikana bila kupata backup kutoka mamlaka zingine??
 
Serikali ingetaka Tundu afe hakika leo hasingekuwepo hai wala Ulaya anabwabwaja kama Mwendawazimu bali angekuwepo Kabulini tena mzoga ulioliwa na mchwa kwani ni dhihaka kwa Kamanda aliyeiva kisawasawa kutumia risasi 38 bila kiumbe kugeuzwa jina kuwa Marehemu, Serikali ingetumia Risasi 01 tu mtu maji haombi mpaka Kiama hivyo yawezekana ni Genge haramu la wahuni la M4C lisilokuwa na weledi wa Machine Gun chini ya Uongozi wa Dj na Wazee wa Unga ndo walikuwa wanafyatua risasi hovyo hovyo kana kwamba wanarusha hewani ambazo zilimpalaza palaza na kumchubua lakini wazee wa Medani dhubutu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.


1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.
Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.

==============================
Baada ya michango mingi iliyowekwa hapa kuna dhana niliyoigusia tu (Internal politics within CHADEMA) na wengi kuuliza kwa nini sikuifafanua. Hapa chini naiongeza ingawaje mwanzoni sikuipa kipaumbele.

Dhana ya 5.
Maadui wa ndani wa CHADEMA walitaka kumuua Lissu ili watimize malengo 3 yafuatayo.

1. Lissu aondoe ushindani katika uchaguzi ujao wa Uenyekiti.

2. Lissu aondoe ushindani katika uteuzi ujao wa mgombea urais ifikapo 2020.

3. Lissu atumiwe kama kafara ili kuipa CHADEMA mvuto na kuonewa huruma na kuichukia serikali katika uchaguzi wa 2020.
Tumekusikia Kifyatu. Kuna maswali 3 ambayo Tundu Lissu amekuwa akiuliza lakini hakuna aliyejitokeza kujibu. Wanaotakiwa kujibu wananyamaza. Hata wewe umekwepa kuyajibu. Si kwamba hujayasikia Bali no kwa kuwa ukijaribu kujibu tu utajikuta unamsonda yule ambaye usingependa aonekane kuwa ndo aliyehusika na jaribio LA mauaji ya Tundu Lissu. Maswali haya no:
1. Kwa nini walinzi wanaolinda kila siku kwenye mango LA kuingilia hawakuwepo wakati was tukio? Je ni nani Kati ya vichaa Fulani, watu wenye chuki na Tundu Lissu, watu wenye chuki na serikali (false-flag attack), CHADEMA au serikali yenyewe ana mamlaka ya kuondoa walinzi katika eneo LA lindo?
2. Ni nani kati makundi yaliyotajwa hapo juu ana mamlaka ya kuamuru CCTV ambazo zili-record tukio ziondolewe?
3. Kwa nini hata MTU mmoja hajahojiwa wala failing LA uchunguzi halijafunguliwa?

Haya no maswali TAL anauliza kila siku lakini hajajibiwa. Labda wewe unaweza kujaribu.
 
Maswali mazuri sana. Nitajaribu kuyajibu.

Majibu yangu ni DHANA (theories) tu kutokana na hisia zangu.

Sio majibu ya Serikali, Polisi au vyombo vingine vya dola.

Mimi sie msemaji wao.

Samahani majibu yangu yatakuwa marefu kidogo.

Tumekusikia Kifyatu. Kuna maswali 3 ambayo Tundu Lissu amekuwa akiuliza lakini hakuna aliyejitokeza kujibu. Wanaotakiwa kujibu wananyamaza. Hata wewe umekwepa kuyajibu. Si kwamba hujayasikia Bali no kwa kuwa ukijaribu kujibu tu utajikuta unamsonda yule ambaye usingependa aonekane kuwa ndo aliyehusika na jaribio LA mauaji ya Tundu Lissu. Maswali haya no:

1. Kwa nini walinzi wanaolinda kila siku kwenye mango LA kuingilia hawakuwepo wakati was tukio? Je ni nani Kati ya vichaa Fulani, watu wenye chuki na Tundu Lissu, watu wenye chuki na serikali (false-flag attack), CHADEMA au serikali yenyewe ana mamlaka ya kuondoa walinzi katika eneo LA lindo?
Hili swali ni zuri sana.

Simjui aliewaondoa walinzi. Kama walihongwa na CDM waondoke itakuwa rahisi kujua kama walihojiwa na polisi baada ya tukio.

Nahisi wale walinzi sio waajiriwa wa serikali bali ni wa hizi security firms.
Sijui kama mwajiri wao anaisaidia polisi.

Tusichokijua mpaka sasa ni kama walinzi wale wale wanaendelea na kazi pale au wameingia mitini na hawajulikani waliko.

Ubaya mmoja kwetu sisi raia ni kuwa hatujaelezwa ni kipi polisi wanakijua na kipi hawakijui.

Sitegemei polisi watueleze kila kitu wanachokijua.

Hapa ndipo wabunge wetu wangepaswa kuhoji Bungeni.

Unakumbuka kamati ya bunge ilichunguza lakini ripoti yao haikusomwa Bungeni?

Maoni yangu ile ripoti ilikuwa na taarifa nzuri za lile tukio lakini polisi wakaamua kuzuia isitolewe kwanza isijeharibu upelelezi.

Hii pia inaweza kuelezea kwa nini kamera za CCTV ziliondolewa. Nitaelezea hili kwenye swali lako la 2.

Tusikimbilie kusema ni serikali iliwaondoa.
Huu uchunguzi bado mbichi kabisa.

2. Ni nani kati makundi yaliyotajwa hapo juu ana mamlaka ya kuamuru CCTV ambazo zili-record tukio ziondolewe?
Hapa nadhani bila shaka POLISI (wapelelezi) ndio walioziondoa kamera na kuchukua mikanda/media zinazorekodi tukio. Walifanya hivyo siku ya pili baada ya tukio.

Msikilize dereva Bakari alivyosimulia mkasa wote alipokuwa Ubeligiji.


Dereva anasema tokea siku ya shambulizi polisi walizunguusha utepe mpaka siku ya pili. Kamera ziliondolewa siku ya pili.

Sasa tuchukulie ni polisi ndio walioziondoa kamera. Kwa nini?

Kabla ya kuendelea zingatia hili:

Kamera na footage viliondolewa BAADA ya Lissu kushambuliwa na sio KABLA

Hii ina maana viliondolewa kama ushahidi katika upelelezi. Kamera za CCTV zinaacha a unique forensic evidence kwenye mkanda (media) wa picha ilizozirekodi.

Huwezi kughushi/ku-edit picha halafu useme zilipigwa na kamera hii.

Kwa hiyo kama utatumia footage ya shambulio kama ushahidi wa kumtia mtu hatiani, unahitaji kua na kamera iliyopiga hizo picha.

Sina shaka haraka sana walileta kamera nyingine mpya na kuzifunga.

Kama Serikali ingekuwa nyuma ya tukio hili, zile kamera zingeondolewa kabla ya lile shambulizi.

3. Kwa nini hata MTU mmoja hajahojiwa wala failing LA uchunguzi halijafunguliwa?
Hii sidhani kuwa ni kweli.

Uchunguzi ulianza.
[emoji830]Maganda na risasi bila shaka zilikusanywa na polisi kwenye tukio na hospitali.

[emoji830]CCTV kamera na footage wanavyo.

[emoji830]Sio lazima tujue nani kahojiwa. Pengine wamefanya hivyo na wamekusanya majibu kama vielelezo.

[emoji830]Lakini kumbuka, wakati wa shambulizi CCTV zilikuwa zinarekodi.

[emoji830]Dereva alitoka nje ya gari na kujificha uvunguni wakati shambulio linaendelea.

[emoji830]Alisema aliwaona magaidi.

[emoji830]Je hii footage inaonesha nini kingine alichokuwa anakifanya dereva?

Unaona umuhimu wa kumpata dereva asaidie uchunguzi?

Waziri Lugola alisema hakuna uchunguzi.
Hii haimaanishi uchunguzi umesitishwa.

Nina uhakika kabisa wakipata lead mpya, kama ya dereva na Lissu mwenyewe uchunguzi utaendelea.

no maswali TAL anauliza kila siku lakini hajajibiwa. Labda wewe unaweza kujaribu.

Nimejaribu kadri nilivyoweza kuyajibu maswali ya TAL.

Narudia tena.
Hizi ni dhana zangu tu.
Sio majibu rasmi ya Serikali au vyombo vya dola.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ukumbusho tu...wakati wa mauaji ya Mwandishi Daud Mwangosi, msemaji wa Jeshi la Polisi alishawatuhumu Chadema kuhusika! Bahati mbaya kwao picha ikamuonesha polisi akimlipua huyo mwandishi na hivyo Chadema wakapona...isingekuwepo picha, hadi leo viongozi wa Chadema wangekuwa ama wanatumikia kifungo au wamepotezwa.

Daah... Umenikumbusha mbali sana!
Hivi ile ishu ilishia wapi..??
 
Sasa tuchukulie ni polisi ndio walioziondoa kamera. Kwa nini?

Kabla ya kuendelea zingatia hili:

Kamera na footage viliondolewa BAADA ya Lissu kushambuliwa na sio KABLA

Kama Serikali ingekuwa nyuma ya tukio hili, zile kamera zingeondolewa kabla ya lile shambulizi

Basi hao CDM ni hatari sana kama wanaweza kuwatuma watu hadi maeneo nyeti kama yale wakashambulia kwa silaha na baadaye wakarudi kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuondoa zile CCTV kamera ili kupoteza ushahidi..!!
Hivi huoni kuwa katika mazingira kama hayo walinzi walioko maeneo ya makazi ya wabunge na hasa hasa makazi ya naibu spika ni wazembe na hawastahili kuitwa walinzi..??
Katika mazingira hayo... Huoni kuwa jeshi la polisi limedhihirisha kuwa ni la kizembe kuliko maelezo..??
Hivi hujafikiria kuwa labda waliopanga lile tukio walilipanga kizembe zembe kama kawaida yao (make tumeshuhudia wakicheza sinema nyingi sana tena za kizembe zembe)?? Na kuwa hilo wazo la uwepo wa CCTV liliwajia baadaye sana baada ya kugundua kuwa mlengwa hakufa kama walivyokuwa wamekusudia..!??

Anyway; imani yangu inaniambia kuwa Tundu Lissu alipona lile tukio ili kuja kuithibitishia dunia uovu wa wenye madaraka!!
Muhimu kujua ni kuwa Damu ya Binadamu haipotei hivi hivi... Lazima waliohusika wote wataangushwa mmoja baada ya mwingine!!
 
Back
Top Bottom