Ni nani atafanikiwa kumfunga paka kengele ili tusiangamie wote?

Ni nani atafanikiwa kumfunga paka kengele ili tusiangamie wote?

buzitata

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2017
Posts
2,370
Reaction score
7,900
Habarini

kwa kipindi kirefu nimejaribu kufuatilia hali ya ndani ya nchi yetu hasa suala zima la afya pamoja na kukithiri kwa rushwa ila nimejikuta nikipata hofu kubwa juu ya nini kitafuata kwa kila mwanajamii tusipolitatua tatizo hili kabla hali haijawa mbaya zaidi

Kwa kipindi cha hivi karibuni kumeibuka kundi kubwa la watu ambao wameanza kukumbwa na tatizo geni kidogo kwa jamii zetu, ambalo ni ugonjwa wa ini pamoja na figo.

Ugonjwa huweza kumpata mtu yeyote lakini ni vema kuangalia zaidi chanzo cha tatizo ili tuweze kujikwamua kama jamii.

Watu wengi ambao wanakumbwa na matatizo hayo kwa historia zao zinaonesha wameathiriwa na mfumo mbovu wa chakula pamoja na unywaji wa pombe hasa pombe kali.

Jambo hili lipo kama utani na jamii huwa inawashangaa walevi kwanini wanaendelea kunywa ilhali wanajua unywaji wa pombe ni hatari kwa afya, kwangu mimi siwalaumu hata kidogo kwasababu ninajua nini maana ya uraibu na ni ngumu kiasi gani kuushinda uraibu

Unywaji wa pombe kupita kiasi ni uraibu ambao mtu unakuwa umemuelemea.

Chanzo kikuu cha watu kukimbilia pombe kali hasa hizi za bei rahisi ni baada ya kushindwa kumudu gharama ya kunywa pombe ambazo zina madhara madogo hivyo hunywa pombe zenye gharama ndogo ambazo zina madhara makubwa

Nini kifanyike
Serikali ikiwapendeza ni bora wapunguze kodi kwenye pombe ambazo zinamadhara madogo ili watu wenye uraibu wapumue. Mtu kama ataweza kunywa bia mpaka akakata kiu yake kwa gharama nafuu hawezi kukimbilia kwenye unywaji wa pombe zenye madhara makubwa kiafya.

Kuna hili jambo lingine naona kama jamii inalichekea ila ipo siku kunakitu kitakuja kulipuka na tusijue namna ya kujinasua

Kuna aina fulani ya kibiashara imeibuka kwa sasa ambayo ni nzuri lakini ni bomu la siku za usoni

Ulaji wa kuku wa broiler, hawa ni kuku ambao wanasifika kuwa wanafugwa kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu hivyo hutengeneza faida nzuri kwa wakulima

Swali la kujiuliza, je kuna taasisi yoyote ambayo inafuatilia ubora wa kiafya ambao upo kwa hao kuku?

Kwa wale ambao wamewahi kuishi nje ya tanzania hapa watakubaliana nami, kuna utofauti mkubwa sana wa broiler wa nje ukimlinganisha na wa tanzania

INgekuwa vema kama jamii ama taasisi kuhoji je kuku anayeenda kwa mlaji awe na umri gani kuliko hali ilivyo sasa ambayo watu wanauza mpaka kuku mwenye umri wa wiki tatu, this is not fair kwa afya zetu.
Ni ngumu kunielewa ila tujue tu hakuna chakula cha kawaida ambacho kinaweza kumfanya kuku wa wiki tatu aweze kuliwa bali wanapewa madawa ya ukuzaji
Swali la kujiuliza je hayo madawa wanayolishwa hao kuku ni salama kwa afya zetu?

Mboga za majani nazo hasa kwa dar sio salama sana kwasababu zinakuzwa kwa maji ambayo sio salama, hapa tunaweza kupata kundi lingine la watu watakaopata magonjwa ya ini na figo japokuwa hawana uraibu ama historia ya kunywa pombe kupita kiasi.


huduma zetu za afya zinajitahidi ila hazina uwezo wa kuturejeshea afya zetu endapo tutapatwa na majanga ambayo leo tunayafumbia macho kwakuwa tunahisi sisi hayatatupata

mwenye shibe hamjui mwenye njaa tuamke jamani hili sio jambo la kuchekewa ni heri kutatua tatizo mapema
 
B497670F-AF24-44D5-9AB8-32F0DAA90252.jpeg
 
Kuhusu kuku Wa kisasa, Nakusahihisha, Kuku harishwi madawa ili akue, hoja yako ya kusema kuku hawezi kuuzwa kwa wiki 3 bila kurishwa madawa ya ukuzaji sio kweli ni matango pori.

Kuku wanarishwa balanced diet, ilio tengenezwa kwa pumba, mahindi, soya, mashudu, Dagaa, Mifupa nk.

Changamoto ya Kuku wa kisasa ni Antibiotics(Hizi ni dawa za kutibu magonjwa, sio kunenepesha) hata hivyo madhara makubwa ya haya madawa ni kuleta Usugu kwa vimelea wanao sababisha ugonjwa kwa binaadamu, hivyo tutakosa antibiotics za kujitibu huko mwishoni.
 
Hatari kubwa ya Figo iko kwenye, Vinywaji varidi vya viwandani, Kama Juisi, Energy drink na Soda.

Pia unywaji wa Beer fake, Za uchochoroni unachochea tatizo.

Kubwa zaidi ni, Madawa ya kutunzia nafaka(Mahindi), Madawa ya kuua wadudu waharibifu (Hapa ni nyanya, Mboga mboga zoote)

Hivyo mleta maada list ni ndefu kuchomoka ni Ngumu, ukizingatia TBS na TMDA wamelala
 
Back
Top Bottom