Ni nani anastahili kuwa MwanaJamiiForums bora wa mwaka?

Ni nani anastahili kuwa MwanaJamiiForums bora wa mwaka?

Nani Mwana JamiiForums bora wa mwaka kati ya hawa?

  • The Boss

  • Faiza Foxy

  • Mzee Mwanakijiji

  • BAK

  • Pasco

  • Heaven Sent

  • Victorie

  • Technically

  • Mshana Jr

  • Lizaboni

Results are only viewable after voting.
Ni vigumu sana kumpata mwana JF bora wa mwaka kwa ujumla kama huu.

Nafikiri kila jukwaa lingekuwa na wagombea wake.
Kwa mfano
Jukwaa la siasa angegombea Technically, Lizaboni, na Mwanahabari huru, The Boss

Jukwaa la Intelligence angegombea MSEZA MKULU, The bold, na I am the winner.

International angegombea BAK, RUCCI, na Ipycalypse

Habari mchanganyiko angegombea mshana jr, chinchilla coat na GENTAMYCINE.

Chit-chat hili halina mpinzani linaenda kwa makapuku forums kwa ujumla kama lilivyo

JF Celbs. warumi, hans Mtanashati, na brave one....wagombee.

MMU nimeshindwa kuweka wagombea.

JF sports @prondo, Mentor Nifah

JF Doctor hili jukwaa atagombea Sky Eclat peke yake maana hakuna mgombea mwingine.

JLM hapa watagombea fakalava Shunie na Ambiele Kiviele

NB huu mfano ni kwa mtazamo wangu mwenyewe.....lakini ndivyo tulitakiwa kuwapata wana JF bora.

Huwezi kusema mtu mmoja atwae tuzo wakati JF ina majukwaa mengi na kila jukwaa lina manguli wanaolitendea haki.
Exactly..
Uimeongea ukweli mtupu. Hakika hii thread ni batili.
Jamii forum futeni huu uzi maana haujatendendea haki majukwaa
 
UPDATES
KUTOKANA NA MAONI YA WADAU , TUMEMUONGEZA MSHANA JR, NA HEAVEN SENT, WATACHUKUA NAFASI ZA , OCAMPOR , NA MISS NATAFTA, NIMEJARIBU KUEDIT KWENYE POLL NIMESHINDWA, MODS WATANISAIDIA. HII KITU NI SERIOUS KABISA, mods saidia ku edit kwenye polls mtoen miss natafta na ocampor,muweke mshana jr na heaven sent

Habari zenu wakubwa,

Matumaini yetu ni kuwa nyote ni wazima wa afya na mnaendelea vema na shughuli zenu ili kuepuka kusoma namba.

Malengo ya uzi huu ni kuweka utaratibu wa kuweza kupata mwanaJF bora wa mwaka hasa jukwaa la siasa, mambo ya kimataifa na mengineyo.

Mambo yafuatayo ndiyo vigezo vitakavyotumika kumpata...
1. Mwenye hoja na uchambuzi mzuri wa masuala yanayohusu taifa letu kwa ujumla
2. Anayechambua mambo ya kisiasa kwa wigo sawa bila kuegemea au kupendelea upande wowote ule, kaka ni CHADEMA au CCM au CUF yuko tiyari kukosoa kwa hoja haijarishi ni chama chake
3. Mwenye nidhamu juu ya majibu anayowapa wengine na mwenye kujibu bila kubagua au kukejeli wengine na kuwadharau au kuwatamkia matusi(makosa yanayopelekea ban)
4. Mwenye michango mingi ya kuelimisha jamii,
5. Asiye mdini au mkabila wala asiyechanbua kwa kupendelea kabila/dini yake na kukashfu za wengie,
6. Mwenye kuheshimu wengine na mamlaka ya nchi haijarishi kamchagua kiongozi aliyeko madarakan au lah.

Orodha yangu ni kama ifuatavyo, ninyi ndio mtapiga kura kwenye poll na kupata mshindi.
1. The Boss
2. Faiza foxy
3. Mzee mwanakijiji
4. BAK
5. Lizaboni
6. Pasco
7. Heaven sent
8. victorie
9. Technically
10.Mshana jr

Haimaanishi ambao hawajawekwa hawakuchangia hapana wamechangia sana ila kwa mwaka huu hawakufika viwango vya hawa hapa

PIGA KURA YAKO.
HAPANAAAAAAAAAAAAAAAAAAAH...Narudia tena HAPANAAAAAAAA....NO..NO..NO...!!!!

Kwanini mumuache The bold huyu kijana anajitahidi kwakweli amekidhi vigezo vyote vya hapo juu...

LIST NI HII:

1:The bold

2:Mzizi mkavu

3:The Boss

4:Chief Mkwawa

5:Mshana jr

Toshaaaa narudia TOSHAAA (in capital letters)
 
Inategemeana na category maana humu karibu kila mtu comments zake ni unilateral au partisan, ktk list hapo juu nitampa kura @Pasco sababu anang'ata na kupuliza pande zote at the same time, The Boss anakaribia kidogo. Wengine hapo ktk orodha wameshindwa kabisa kuficha mahaba yao eidha ya kichama, au kiimani, au kimuziki, au kimichezo etc.
 
Ni vigumu sana kumpata mwana JF bora wa mwaka kwa ujumla kama huu.

Nafikiri kila jukwaa lingekuwa na wagombea wake.
Kwa mfano
Jukwaa la siasa angegombea Technically, Lizaboni, na Mwanahabari huru, The Boss

Jukwaa la Intelligence angegombea MSEZA MKULU, The bold, na I am the winner.

International angegombea BAK, RUCCI, na Ipycalypse

Habari mchanganyiko angegombea mshana jr, chinchilla coat na GENTAMYCINE.

Chit-chat hili halina mpinzani linaenda kwa makapuku forums kwa ujumla kama lilivyo

JF Celbs. warumi, hans Mtanashati, na brave one....wagombee.

MMU nimeshindwa kuweka wagombea.

JF sports @prondo, Mentor Nifah

JF Doctor hili jukwaa atagombea Sky Eclat peke yake maana hakuna mgombea mwingine.

JLM hapa watagombea fakalava Shunie na Ambiele Kiviele

NB huu mfano ni kwa mtazamo wangu mwenyewe.....lakini ndivyo tulitakiwa kuwapata wana JF bora.

Huwezi kusema mtu mmoja atwae tuzo wakati JF ina majukwaa mengi na kila jukwaa lina manguli wanaolitendea haki.
I cecond you...

Huu mtiririko wako ndo mzuri...
 
Uzi kama huu ulitakiwa uanzishwe na Jamii forums wenyewe,hakuna ajuaye lengo hasa la mleta mada kuanzisha uzi huu ni lipi?

Watu wengi humu wanatumia ID fake na hawapo tayari kujulikana, so sidhani kama kuna yeyote atakaeshinda "shindano" hili itakua ni rahisi kwake kumtumia contact zake mtu asiyemjua (mleta mada) ili amtumie hiyo laki moja,

nadhani itakua busara zaidi kama uongozi wa jamii forums watauchukue huu uzi na kuuboresha au waufute kabisa,

huu ni mtazamo wangu tu.

Lol! Hahahaha siyo swala la kupanick Mkuu ni swala la kusikitishwa na nchi yetu iliyojaliwa utajiri mkubwa sana kuendeshwa hovyo hovyo kiasi ambacho utajiri wa nchi unawanufaisha kundi dogo sana la Watanzania huku nchi ikibaki nyuma kwenye kila sekta. Ujio wa Lowassa haujanivuruga na kamwe hautanivuruga kwa sababu kama alivyosema Baba wa Taifa CHADEMA si mama yangu. Na sitashangaa kama Lowassa siku moja akiamua kurudi CCM, BAK atakuwa wa kwanza kushangilia.

Siku hizi BAK anapaniki sana, hana uvimilivu wala mada motomoto kama zamani. Ujio wa Lowasa ndani ya Chadema umemvuruga sana japo huwezi kumuona akikiri hadharani.
 
Back
Top Bottom