Ni neno gani baba yako alitamka ambalo unaliishi mpaka Leo!

Bolotoba

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
4,545
Reaction score
10,426
Ikiwa Leo ni siku ya baba duniani?
Nakumbuka mzee wangu aliwahi kusema "hakuna mkamilifu asilimia kwa Mia kwa mia na hakuna mbovu asilimia mia kwa Mia kila mtu ukimtumia vizuri kuna fursa atakupa"

Lakini aliniambia usioe kwa kuangalia umbo bali
"Angalia ni mchezaji gani unayemtaka unaamini ukimsajili katika timu yako Ataleta matokeo unayotaka"

Vipi kwa upande wenu wanajamvi
Ni maneno gani ambayo baba yako alitamka mpaka Leo unalikumbuka na kuliishi?

Karibuni kwa michango 🤝
 
Mshua aliniambia hivi

“Usipoyabadilisha mazingira,yatakubadilisha”

Akimaanisha Ikiwa hutafanya juhudi ya kubadilisha hali ya maisha yako kama vile kazi au biashara isiyoridhisha, mazingira ya kimaisha magumu, au mahusiano yenye matatizo basi mazingira hayo yatakugharimu na kukufanya kuwa mtumwa wa mazingira hayo
 
Ikiwa Leo ni siku ya baba duniani?
Nakumbuka mzee wangu aliwahi kusema "hakuna mkamilifu asilimia kwa Mia kwa mia na hakuna mbovu asilimia mia kwa Mia kila mtu ukimtumia vizuri kuna fursa atakupa"

Lakini aliniambia usioe kwa kuangalia umbo bali
"Angalia ni mchezaji gani unayemtaka unaamini ukimsajili katika timu yako Ataleta matokeo unayotaka"

Vipi kwa upande wenu wanajamvi
Ni maneno gani ambayo baba yako alitamka mpaka Leo unalikumbuka na kuliishi?

Karibuni kwa michango 🤝
Hayo alikuambia mzee wako,leta aliyokuambia baba yako sasa.
 
Vitu vinne epuka sana ukitaka kuishi maisha marefu yasiyokuwa na maumivu mengi.....
Migogoro ya ardhi, mke wa mtu, kugombania mali za urithi na mwisho kabisa kuwa mwenye elim katikati ya kundi la wajinga🚶🚶

Mzee aliyetoa hizo hoja hata darasan hakwenda,,,,, n Ile street smart na experience ya kutosha kwenye maisha!!
R.i.p tata
 
Kwamba kuwa mwenye elimu katikati ya wajinga ni kosa
 
Back
Top Bottom