Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.

1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.

==============================
Baada ya michango mingi iliyowekwa hapa kuna dhana niliyoigusia tu (Internal politics within CHADEMA) na wengi kuuliza kwa nini sikuifafanua. Hapa chini naiongeza ingawaje mwanzoni sikuipa kipaumbele.

Dhana ya 5.
Maadui wa ndani wa CHADEMA walitaka kumuua Lissu ili watimize malengo 3 yafuatayo.

1. Lissu aondoe ushindani katika uchaguzi ujao wa Uenyekiti.

2. Lissu aondoe ushindani katika uteuzi ujao wa mgombea urais ifikapo 2020.

3. Lissu atumiwe kama kafara ili kuipa CHADEMA mvuto na kuonewa huruma na kuichukia serikali katika uchaguzi wa 2020.
Una hoja nzuri ambazo inawezekana ukawa sahihi lakini ikiwa unahisi kuna watu wasioitakia mema serikali ndio wasababishi wa shambulio na si serikali mbona wapinzani walipo hitaji uchunguzi huru ikibidi kutoka vyombo huru mbona serikali haikukubali ikiwa uchunguzi huo ulikuwa unakuja kuwaangamiza hao wabaya wa serikali walioratibu shambulio hilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
waliochukua cctv camera na kuondoa walinzi getini na kuzuia Polisi kuwahoji majirani kuzuia watu kuvaa T-shirt za Tundu Lisu na kuzuia maombi sala dua mbalimbali ndiyo hao walitaka kumuua Tundu Lisu, kwa lugha rahisi ni wewe na wenzako huko CCM
 
Tumekusikia Kifyatu. Kuna maswali 3 ambayo Tundu Lissu amekuwa akiuliza lakini hakuna aliyejitokeza kujibu. Wanaotakiwa kujibu wananyamaza. Hata wewe umekwepa kuyajibu. Si kwamba hujayasikia Bali no kwa kuwa ukijaribu kujibu tu utajikuta unamsonda yule ambaye usingependa aonekane kuwa ndo aliyehusika na jaribio LA mauaji ya Tundu Lissu. Maswali haya no:
1. Kwa nini walinzi wanaolinda kila siku kwenye mango LA kuingilia hawakuwepo wakati was tukio? Je ni nani Kati ya vichaa Fulani, watu wenye chuki na Tundu Lissu, watu wenye chuki na serikali (false-flag attack), CHADEMA au serikali yenyewe ana mamlaka ya kuondoa walinzi katika eneo LA lindo?
2. Ni nani kati makundi yaliyotajwa hapo juu ana mamlaka ya kuamuru CCTV ambazo zili-record tukio ziondolewe?
3. Kwa nini hata MTU mmoja hajahojiwa wala failing LA uchunguzi halijafunguliwa?

Haya no maswali TAL anauliza kila siku lakini hajajibiwa. Labda wewe unaweza kujaribu.
CCM yote ni mbulula hakuna anayeweza kujibu hayo maswali
 
Una hoja nzuri ambazo inawezekana ukawa sahihi lakini ikiwa unahisi kuna watu wasioitakia mema serikali ndio wasababishi wa shambulio na si serikali mbona wapinzani walipo hitaji uchunguzi huru ikibidi kutoka vyombo huru mbona serikali haikukubali ikiwa uchunguzi huo ulikuwa unakuja kuwaangamiza hao wabaya wa serikali walioratibu shambulio hilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Vyombo vya uchunguzi vya Marekani vilifanya upelelezi kwa Siri vikawapata wahusika wote na kumpatia list yote Tundu Lisu pindi akiona inafaa atawaanika kwani wengi ni wakazi wa Dsm walienda kufanya shambulio wakarejea Dsm ingawa wengine wamezawadiwa vyeo wapo mikoani sasa
 
Basi hao CDM ni hatari sana kama wanaweza kuwatuma watu hadi maeneo nyeti kama yale wakashambulia kwa silaha na baadaye wakarudi kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuondoa zile CCTV kamera ili kupoteza ushahidi..!!
Hivi huoni kuwa katika mazingira kama hayo walinzi walioko maeneo ya makazi ya wabunge na hasa hasa makazi ya naibu spika ni wazembe na hawastahili kuitwa walinzi..??
Katika mazingira hayo... Huoni kuwa jeshi la polisi limedhihirisha kuwa ni la kizembe kuliko maelezo..??
Hivi hujafikiria kuwa labda waliopanga lile tukio walilipanga kizembe zembe kama kawaida yao (make tumeshuhudia wakicheza sinema nyingi sana tena za kizembe zembe)?? Na kuwa hilo wazo la uwepo wa CCTV liliwajia baadaye sana baada ya kugundua kuwa mlengwa hakufa kama walivyokuwa wamekusudia..!??

Anyway; imani yangu inaniambia kuwa Tundu Lissu alipona lile tukio ili kuja kulithibitishia dunia uovu wa wenye madaraka!!
Muhimu kujua ni kuwa Damu ya Binadamu haipotei hivi hivi... Lazima waliohusika wote wataangushwa mmoja baada ya mwingine!!
Tatizo watu wanaotumwa kuja Mitandaoni kuitetea serikali ya wasukuma wawili makatili huwa hawatafakari kabla ya kuandika hujiandikia tu hovyo hovyo kisha kuchukua posho na kuondoka lakini baadae wakisoma majibu ya watanzania wenye weledi na upeo hukaa na kujutia umbulula wao na tayari wamegundua Tanzania ya sasa si ile ya zamani ya kutengeneza mazingira ya kuwabambikia kesi wau kirahisi
 
Vyombo vya uchunguzi vya Marekani vilifanya upelelezi kwa Siri vikawapata wahusika wote na kumpatia list yote Tundu Lisu pindi akiona inafaa atawaanika kwani wengi ni wakazi wa Dsm walienda kufanya shambulio wakarejea Dsm ingawa wengine wamezawadiwa vyeo wapo mikoani sasa
wanaficha camera huku kila kitu kiko wazi !
 
Wasalaam, naomba kuuliza kwa upole kabisa ni wakinanani walishiriki katika jaribio kuua mbunge ambaye ni muwakilishi wa wanasingida na watanzania kwa ujumla? Ni nani watu wasiojulikana? Maana bado wapo na hawajajulikana. Je lissu akirudi nyumbani Tanzania Leo si atakutananao tena watu wasiojulikana maana hawajakamatwa kwasababu hawajulikani. ( watu wasiojulikana)
 
Mkuu walisema ni watu wasiojulikana na bado hawajajulikana hadi Leo hii
Wacha kujitoa ufahamu ndugu haihitaji akili ya darasani kuwajua, we angalia wanaotokwa povu kwa kupona kwake kisha tafuta boss wao na wapambe wake usipowajua na wewe utakua hamnazo. ila ukiwajua urudi hapa nikupe like.
 
Back
Top Bottom