Ni nani atafanikiwa kumfunga paka kengele ili tusiangamie wote?

Ni nani atafanikiwa kumfunga paka kengele ili tusiangamie wote?

Wewe ukipita zile aptitude niite nyau na nahamia kwako bila taarifa😎
Niliwah kufanya moja, na mpaka leo cjui nilifaulu vp mana Nilikuwa najibu kwa kufumba macho na kugusa jibu na ndo hilo hilo najaza 😂
 
Habarini

kwa kipindi kirefu nimejaribu kufuatilia hali ya ndani ya nchi yetu hasa suala zima la afya pamoja na kukithiri kwa rushwa ila nimejikuta nikipata hofu kubwa juu ya nini kitafuata kwa kila mwanajamii tusipolitatua tatizo hili kabla hali haijawa mbaya zaidi

Kwa kipindi cha hivi karibuni kumeibuka kundi kubwa la watu ambao wameanza kukumbwa na tatizo geni kidogo kwa jamii zetu, ambalo ni ugonjwa wa ini pamoja na figo.

Ugonjwa huweza kumpata mtu yeyote lakini ni vema kuangalia zaidi chanzo cha tatizo ili tuweze kujikwamua kama jamii.

Watu wengi ambao wanakumbwa na matatizo hayo kwa historia zao zinaonesha wameathiriwa na mfumo mbovu wa chakula pamoja na unywaji wa pombe hasa pombe kali.

Jambo hili lipo kama utani na jamii huwa inawashangaa walevi kwanini wanaendelea kunywa ilhali wanajua unywaji wa pombe ni hatari kwa afya, kwangu mimi siwalaumu hata kidogo kwasababu ninajua nini maana ya uraibu na ni ngumu kiasi gani kuushinda uraibu

Unywaji wa pombe kupita kiasi ni uraibu ambao mtu unakuwa umemuelemea.

Chanzo kikuu cha watu kukimbilia pombe kali hasa hizi za bei rahisi ni baada ya kushindwa kumudu gharama ya kunywa pombe ambazo zina madhara madogo hivyo hunywa pombe zenye gharama ndogo ambazo zina madhara makubwa

Nini kifanyike
Serikali ikiwapendeza ni bora wapunguze kodi kwenye pombe ambazo zinamadhara madogo ili watu wenye uraibu wapumue. Mtu kama ataweza kunywa bia mpaka akakata kiu yake kwa gharama nafuu hawezi kukimbilia kwenye unywaji wa pombe zenye madhara makubwa kiafya.

Kuna hili jambo lingine naona kama jamii inalichekea ila ipo siku kunakitu kitakuja kulipuka na tusijue namna ya kujinasua

Kuna aina fulani ya kibiashara imeibuka kwa sasa ambayo ni nzuri lakini ni bomu la siku za usoni

Ulaji wa kuku wa broiler, hawa ni kuku ambao wanasifika kuwa wanafugwa kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu hivyo hutengeneza faida nzuri kwa wakulima

Swali la kujiuliza, je kuna taasisi yoyote ambayo inafuatilia ubora wa kiafya ambao upo kwa hao kuku?

Kwa wale ambao wamewahi kuishi nje ya tanzania hapa watakubaliana nami, kuna utofauti mkubwa sana wa broiler wa nje ukimlinganisha na wa tanzania

INgekuwa vema kama jamii ama taasisi kuhoji je kuku anayeenda kwa mlaji awe na umri gani kuliko hali ilivyo sasa ambayo watu wanauza mpaka kuku mwenye umri wa wiki tatu, this is not fair kwa afya zetu.
Ni ngumu kunielewa ila tujue tu hakuna chakula cha kawaida ambacho kinaweza kumfanya kuku wa wiki tatu aweze kuliwa bali wanapewa madawa ya ukuzaji
Swali la kujiuliza je hayo madawa wanayolishwa hao kuku ni salama kwa afya zetu?

Mboga za majani nazo hasa kwa dar sio salama sana kwasababu zinakuzwa kwa maji ambayo sio salama, hapa tunaweza kupata kundi lingine la watu watakaopata magonjwa ya ini na figo japokuwa hawana uraibu ama historia ya kunywa pombe kupita kiasi.


huduma zetu za afya zinajitahidi ila hazina uwezo wa kuturejeshea afya zetu endapo tutapatwa na majanga ambayo leo tunayafumbia macho kwakuwa tunahisi sisi hayatatupata

mwenye shibe hamjui mwenye njaa tuamke jamani hili sio jambo la kuchekewa ni heri kutatua tatizo mapema
Kwenye pombe ndo pa kupigia hela kwa serikali zilizo nyingi, maana hata ikiongezeka kodi, bei zikipanda, watu watanunua tu kwasababu ya uraibu wao so serikali itapata pesa tu. Wakipunguza bei za bia, mataputapu yatakosa wateja na wauzaji wao wanategemea hizo hela ili wasomeshee watoto. NB sinywi pombe na sina mpango wa kuinywa.
 
Niliwah kufanya moja, na mpaka leo cjui nilifaulu vp mana Nilikuwa najibu kwa kufumba macho na kugusa jibu na ndo hilo hilo najaza 😂
hahaha aptitude ya jana ndio nilichofanya kwenye kutafuta umri za watu sijazaa😅
 
Kuna siku nilivunja yai la kuku wa kigeni nikakuta kiini kina rangi ya orange, nilijiuliza ni kwasababu ya vyakula wanavyokula?
Yameenea haya mayai ya kisasa
Ya kiini cha orange
 
Ahsante kwa kunisahihisha, hata nguruwe kulishwa ARV ni matango pori tunamezeshwa sio

Matango pori kabisa, Nimefanya kazi na Mostly successive pig farmers in Tz, Hakuna anae lisha hayo madudu.

Labda huko uchochoroni huko, ambapo nahakika bado hawawezi kupata matokeo mazuri maana hayo madawa hayawezi kua mbadala wa chakula kizuri
 
Japo mie si mtaalamu nachangia kipande kidogo tu.
Kama ni madawa hakuna asiyaepuka na anayeweza kuyaepuka. Nalima mazao pia na mboga mboga
Huku bila mbolea ya kupandia, kukuzia, mbolea ya kukupa mazao yaliyonona plus booster. Hapo pia Kuna dawa za kupuliza zipo zenye gundi ukipuliza hata ikinyesha mvua hazitoki kwenye mmea , Jani au zao lenyewe. Bila kufanya hivyo hujafanya kilimo.
Kwa muktadha huo hakuna pa kuponea.
Ndo maana mi najilipuaga tu nafanya na natumia chochote nikijisikia.....

Ni Hatari sana, Japo mbolea hazina shida yeyote, ila hayo madawa ndo shetani mwenyewe.
 
Matango pori kabisa, Nimefanya kazi na Mostly successive pig farmers in Tz, Hakuna anae lisha hayo madudu.

Labda huko uchochoroni huko, ambapo nahakika bado hawawezi kupata matokeo mazuri maana hayo madawa hayawezi kua mbadala wa chakula kizuri
Ongea na watu vizuri utajua mengi.. wenzako wanalisha sana ARV nguruwe zao ila hawawezi kukuambia wewe kwasababu kwa ninavyoona uandishi wako unaonekana ni mtu ambaye hujui kutunza siri
 

Shida Ya Figo Na Maini Haisababishwi Na Pombe Tu,,Ni Mifumo Mzima Wa Maisha Ya Sasa,,G.M.O(Genital Modified Organisms)Kwenye Mbogamboga Tunazo Kula Zinapigwa Sana Sumu,,Wanyama Nao Antibiotics Kibao Na Mbaya Zaidi Wengi Wanatumia Viatilifu Hivyo Bila Utaalamu Na Kutozingatia Muda Wa Kuuza Baada Ya Matumizi Hayo Ya Madawa,,,Tutanatafuna Sana Sumu Na Usipozingatia Hata Usafi Wa Kusafisha Hayo Manunuzi YETU Ndio Hatari Zaidi,,,Madhara Yanakuwa KidogoKidogo Kwa Muda Mrefu,,,Na Utaratibu Pia Wakucheki Afya Mara Kwa Mara Maisha Yetu,,Ni Mgumu,,Tatizo Linakuja Kugundulika Umeshanywea Haswaa Na Uchumi Huna,,,Matibabu Gharama,,Stressi Nazo Zimejaa Pomoni Kwa Kichwa,Kutokana Na Michakato Migumu Ya Kila Siku,,Lazima Ukufe Tu....Afya Zetu Ni Biashara Zao....
Watu Wanajali Kwantinti Kuliko Kwaliti Yatakayokutokea Ni Juu Yako....Na Kukwepa Ni Ngumu Mnoo Zaidi Ni Kuwa Na Kiasi Na Umakini Wa Hali Juu Tu...
###WeweKuweza###
​
 
Ongea na watu vizuri utajua mengi.. wenzako wanalisha sana ARV nguruwe zao ila hawawezi kukuambia wewe kwasababu kwa ninavyoona uandishi wako unaonekana ni mtu ambaye hujui kutunza siri

Wanaweza kua wanarisha hizo ARV, ila hawawezi pata matokeo ya kushtua na wanao fanya hivo ni wale wafugaji koko, Lishe inawashinda ndo wanatafuta mbadala.
 
Back
Top Bottom