Ni nani anayetaka kuweka maisha yake hatarini kwa sababu ya kuhoji tu?

Ni nani anayetaka kuweka maisha yake hatarini kwa sababu ya kuhoji tu?

Wewe unashida Sana, unahitajika maombi. Utakodi kitu huna kibali nacho. Yani utakodi fremu ya biashara na kulipia pango bila kupata kibali Cha biashara manispaa?.

Unapata kibali kwanza ndio una Kodi chopa. Usipende kuongea vice versa na kulazimisha kuwa kweli. Kabla ya kukodi chopa , unaomba kwanza kibali na kibali kinajieleza ndio unakodi chopa.

Yani unakodi chopa kipindi hiki Cha mvua au Magufuli au Hali ya hewa mbaya bila kibali?.
Haya ndio maswali ambayo ukiuliza nakubaliana na wewe kwamba umeyafikiria kabla ya kuuliza.
 
Mbona haya maneno kayasema Makonda. Tena kawaita Viongozi wa CCM chura.
Huko kwa kina Makonda watu wana uhuru na demokrasia ndio maana Makonda anautumia huo uhuru kuwaita watu hivyo ulivyosema.

Lkn upande wa pili hata wewe unampigania mwenyekiti hapa ukienda kinyume na ule utaratibu wa kumsifu na kumpigania mitandaoni, nakwambia utaitwa msaliti, sijui unatumiwa na CCM, umetumwa nk.

Alafu anakuja mtu anahadaa watu et Chadema kuna demokrasia.
Upuuzi mtupu.
 
Cha kufurahisha huwa mnajifanya mna akili Sana, wakati hata vyoo vya wanafunzi mashuleni mnajengewa na wadhamini. Yani serikali itakuwa ya kijinga kutumia nguvu nyingi kuimaliza CHADEMA kuliko kumaliza Deni la taifa.
Lengo sio kuimaliza Chadema wala upinzani wowote mkuu. Kwa sababu Chadema au upinzani ukifa serikali itakosa pesa kutoka Ulaya ambazo hugawiwa zile nchi zote zenye kuendeleza demokrasia duniani.

Kinachofanyika ni mamlaka kuhakikisha mtu wao Mbowe anabaki hapo, na kamwe yule anaeonekana kuwa mpinzani wa kweli wa serikali (Lisu) hapewi nafasi ya kuongoza chama.
Hata Cuf ilikuwa hivyo hivyo, Lipumba alitoka na kurudi chamani huku maalim Seif alieonekana tishio kwa mamlaka akajikuta anabaki karibu mkuu asiekuwa na maamuzi yoyote kichama na kikatiba hadi akaamua kukimbia mwenyewe na kuhamia chama kingine.
 
Baba yangu, umri wangu nina wajukuu unataka nizungumzie baba?
we vipi we mtoto?
Mumeo hajawahi kumzungumzia Elon Musk, Bill Gates, Ronaldo, Messi, Gaddafi na Kiduku wa Korea?Hao si waume za watu? AFYA YA AKILI!

Wewe hujawahi kumzungumzia Ridhiwani Kikwete, Mo DEwji na Ghalib GSM? si waume za watu?

#Mpuuzi mmoja
Mimi ni ME ndo maana namsifia Samia.
Aibu kwa ME kumsifia ME mwenzako 😂😂
 
Punguza uongo. Kuna wauaji zaidi ya CCM?. Si juzi mlikuwa mnalia kuwa Magufuli kauawa? Au sio nyie?. Mpaka Mzee Makamba akapiga jiwe kuwa Wazuri hawafi. Hakuna kiongozi wa upinzani anaweza kufanya scheme yeyote akaachwa salama.

Mbowe kuajiri wanajeshi wastaafu, tayari kapewa kesi ya ugaidi.
Mbowe hakupewa kesi, bali kapachikiwa tu kazi inayoambatana na masharti ya kifungo na wenye mamlaka ili kuwafubaza vijana waweze kuelewa kuwa na yeye ni mpinzani.

Ndio maana siku aliyoachiwa akaenda kuonana na amiri jeshi wa kazi ili apewe pole kwa kifungo kile cha kazi aichotumikia.

Kwa vile alienda mwenyewe makusudi bila kuongozana na kiongozi yoyote wa chama, hivyo hakuna anaefahamu mazungumzo yalikuaje baada ya kumaliza kupewa pole.

Ila kwa sisi tunaofahamu kazi za hao jamaa duniani, hatuoni lolote linaloweza kutudanganya kuhusu jamaa.
Huko kwa wenzetu utakuta FBI au CIA anajiingiza hadi kwa magaidi au kwenye magenge ya wahalifu hatari, huku akijifanya na yeye ni mdhamini mkuu wa magenge hayo, kumbe nyuma ya pazia ndo mtoa taarifa mkubwa wa operation zote za magenge hayo kwa FBI au CIA.

So ije kuwa kifungo cha mtu anawekwa tu sehemu, afu mwisho wa siku anafunguliwa kwenda kuonana na mkuu.
 
Sio huogopi, unajua CHADEMA sio CCM inayouwa watu bila kuchukuliwa hatua.
CCM inayoua watu vipi mkuu na wakati kina Tibaijuka wamemchalenge mwenyekiti ambae jeshi na vyombo vyote vya ulinzi na usalama vipo mikononi kwake?
Na bado wanadunda tu mitaani mpaka leo!
 
Yule jamaa sijui walimuweka pale kwa lipi, hana presence kabisa. Ile nafasi angepewa Lema ingesaidia kidogo
Mkuu ukisoma post ya #27 ndo utaelewa kwamba hao unataka wawepo hapo katika uongozi wa juu kamwe hawawezi kuwekwa.
Hapo wanatakiwa watu ambao watakuwa tayari kufanya kazi na mwenyekiti moja kwa moja bila kusita wala kuhoji chochote.
 
JIWE hukusifia?
Wanaume akina Makonda na Mawaziri wote waliokuwa wanamsifia JIWE walikuwa wanawake?
Kumsifia mtu kunachagua gender?
Kama wewe una uume na unasema unasifia uuke, unamaana gani?
Hahaha 🤣🤣 basi mkuu acha tuongee kwa hoja, maana sisi wote ni watanzania na lengo letu ni kuiona Tanzania iliyokuwa bora kwa ajili yetu na vizazi vyetu, japo ukweli ni kwamba wanasiasa wote wa pande zote za tawala na upinzani wanatuona sisi ndio mitaji yao ya kufikia mafanikio yao na familia zao. Iwe kisiasa au kimaisha.

Mimi huwa nawakubali wewe na econonist jinsi tunavyochangiaga uzi kistaarab bila mmoja wetu kumuudhi au kumtukana mungine kwa sababu ya siasa au mwanasiasa.
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Nauliza hili swali hapa, ila nina uhakika hakuna atakaekuwa tayari kujitokeza kunijibu. Hii ni kwa sababu wengi wanatumiwa ili mkono uende kinywani, lkn umafia wa yule anaewatumia wanaujua vizuri sana.

Hapa nazungumzia ule upande wa kondoo kutembea kichwa chini (usihoji chochote kuhusu mwenyekiti) ambapo mtu akijifanya mbuzi kunyanyua kichwa juu (kuhoji kuhusu mwenyekiti) anakumbana na hatari mbele yake.

Makamu mwenyekiti anaeishi Ulaya na familia yake, juzi amejaribu kuwatoa watu uoga wa kuhoji au kukosoa, lkn mpaka sasa watu bado wanaogopa kuanza kukosoa, au kujitokeza kuhoji haswa wakikumbuka yale yaliomtokea Chacha Wangwe, Zito Kabwe na wengine wengi wa aina hiyo.

Sio kwamba wanachama wao hawajui kuwa mwenyekiti wao chama kishamshinda, na juhudi zake za kukijenga chama bila kuwa na makamu wake karibu zimeshindikana. Au sio kwamba wanachama wao hawakumbuki ile kauli ya mwenyekiti wao kuwa ataachia kiti cha uenyekiti mwaka huu wa 2023, baada ya kupigiwa kelele huko nyuma na wenye uchungu na chama ajiuzulu, lahasha.

Wanajua na wanakumbuka sana, lkn nani atakaekuwa tayari kumchalenge Mafia wa chama ili mchalenjiji huyo aweke maisha yake na ya familia yake hatarini?

Wengi wanajiuliza, ikiwa makamu ambae yuko Ulaya anaogopa kumface mwenyekiti, na badala yake anatumia mafumbo ya hapa na pale, je wao ambao wapo karibu na mwenyekiti huyo watatoa wapi ujasiri wa kuhoji na kuuliza siku rasmi ya mwenyekiti kuachia ofisi?
Hilo ndo swali
 
Lita 1 ya Diesel ni 3510, na vyakula bei juu, alaf mwenyekiti anataka kila mkutano azunguke kwa chopa.

Kwanini hiyo hela ya kuzunguka na chopa asiitumie kuwasaidia nyie chawa wake masikini kwa kuwanunulia japo kilo mbili mbili za unga na moja moja ya sukari ili iwe chachu ya watu kukichagua chama chake katika uchaguzi mkuu?
Akili zako zipo nyuma na umezikalia.
Nani chawa wa Mbowe?

Mnapeleka bungeni sheria za wake wa viongozi wastaafu walipwe huku watoto wengi wakikaa chini ardhini bila madawati,bima ya afya kwa watoto chini ya miaka 5 imefuta,kikokotoo kinaliza wastaafu wengi halafu kenge kama wewe unatanua domo kuleta ushabiki maandazi.
 
Akili zako zipo nyuma na umezikalia.
Nani chawa wa Mbowe?

Mnapeleka bungeni sheria za wake wa viongozi wastaafu walipwe huku watoto wengi wakikaa chini ardhini bila madawati,bima ya afya kwa watoto chini ya miaka 5 imefuta,kikokotoo kinaliza wastaafu wengi halafu kenge kama wewe unatanua domo kuleta ushabiki maandazi.
Dada acha kupanic. Uliekuja kumtetea mitandaoni kaishaowa kitambo, hivyo wewe hata uje kumtetea vipi hawezi kukufanya mke wa pili. Sana sana atakupakua kisamvu alaf akutelekeze. Hivyo punguza hasira na panic dada yangu. Hebu fikiria watoto wake wapite humu alaf waone mtu wasiemfahamu, wala kufahamiwa na baba yao unavyotoa mishipa na povu kumpigania baba yao ambae ni mume wa mama yao kindoa, unafikiri watakuonaje?

Kwanini usitumie hili povu kumtetea baba yao huko kwenu nanjili au angalau umtetea hata bwana anaekulipia kodi ya nyumba mjini?
 
Dada acha kupanic. Uliekuja kumtetea mitandaoni kaishaowa kitambo, hivyo wewe hata uje kumtetea vipi hawezi kukufanya mke wa pili. Sana sana atakupakua kisamvu alaf akutelekeze. Hivyo punguza hasira na panic dada yangu. Hebu fikiria watoto wake wapite humu alaf waone mtu wasiemfahamu, wala kufahamiwa na baba yao unavyotoa mishipa na povu kumpigania baba yao ambae ni mume wa mama yao kindoa, unafikiri watakuonaje?

Kwanini usitumie hili povu kumtetea baba yao huko kwenu nanjili au angalau umtetea hata bwana anaekulipia kodi ya nyumba mjini?
Tuzi lako linakuwasha wewe,utakamuliwa tu muda sio mrefu.
Ww na mm ndani katoka povu? Mtu unaandika ukurasa mzima.?
 
Back
Top Bottom