Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Serikali haiwezi kukosa kujua liye fanya haya Mashambulizi, POLICE, Mgambo, jeshi, TISS hao woote washindwe? na wasijue? km mjeda anavamiwa tu mtaani lkn anaamua kumsaka mbaya wake na wenzake tena kirahisi kabisa, sembuse kwa nchi?
 
1. Ni nani aliyemnyima TL hela ya matibabu wakati akiwa mahututi?
2. Nani alimvua ubunge wakati akiwa bado akiendelea na matibabu
3. Nani aliwatoa wale maaskari wa zamu siku ya shambulio?
4. Nani alitoa amri ya line clear barabarani baada ya wahalifu kumaliza kumtwanga risasi Lissu?

5. Ni nani alitoa CCTV cameras baada tu ya shambulio kupoteza ushahidi?

Tuanzie hapo kwanza!!
wew ndiye unahusika?
 
Umetumia mbinu tunayoiita Analysis for Competitive Hypothesis ACH, Ila umekosa matrices zinazochuja validity ya dhana zako hizo.
 
Habari wakuu, leo nafikia ukomo wa kiu yangu ya kutaka kuueleza ukweli umma wa watanzania kupitia jukwaa la siasa la JF.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu na ikizingatiwa kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakilitumia tukio la kupigwa risasi kwa aliyekuwa mbunge wa Singida mashariki, Rais wa TLS na sasa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, Tundu Antipas Lissu kama ajenda ya kuombea kura huku wengi wakiituhumu serikali ya Tanzania kuhusika na ' jaribio hilo la kumwua' Lissu.

Jambo kubwa la kujijliza ni kuwa kwanini Lissu alipigwa risasi? Kwanini mpaka sasa hakuna mtu anayetuhumiwa na tukio hilo? Kwanini Lissu hashughuliki na kufungua jalada/shauri katika vyombo vya dola vyenye dhamana ya kulinda usalama wa taifa letu?

Haya yote yana maelezo niliyoyapata kutoka vyanzo tofauti vya kuaminika.

Ikumbukwe kuwa wakati tukio hilo linatokea nchi ilikuwa katika kipindi cha sintofahamu juu ya ujio wa ndege iliyokuwa imezuiwa na wadeni wa taifa, pia mvutano kati ya kampuni ya ACACIA mining PLC na serikali juu ya sakata la makinikia. Ni dhahiri kuwa haya yote yalikuwa mzigo mzito kwa serikali ya CCM iliyotaka kujiimarisha kisiasa.

Mbali na kuwa haya yalikuwa yakitokea Lissu hakusita 'kupiga spana' kwa serikali aliyokuwa akiipinga. Kimsingi mwenendo wa matukio ya wakati huo yaliashiria kuhusika kwa serikali katika shambulizi la Lissu lakini ukweli ni huu hapa: Tundu Lissu alikuwa akikaririwa kuwatetea wadeni na ACACIA MINING PLC, huku akitumia taaluma yake ya sheria na weledi wake wa kuwasilisha hoja kuendelea kuikandia serikali.

Alienda mbali zaidi hata kuzitaka nchi wahisani kusitisha misaada nchini na kuomba Tanzania iwekewe vikwazo na nchi hizo. Kufuatia jitihada zake hizo kukwama ndipo tukio la kupigwa risasi 16 likatokea. Naufahamisha umma kuwa Lissu alijaribu kukutana na viongozi waandamizi wa jumuiya ya wawekezaji wa kigeni wa madini nchini na kuingia makubaliano ya kutoa msaada kuhakikisha kuwa mkakati wa udhibiti wa biashara za madini nchini uliokuwa ukitekelezwa na serikali unakwama kupitia upinzani.

Kwa bahati mbaya au nzuri mkakati huo ulishindikana kuzuilika kwa mujibu wa makubaliano aliyoyafanya Lissu na wabia wake hao. Alilipwa kiasi cha fedha kutokana na makubaliano ya awali na wabia wake hao walitakiwa kumlipa 10% ya faida ya madini itakayokuwa inapatikana kwa miaka kumi kama mpango huo ungekamilika.

Ziko taarifa pia watu wanaomwezesha kiuchumi katika uchaguzi huu wamesaini makubaliano kama hayo ikiwa atashinda Urais mwaka huu. Baada ya mpango huo kukwama ndipo bodi ya wakurugenzi wa baadhi ya makampuni ya kigeni ya madini nchini walipojitoa katika makubaliano hayo na kuandaa shambulizi dhidi ya Lissu. Na hapo ndipo serikali iliposhindwa kutoa ushirikiano baada ya kuanza kusakamwa na kutuhumiwa katika shambulizi hilo.

Ili kupata kuelewa mwenendo wa matukio hayo, mambo yafuatayo yanafaa kuzingatiwa:

1. Kwanini Serikali haikumshambulia Dr. Wilbroad Slaa wakati wa vuguvugu la Richmond?

2. Kwanini Serikali haikumshambulia Freeman Mbowe wakati ikitekeleza malipo kwa DOWANS?

3. Kwanini Serikali haijazuia passport ya kusafiria ya Lissu alipokuwa akizunguka nchi kadhaa duniani huku akiipinga Serikali ya Magufuli?

Kwakweli haya yote yangewezekana kutekelezeka kwa namna yoyote lakini hayakufanyika.
U mean dia mengi lakini hukujiuliza kwa nini?

1. Cctv camera ziliondolewa baada ya tukio.
2. Walinzi siku ya tukio katika eneo lenye ulinzi muda wote hawakuwepo?
3. Kila lilikuwa linataka kufanywa kwa ajili ya lissu kama kuombewa dua,kumchangia damu, t-shirt zenye jina "pray for Lissu" serikal ili zilipiga marufuku?
 
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.

1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.

==============================
Baada ya michango mingi iliyowekwa hapa kuna dhana niliyoigusia tu (Internal politics within CHADEMA) na wengi kuuliza kwa nini sikuifafanua. Hapa chini naiongeza ingawaje mwanzoni sikuipa kipaumbele.

Dhana ya 5.
Maadui wa ndani wa CHADEMA walitaka kumuua Lissu ili watimize malengo 3 yafuatayo.

1. Lissu aondoe ushindani katika uchaguzi ujao wa Uenyekiti.

2. Lissu aondoe ushindani katika uteuzi ujao wa mgombea urais ifikapo 2020.

3. Lissu atumiwe kama kafara ili kuipa CHADEMA mvuto na kuonewa huruma na kuichukia serikali katika uchaguzi wa 2020.
Ni yule yule aliyetaka kumuua Nape Nnauye
 
U mean dia mengi lakini hukujiuliza kwa nini?

1. Cctv camera ziliondolewa baada ya tukio.
2. Walinzi siku ya tukio katika eneo lenye ulinzi muda wote hawakuwepo?
3. Kila lilikuwa linataka kufanywa kwa ajili ya lissu kama kuombewa dua,kumchangia damu, t-shirt zenye jina "pray for Lissu" serikal ili zilipiga marufuku?
Ziko taarifa kuwa walinzi na waangalizi wa CCTV camera walinunuliwa kabla ya tukio.
 
Habari wakuu, leo nafikia ukomo wa kiu yangu ya kutaka kuueleza ukweli umma wa watanzania kupitia jukwaa la siasa la JF.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu na ikizingatiwa kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakilitumia tukio la kupigwa risasi kwa aliyekuwa mbunge wa Singida mashariki, Rais wa TLS na sasa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, Tundu Antipas Lissu kama ajenda ya kuombea kura huku wengi wakiituhumu serikali ya Tanzania kuhusika na ' jaribio hilo la kumwua' Lissu.

Jambo kubwa la kujijliza ni kuwa kwanini Lissu alipigwa risasi? Kwanini mpaka sasa hakuna mtu anayetuhumiwa na tukio hilo? Kwanini Lissu hashughuliki na kufungua jalada/shauri katika vyombo vya dola vyenye dhamana ya kulinda usalama wa taifa letu?

Haya yote yana maelezo niliyoyapata kutoka vyanzo tofauti vya kuaminika.

Ikumbukwe kuwa wakati tukio hilo linatokea nchi ilikuwa katika kipindi cha sintofahamu juu ya ujio wa ndege iliyokuwa imezuiwa na wadeni wa taifa, pia mvutano kati ya kampuni ya ACACIA mining PLC na serikali juu ya sakata la makinikia. Ni dhahiri kuwa haya yote yalikuwa mzigo mzito kwa serikali ya CCM iliyotaka kujiimarisha kisiasa.

Mbali na kuwa haya yalikuwa yakitokea Lissu hakusita 'kupiga spana' kwa serikali aliyokuwa akiipinga. Kimsingi mwenendo wa matukio ya wakati huo yaliashiria kuhusika kwa serikali katika shambulizi la Lissu lakini ukweli ni huu hapa: Tundu Lissu alikuwa akikaririwa kuwatetea wadeni na ACACIA MINING PLC, huku akitumia taaluma yake ya sheria na weledi wake wa kuwasilisha hoja kuendelea kuikandia serikali.

Alienda mbali zaidi hata kuzitaka nchi wahisani kusitisha misaada nchini na kuomba Tanzania iwekewe vikwazo na nchi hizo. Kufuatia jitihada zake hizo kukwama ndipo tukio la kupigwa risasi 16 likatokea. Naufahamisha umma kuwa Lissu alijaribu kukutana na viongozi waandamizi wa jumuiya ya wawekezaji wa kigeni wa madini nchini na kuingia makubaliano ya kutoa msaada kuhakikisha kuwa mkakati wa udhibiti wa biashara za madini nchini uliokuwa ukitekelezwa na serikali unakwama kupitia upinzani.

Kwa bahati mbaya au nzuri mkakati huo ulishindikana kuzuilika kwa mujibu wa makubaliano aliyoyafanya Lissu na wabia wake hao. Alilipwa kiasi cha fedha kutokana na makubaliano ya awali na wabia wake hao walitakiwa kumlipa 10% ya faida ya madini itakayokuwa inapatikana kwa miaka kumi kama mpango huo ungekamilika.

Ziko taarifa pia watu wanaomwezesha kiuchumi katika uchaguzi huu wamesaini makubaliano kama hayo ikiwa atashinda Urais mwaka huu. Baada ya mpango huo kukwama ndipo bodi ya wakurugenzi wa baadhi ya makampuni ya kigeni ya madini nchini walipojitoa katika makubaliano hayo na kuandaa shambulizi dhidi ya Lissu. Na hapo ndipo serikali iliposhindwa kutoa ushirikiano baada ya kuanza kusakamwa na kutuhumiwa katika shambulizi hilo.

Ili kupata kuelewa mwenendo wa matukio hayo, mambo yafuatayo yanafaa kuzingatiwa:

1. Kwanini Serikali haikumshambulia Dr. Wilbroad Slaa wakati wa vuguvugu la Richmond?

2. Kwanini Serikali haikumshambulia Freeman Mbowe wakati ikitekeleza malipo kwa DOWANS?

3. Kwanini Serikali haijazuia passport ya kusafiria ya Lissu alipokuwa akizunguka nchi kadhaa duniani huku akiipinga Serikali ya Magufuli?

Kwakweli haya yote yangewezekana kutekelezeka kwa namna yoyote lakini hayakufanyika.
Waliomshambulia Lissu Kwa maelekezo toka juu ni:
1. Paul Makonda
2. Mwigulu Nchemba
3. Job Ndugai
 
Waliomshambulia Lissu Kwa maelekezo toka juu ni:
1. Paul Makonda
2. Mwigulu Nchemba
3. Job Ndugai
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.

1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.
Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.

==============================
Baada ya michango mingi iliyowekwa hapa kuna dhana niliyoigusia tu (Internal politics within CHADEMA) na wengi kuuliza kwa nini sikuifafanua. Hapa chini naiongeza ingawaje mwanzoni sikuipa kipaumbele.

Dhana ya 5.
Maadui wa ndani wa CHADEMA walitaka kumuua Lissu ili watimize malengo 3 yafuatayo.

1. Lissu aondoe ushindani katika uchaguzi ujao wa Uenyekiti.

2. Lissu aondoe ushindani katika uteuzi ujao wa mgombea urais ifikapo 2020.

3. Lissu atumiwe kama kafara ili kuipa CHADEMA mvuto na kuonewa huruma na kuichukia serikali katika uchaguzi wa 2020.
Libashite na baba yake
 
Waliomshambulia Lissu Kwa maelekezo toka juu ni:
1. Paul Makonda
2. Mwigulu Nchemba
3. Job Ndugai
Huyo Job Ndugai hakushirikishwa kabisa kuhusu tukio, hata CCM hawakujua.

Ndio maana aliunda mpaka tume ya kibunge kwaajili ya uchunguzi.

Ila alivyojua Jiwe ndio mastermind akanywea na hivyo kuanza kutumia nguvu kuuubwa kujipendekeza kwa Jiwe.

Hata Mwigulu hakushirikishwa
 
Kumbe ni Makonda na babake !
 
ndammu,

..msikilize Mwigulu Nchemba mpaka mwisho.

..sikiliza hapo alipoulizwa kuhusu walinzi wa area D.

Habari wana JF,

Hivi kati ya hawa watano tukiachana na story za kufikirika na za vijiweni ni nani hasa alihusika na shambulio la Tundu Lissu?

Binafsi nimemuelewa Tundu Lissu hataki kurudi nchini inawezekana kabisa hajui adui yake halisi ni nani.

sasa kati ya hawa mwenye maelezo ya kutosha amtoe wasiwasi Tundu Lissu ili arudi Tanzania:-

1. Vibaka au Majambazi kwa ajili ya kutaka Mali

2. Serikali ya Awamu ya tano ikiongozwa na Hayati JPM kwa ajili ya faida za kisiasa au Maendeleo ya Nchi kwamba alikuwa kikwazo

3. CHADEMA ili kuchafua Serikali kwa faida ya kisiasa au migogoro Chamani

4. WanaCCM wasiokuwa wanapenda kinachoendelea Awamu ya Tano na Uongozi wa JPM

5. Wengineyo ,kama kwa ajili ya wivu wa kimapenzi na n.k

Ni nani hasa? Ujue kwenye Siasa kuna mambo mengi unaweza aminishwa kitu kumbe ni Propaganda tu.
 
Back
Top Bottom