Hahaha... Aisee inashangaza sana kuona mtu unaejifanya mjanja mitandaoni mpaka leo unashindwa kutumia ujanja wako kumsoma Mbowe na kumjua kuwa ni mtu gani, na wa aina gani ndani ya chama 🤣🤣🤣
Kifupi jamaa kawekwa hapo (sio kujiweka mwenyewe au chama kama mnavyoaminishwa) kwa Kazi maalum.
Na hiyo kazi ashaifanya (moja wapo) ni ile ya 2015, na zingine za sirini ambazo sio rahisi mtu ambae hatumii akili iliyohuru kuzijua.
Kesi za kubumba bumba (ili kuwafubazeni) aliyopewa Mbowe, na baada ya kuachiwa tu kukimbilia ikulu fasta siku hiyo hiyo kupewa pole na yule aliemfunga, inamfanya mtu alie huru kimawazo kufikiria mara mbili mbili kama kweli jamaa ni mpinzani thabiti kama Yule aliekumbilia Ulaya au ni jamii ya hawa hawa kina Mrema, Cheo, Lipumba, Zito nk.
Hata swala la kuharibiwa mashamba limezubaza wengi akili, huku mwamba akiwa kalipwa double kupitia njia za siri. Kinachomkuta Mbowe au kile anachokifanya katika chama hadi nyie kupiga makelele kwamba atoke sio cha bahati mbaya, bali ni moja kati ya majukumu yake aliyopewa na wenye mamlaka ili kuhakikisha vyama vyote vipya na vya zamani vitaendelea kuwa vya upinzani tu na kupewa wabunge wawili watatu kama walivyokubaliana katika mapatano yao na CCM.
Mrema alianza vizuri, baada ya muda akajigeuza sultan wa chama ili asijitokeze mwanamageuzi wa kweli wa kuichalenge serikali. Mwisho chama kikaanza kupoteza ushawishi taratibu, na baadae kubaki jina.
Mara akaja Lipumba akaiteka bara na visiwani watu wakamuona ni mwana mageuzi wa kweli hadi kupelekea watu kufa na kufungwa katika maandamano na vurugu mbali mbali. Pia kama mwenzake, na yeye akaanzisha mfumo wa kubaki yeye tu uongozini, ili kuhakikisha hatokei mtu mwenye mawazo, na plan ya kweli ya kukitoa chama tawala madarakani. Chama kikaanza kupoteza mvuto na wanachama, wazee wakahamia Chadema, wakamuweka Mbowe, jamaa akaanza kama wenzake pengine yeye akawa zaidi ya hata Lipumba kwa ushawishi. Mambo yakaenda vizuri, ila kama ilivyo ada na yeye akabadili sheria makusudi ili watu kama kina Lisu wanaoonekana ni wapinzani halisi wasije kukalia kiti na kuichalenge serikali. Jamaa kang'ang'ania hadi leo bila kujali boko aliyotoa mwaka 2015 japo wengi tunafahamu kuwa ni moja kati ya majukumu aliyopewa na waliomuweka pale, lkn angeona aibu na kujiuzulu kutokana na kelele za watu kwake.
Anyway watanzania wengi hawana upeo, hivyo acha jamaa atumikie ofisi mbili kwa wakati mmoja. Kama tukiwa hai, hayo ya kutumikia ofisi mbili tutakuja kuyajua katika wasifu wake siku Mungu atapoamua kumchukua kama ilivyokuwa kwa kina Mrema, Membe nk.