Ni nani atafanikiwa kumfunga paka kengele ili tusiangamie wote?

Ni nani atafanikiwa kumfunga paka kengele ili tusiangamie wote?

Hatari kubwa ya Figo iko kwenye, Vinywaji varidi vya viwandani, Kama Juisi, Energy drink na Soda.

Pia unywaji wa Beer fake, Za uchochoroni unachochea tatizo.

Kubwa zaidi ni, Madawa ya kutunzia nafaka(Mahindi), Madawa ya kuua wadudu waharibifu (Hapa ni nyanya, Mboga mboga zoote)

Hivyo mleta maada list ni ndefu kuchomoka ni Ngumu, ukizingatia TBS na TMDA wamelala
Kwenye hiyo list ndefu ndipo nilipomaanisha mimi

Mamlaka zimelala fofo zinasubiri tukio litokee halafu wapate kiki ya kuja mjini
 
Kuhusu kuku Wa kisasa, Nakusahihisha, Kuku harishwi madawa ili akue, hoja yako ya kusema kuku hawezi kuuzwa kwa wiki 3 bila kurishwa madawa ya ukuzaji sio kweli ni matango pori.

Kuku wanarishwa balanced diet, ilio tengenezwa kwa pumba, mahindi, soya, mashudu, Dagaa, Mifupa nk.

Changamoto ya Kuku wa kisasa ni Antibiotics(Hizi ni dawa za kutibu magonjwa, sio kunenepesha) hata hivyo madhara makubwa ya haya madawa ni kuleta Usugu kwa vimelea wanao sababisha ugonjwa kwa binaadamu, hivyo tutakosa antibiotics za kujitibu huko mwishoni.
Ahsante kwa kunisahihisha, hata nguruwe kulishwa ARV ni matango pori tunamezeshwa sio
 
Japo mie si mtaalamu nachangia kipande kidogo tu.
Kama ni madawa hakuna asiyaepuka na anayeweza kuyaepuka. Nalima mazao pia na mboga mboga
Huku bila mbolea ya kupandia, kukuzia, mbolea ya kukupa mazao yaliyonona plus booster. Hapo pia Kuna dawa za kupuliza zipo zenye gundi ukipuliza hata ikinyesha mvua hazitoki kwenye mmea , Jani au zao lenyewe. Bila kufanya hivyo hujafanya kilimo.
Kwa muktadha huo hakuna pa kuponea.
Ndo maana mi najilipuaga tu nafanya na natumia chochote nikijisikia.....
 
kukosa elimu ni janga sana
Yani watu walishajiaminisha Figo kufeli au kuwa na mawe inasababishwa na pombe kali kitu ambacho sio.
Bila shaka kama umesoma vizuri uzi wangu nimesema kuna kundi la wanywa pombe kali pamoja na ambao wanapata magonjwa kutokana na aina ya vyakula tunavyokula

Halafu unaposema kukosa elimu unakosea sana yawezekana wewe ndio hujui, hapo kwa upande wa watu wenye uraibu nimemaanisha alchol hepatitus sio hepetitus B
 
Mboga za majani nazo hasa kwa dar sio salama sana kwasababu zinakuzwa kwa maji ambayo sio salama, hapa tunaweza kupata kundi lingine la watu watakaopata magonjwa ya ini na figo japokuwa hawana uraibu ama historia ya kunywa pombe kupita kiasi.
Duuuh sasa sisi Vegetarian itakuaje?
 
Hv inawezekana vp mtu hana pesa ya kula ila ana pesa za pombe?

Au mtu anajua kabisa hii ni pombe kali afu anakunywa bila kula?
Ndio maana halisi ya uraibu, ukishakuwa mraibu wa kitu huwezi kujizuia kama unavyodhani.

Watumia pombe kali wote wanajua fika kua hii kitu ni hatari na baadhi ya effect anaziona kabisa kuwa nakoelekea watakuja kunizika ila ndio hivyo tena hawezi.
 
Changamoto inaanzia kwenye UONGOZI.

AINA YA UONGOZI NA JINSI INAVYOJIENDESHA INAPELEKEA RUSHWA KUBWA NA ILIYOKITHIRI MAMLAKANI HUKO VITU VINGI VINAGUSHIWA, AGRI INPUT(MBEGU MBOLEA TUMEPIGWA SANA), VINYWAJI, UPOTEVU WA MAPATO (TRA, BANDARI, AIRPORT, BORDER ETC).

Anajinufaisha mtu mmoja au ishirini arafu kanda nzima kama sio Nchi yote inaangamia.

Tutaendelea kuangamia sisi na familia zetu kama hakutakua na mabadiliko.

JUST IMAGINE MTU ANAYECHEZA NA USTAWI WA JAMII YA NCHI HII, ADHABU YAKE NI AZOMEWE ILI AONE AIBU KESHO ASIRUDIE... SERIOUS!?
 
hepatitus ndio kitu gani
sema hepatitis B
Kwaiyo wewe unahisi ipo hepatits B peke yake? Sijaweka A,B,C kwasababu maalum(halafu usipende kunichezesha ngoma unayoitaka wewe hapa mada ni ini lililoathirika kwa pombe na vyakula huko kwenye gonjwa linalosababishwa na zinaa mimi sipo)
 
Back
Top Bottom