NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Habari wakuu, nguo ni mojawapo ya mahitaji matatu muhimu. Ni hitaji muhimu lakini bajeti yake nayo inabidi ichungwe hasa kwa kina sisi ambao bado uchumi haujawa stable.
Huwa nasikitika sana nimenunua nguo lakini nikifua tu mara mbili ama mara tatu ni hohe hahe, nguo inakuwa imeanza kufifia na kuchuja, hapa kukwepa aibu ni kununua tu nyingine ila bajeti nayo inapigwa na upepo wa kisuli suli.
Nguo zenyewe hususani ni hizi jeans na cardets hata za mitumba zilizovaliwa sana huko lakini huku zikifika ukifua mara 4 mara 5 shida yani.
Tunakwepa sabuni za unga tunatumia sabuni za vipande lakini wapi, Kuna jeans yangu niliipenda sana niliifua kama mara tano hivi haitamaniki
Ni vipi tunaweza kufua nguo kwa kuhakikisha zinakaa muda mrefu?