Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
- Thread starter
- #41
Yah hiyo ndio demokrasia ya kweli sasa.Kuna jamaa alikua anawaka kumsema m/kiti vibaya kuhusu bandari, nikamuuliza kwani hiyo bandari nafananaje, akasema inafanana kama na madini ya dhahabu, watu wote tulicheka kwaujinga wake. Hata bandari haijui ila anatoa povukuongea.
Fikiria mtu asieijua hata bandari yenyewe inafananaje, ana uhuru wa kumsema mwenyekiti wa chama bila kuchukuliwa hatua yoyote, hapo bado sijamtaja Tibaijuka na kundi lake lote lililomsakama mwenyekiti wao kuhusu bandari lkn hadi leo wapo chamani na mwenyekiti anawajua na kuwaona.
Sasa kuna mwenyekiti aliewashughulikia kina Zito Kabwe kwa sababu ya kuhoji tu uhalali wa mwenyekiti kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka 10 kinyume na katiba ya chama.
Badala ya kumjibu tu Zito kistaarab kwamba mwenyekiti alinyofoa hicho kifungu cha katiba ili atawale yeye peke yake, wao walichofanya ni kumfukuza kabisa chamani na kupelekea wengine kuogopa utaratibu wa kuhoji hoji kama Zito.
RIP Chacha Wangwe.