Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Lisu alilaza kiti akalala kifudi fudi huko kulala alisaidiwa na dereva wake mwenyewe ndo maana ya ile bond unayoiona Kati ya Lissu na dereva wake. Over

Kama alilaza kiti zile risasi zingepitiliza na kumpiga dereva. Tafadhali angalia picha ya lile gari uone risasi zilipigwa wapi!! Ni dirishani na kwenye mlango kwa juu, yaani chini kidogo ya dirisha. Maana yake ni kuwa Mhe. Lisu asingepigwa risasi hata moja.

Queen Esther
 
Alimlaza kwenye kiti chake??duuh.Mimi nafikiri kama alipata muda wa kumlaza kwenye kiti basi alitakiwa atoke naye mlangoni eidha kwa kumvuta kuelekea chini!!halafu alimlazaje??Hivi gari za wabunge zina viti vya Ku roll up and down??hahahaaa!!yani unamlaza mwenzio (sijui kwa tekniki IPI)bado we we hupati hata kajeraha hata kidogo??
 
Alimlaza kwenye kiti chake??duuh.Mimi nafikiri kama alipata muda wa kumlaza kwenye kiti basi alitakiwa atoke naye mlangoni eidha kwa kumvuta kuelekea chini!!halafu alimlazaje??Hivi gari za wabunge zina viti vya Ku roll up and down??hahahaaa!!yani unamlaza mwenzio (sijui kwa tekniki IPI)bado we we hupati hata kajeraha hata kidogo??
Ndg yangu Zalemda kuna mambo ya ajabu sana hapa. Yaani kwa maelezo yao ina maana walipaki gari wakaanza kulazana vitini wakati huo mwenye bunduki anawasubiri tena Ak 47 anawasubiri wamalize kulazana.

Queen Esther
 
Hivi mtu akiwa kushoto hawezi kulenga mguu wa kushoto?


Hivi mtu hawezi kuweka miguu ili asipigwe kichwa.
 
Pamoja tofauti/chuki za kiitikadi,mwisho wa siku tuwe na hofu ya Mungu na UBINADAMU. Kwa risasi zilizotolewa ndani ya mwili wake,inatosha kutambua ukubwa wa tukio na namna Mungu alivyosimama upande wake. Badala ya kuhoji (kwa KEJELI) mguu upi ulipaswa upigwe risasi,tuhoji ASKARI wa lindo walikuwa wapi siku ile? CCTV CAMERA imeenda wapi? Ni kweli tunahitaji uwepo wa DEREVA wake kukamilisha upelelezi? Kama vyombo vya ulinzi na usalama (polisi) vimeshindwa kutuletea MAJIBU,basi tumuache Lisu apumzike badala ya kumsimanga na kumkejeli.
Hizo risasi uliziona?
 
Hivi mtu akiwa kushoto hawezi kulenga mguu wa kushoto?


Hivi mtu hawezi kuweka miguu ili asipigwe kichwa.

Kwa namna gari lilivyochakazwa na risasi labda zilikuwa zinapiga kona.

Suala la kuweka miguu ili usipigwe kichwa ni jipya hilo!! Kwa mlio na kishindo cha AK 47 hivi unaweza kweli kuyafanya hayo? Labda hujawahi kusikia kishindo hicho cha risasi inapofyatuliwa.

Queen Esther
 
JF ni Jukwaa la kipekee Tz na lina watu wenye weledi mbalimbali.

Naomba mnisaidie kuelewa mambo yafuatayo:-
1. Picha ya gari lililopigwa risasi kumshambulia Tundu Lissu linaonesha risasi zimepigwa mlango wa kushoto.

2 Mguu ulioumia ni wa kulia..

3. Risasi zimepiga kioo, sasa ina maana Tundu Lissu aliinua mguu kwenye dirisha?

4. Yeye mwenyewe anasema alilaza kiti!! Hizi risasi zilipita wapi?

5. Dereva yupo wapi atusaidie hili.

Karibuni wataalamu tudadavue.

Queen Esther

JF ni Jukwaa la kipekee Tz na lina watu wenye weledi mbalimbali.

Naomba mnisaidie kuelewa mambo yafuatayo:-
1. Picha ya gari lililopigwa risasi kumshambulia Tundu Lissu linaonesha risasi zimepigwa mlango wa kushoto.

2 Mguu ulioumia ni wa kulia..

3. Risasi zimepiga kioo, sasa ina maana Tundu Lissu aliinua mguu kwenye dirisha?

4. Yeye mwenyewe anasema alilaza kiti!! Hizi risasi zilipita wapi?

5. Dereva yupo wapi atusaidie hili.

Karibuni wataalamu tudadavue.

Queen Esther
It seems like you among the members of Black Propaganda or Characters Assassination teams' campaigners
 
It seems like you among the members of Black Propaganda or Characters Assassination teams' campaigners

Hebu soma hapo chini bandiko la JF member mwingine aitwaye Kaka Pacal Mayala, labda utanielewa.

Mhe. Tundu Lissu,
Kwanza pole sana kwa yaliyokusibu.
Umezungumza mengi kuhusu kilichotokea mwaka mmoja uliopita, ila watu wanaohoji kuhusu dereva wako, nakuomba sana usiwaite wajinga, au wametumwa, kwa sababu mashaka yao ni very valid.

Kwa vile mashuhuda ni nyinyi wawili tuu, wewe na dereva wako, then kuna mambo tungependa kujua kutoka kwa Lissu mwemyewe na dereva wake.

Hoja kuwa tumetoka naye mbali hivyo tunaaminiana, hazina mashiko mbele ya watu na kazi zao. Lissu alipotoka na dereva wake, anaweza kujilinganisha Dr. Slaa na mlinzi wake Kagenzi walipotoka?, halafu what happened?!. Kwenye mambo ya assignment, anaweza hata akatumika mke wako aliyekuzalia wanao, sembuse itakuwa dereva tuu mliotoka nae mbali!.
Baadhi ya maswali ni haya...
Kwa vile Lissu aliwahi kuripoti kufuatiliwa, kupitia press conference, kwa nini hakuripoti polisi?!.

Baada ya Chadema kupokea taarifa ya Mnadhimu wake kufuatiliwa, walichukua hatua gani?.

Baada kuona kuna gari linawafuatilia, mlichukua hatua gani?.

The common sense ya kufuatiliwa inaelekeza, uki note you're followed, hatua ya kwanza ni kumpote anaye kufollow kwa makusudi, ili kwanza kujiridhisha kuwa anakufollow.

Ukiisha jiridhisha you are followed, una change direction kumpoteza maboya.
Ukimuona bado yupo, then kama uko fit, unamlengesha mahali kwenye kona ambapo hawezi kuchomoka, mnamalizana!.

Kama hauko fit, unamlengesha kwenye safe area ,usually sehemu open kwenye makundi ya watu na kumripoti kunakohusika.

Baada ya kuona mnafuatwa, kwa nini mliendelea kuelekea nyumbani?.
Mlipofika mkasimama, mkawaona watu wawili wanashuka na AK 47, kitendo tuu cha kujua tuu bunduki zile ni AK 47, hii maana yake ni close proximity, kwenye shooting that close!, risasi 38!, dereva huyu amesalimikaje asipitiwe hata na moja?.

(Mimi niliwahi kuwa mwanajeshi wa JWTZ hivyo kuna kitu nakijua kuhusu hizi AK47 ndani ya jeshi letu, lakini vitu vingine ni siri za usalama wa taifa letu, sina uhakika mtu asiyepitia JWTZ, ana uwezo gani kuijua AK 47!.)

Ametokaje kwenye gari na kujificha chini ya gari ya jirani bila kugundulika?!.
Anafichwa nini kuhojiwa?, kuna nini kinafichwa?.

Maswali haya yameendelea kwa msaada wa mwana jf huyu
Dr Akili said:
Hata kama wangemuhoji huko Nairobi au Ubeligiji angesema hayo hayo ambayo amekuwa akiyasema kwenye social media na vyombo vingine vya habari kila mara ambayo hayana msaada wo wote wa kuwanasa hao assailant wake.
[*]Kwa dalili zo zote dreva wake ni suspect number one.

Bunduki iliyotumika waliiona ni AK 47 iliyokuwa na full magazine (risasi 40) ambayo ilimimina risasi zote 40 at close range. Kati ya hizo 17 zilizama kwenye miguu, mikono na kiuno cha Tundu Lissu.
Risasi zilimiminwa kutoka upande wa kulia wa gari ambao ni upande wa dreva lakini dreva hakupatwa na risasi hata moja na alipata hata fursa ya kuteremka kwenye gari na kwenda ku take cover kwenye magari yaliyokuwa yamepaki eneo hilo. Assailants walikuwa upande wa kulia wa gari, hivyo risasi zilizama zaidi kwenye mguu wa kulia, paja la kulia, mkono wa kulia, kiuno upande wa kulia na kutokea tumboni na mkono wa kushoto.

These are the documented medical forensic clues.
Majeshi yetu hayana bunduki za AK 47, yana SMG badala yake ambayzo full magazine zake ni risasi 30. Bunduki za AK47 zinamilikiwa na majambazi yanazozipata kutoka kwa wanajeshi wa Burundi wanaokimbilia Tanzania ambao huwa wanaziuza kwa bei ya shillingi 20,000 tu!! Silaha hizi ndizo zilitikisa huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

Hakuna mwanajeshi ye yote (aliyepata mafunzo ya kijeshi) ambaye ampige mtu (adui) risasi 38 from an AK 47 gun at a close range halafu mtu huyo asalimike!! Never on earth. Kwanza atahitaji risasi moja tu na atafumua kichwa au moyo.

Hivyo it is so obvious kwamba assailants wa Tundu Lissu walikuwa ni wahuni tu wa mitaani wasiojua kutumia bunduki. Yaani risasi 38 zote zinakosa target (kichwa au moyo) zinaishia kupiga makalio na hewa!! Hili halihitaji askari wa Scotland yard kulitambua.

Swali ni nani aliwakodi hawa wahuni wasiojua shabaha? Kwa nini dreva wa Lissu akawa mkimbizi nchi za nje? Nini kakimbia? Kwani hata polisi wetu wakienda kumhoji huko kwani atasema lo lote la maana? Huko hawawezi kumu arrest. Alipaswa kuwa behind bars ili aeleze vizuri. Tundu Lissu alipaswa kujua hili. Mara nyingi kikulacho unacho nguoni mwako. Eti ninamuamini sana. Mbele ya pesa kunakuamini mtu? Yaani apewe shillingi million 500 aache kukumaliza? Yaani Tundu Lissu hajui kwamba "Money is the source of all evils in this world?"

Hospitali ya serikali ya Dodoma na madaktari wa serikali wa Dodoma hospital ndiyo waliookoa maisha yake. Kama serikali ilikuwa na mpango wa kumuua, ingalishindwaje kumumalizia hapo hapo kwenye hospitali yake ya Dodoma humo humo operation theatre?

It was so simple eg hiyo damu aliyopewa hangeipata au angalipewa incompatible blood ambayo ingalimumaliza hapo kwa hapo! Lazima aishukuru serikali kwa kuokoa maisha yake badala ya kuilaumu. Upinzani haupaswi kuwa wa aina hii. Tujifunze kwenye nchi zilizotutangulia.
Bunduki kama AK 47 au SMG ikiunguruma si mchezo.

Kwa askari yo yote trained, hata kama naye ana bunduki ya aina hiyo hiyo lakini kashutikizwa, reaction ya kwanza ni ku take cover. Atalala chini na ku craw hadi mahala salama. Hapo ndipo atatafuta kuona adui/ maadui walipo na kutafakari kama anao uwezo wa kupambana nao au kuomba reinfocement au kutokomea kabisa kwenye eneo hilo. Trained soldier hakurupuki tu kuanza kurusha risasi ovyo ovyo anapositukizwa na milio ya risasi.

Hivyo kwa jinsi tukio lilivyotokea hapo usingalitarajia askari waliokuwa karibu na eneo hilo kuwa wangaliweza kuanza kujibu mapigo kwa muda huo mfupi uliotumika kabla ya majambazi hayo kutokomea kusikojulikana. Dreva wa Lissu aliyaona live na alitaja hata aina ya gari yalilotumia na plate namba zake. Polisi walikamata magari kadhaa ya aina hiyo lakini dreva huyo alikataa kwenda kuyatambua na hivyo yakabidi yaachiwe kwani hakuna shahidi aliyejitokeza.

Shahidi muhimu alikuwa Nairobi akidaiwa anapata tiba ya kisaikolojia. Sasa hivi Lissu anasema dreva huyo yuko masomoni Ubeligiji. Sijui anasoma digrii gani hapo Leuven University teaching hospital anapotibiwa boss wake. Jamani aacheni kutufanya wajinga. Pascal yuko sahihi kabisa.

Huko nyuma niliisha wahi kuzungumza haya kuhusu dereva wa Lissu.


Pascal Mayalla
 
Bas
Kwa namna gari lilivyochakazwa na risasi labda zilikuwa zinapiga kona.

Suala la kuweka miguu ili usipigwe kichwa ni jipya hilo!! Kwa mlio na kishindo cha AK 47 hivi unaweza kweli kuyafanya hayo? Labda hujawahi kusikia kishindo hicho cha risasi inapofyatuliwa.

Queen Esther
iBasi amini nakuambia inawezekana kulenga risasi mguu wa kulia ukiwa kushoto.
 
Kama kweli ameumia mguu wa kulia kweli inafikirisha kwani kwa magari yanayotumika Tanzania dereva hukaa upande wa kulia na anayemuendesha kushoto. Labda kama alikaa nyuma ya dereva, kama alikaaa mbele mhh
Na ni Tanzania hapa hapa yalo magari mengi tu dereva anakaa kushoto.
 
Hizi nondo huwa hawataki kabisa kuzisikia. Wao walichokaririshwa ni CCTV, Mlinzi sijui serikali basi.
 
Kwa namna gari lilivyochakazwa na risasi labda zilikuwa zinapiga kona.

Suala la kuweka miguu ili usipigwe kichwa ni jipya hilo!! Kwa mlio na kishindo cha AK 47 hivi unaweza kweli kuyafanya hayo? Labda hujawahi kusikia kishindo hicho cha risasi inapofyatuliwa.

Queen Esther
Ukisikiliza story za hawa jamaa utajiuliza wanaakili timamu au mazombie?Utasiki dereva akalaza kiti then akaruka na kujificha chini ya gari hahahahahahah.
 
Alimlaza kwenye kiti chake??duuh.Mimi nafikiri kama alipata muda wa kumlaza kwenye kiti basi alitakiwa atoke naye mlangoni eidha kwa kumvuta kuelekea chini!!halafu alimlazaje??Hivi gari za wabunge zina viti vya Ku roll up and down??hahahaaa!!yani unamlaza mwenzio (sijui kwa tekniki IPI)bado we we hupati hata kajeraha hata kidogo??
Hayo ni maelezo niliyoona gazeti limemnukuu hata mimi siwezi kujua zaidi ya hapo
 
Ebu iweni watu wenye utu kidogo. Izo propaganda, hazina maana, wala hazisaidii kitu katika kumfanya apone. Alishaumizwa, amekaa katika mateso kwa miaka almost 2. Hoja, ni kwamba, ameumizwa, sio upuuzi wa sijui risasi ziliingia, sijui kutoka, mara kulia mara kushoto. Lakini katika yote, tukumbuke kwamba, we cant escape from the consequences of actions, its just a matter of time.
 
Back
Top Bottom