Ni njia ipi nzuri ya kufua Nguo ili zidumu na ubora wake kwa muda mrefu bila kufifia rangi/kuchuja?

Ni njia ipi nzuri ya kufua Nguo ili zidumu na ubora wake kwa muda mrefu bila kufifia rangi/kuchuja?

maxresdefault.jpg

Habari wakuu, Nguo ni mojawapo ya mahitaji matatu muhimu. ni hitaji muhimu lakini bajeti yake nayo inabidi ichungwe hasa kwa kina sisi ambao bado uchumi haujawa stable.

huwa nasikitika sana nimenunua nguo lakini nikifua tu mara mbili ama mara tatu ni hohe hahe, nguo inakuwa imeanza kufifia na kuchuja, hapa kukwepa aibu ni kununua tu nyingine ila bajeti nayo inapigwa na upepo wa kisuli suli.

Nguo zenyewe hususan ni hizi jeans na cardets hata za mitumba zilizovaliwa sana huko lakini huku zikifika ukifua mara 4 mara 5 shida yani.

Tunakwepa sabuni za unga tunatumia sabuni za vipande lakini wapi, Kuna jeans yangu niliipenda sana niliifua kama mara tano hivi haitamaniki

Ni vipi tunaweza kufua nguo kwa kuhakikisha zinakaa mda mrefu ?
Ndugu fanya mazoezi sana, mwanaume haupaswi kuwa na MASABURI makubwa namna hiyo
 
😂Inakera mno unatamani uirudishe dukani mie napata tabu sana na mitandio Yani ukiweka kwenye maji yanabadilika rangi sikuhiz nitakuwa nanunua yenye asili ya shiffon hata magaun nilojaribu kununua ya dizain hiyo Yako vizuri ila hiz zingine ni majanga
Shiffon is the best. Hazipauki
Sina sketi 🤣 kwahiyo ni magauni tu. Ni kubadili, leo cotton kesho shifon. Shiffon hana mpinzani.

Ingawa kuna shiffon ukiipitisha kwenye kitu cha ncha kali inatoa nyuzii.
 
Mkuu jeans zetu hizi za bongo zinatoa rangi zinachuja kipindi inachuja na kutoa rangi pia na uchafu unatoka directly

Na the more you soak in soapy water the more it bleach and kupauka so solution

Usiziloeke, ukitaka kufua chukua maji yako bila soap au eka kiduchu sana then fua suuza anika

But hii ni theory yangu tu [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] mi ndo hufua hivo jeans zangu na bado zinamuonekano mzuri hata zilizonirruka

Sio wewe peke yako jinzi mimi miaka yote sifulii sabuni na tishirt na mashati nafulia sabuni ya kipande nguo zangu hudumu sana , na mara moja moja jinzi nikiona imezidi uchafu naanza kufua mashati na tishet halafu lile povu lake lisilo na nguvu ndio napitishia suruali humo nafua then nasuuza na sipaki sabuni hata ya kipande, jinzi hadi naiacha inakua na muonekano mzuri na rangi yake ile ile na ukiweza usianike nguo kwenye jua
 
Shiffon is the best. Hazipauki
Sina sketi 🤣 kwahiyo ni magauni tu. Ni kubadili, leo cotton kesho shifon. Shiffon hana mpinzani.

Ingawa kuna shiffon ukiipitisha kwenye kitu cha ncha kali inatoa nyuzii.
Ni kweli lakini nyingi ziko vizuri ila Magauni ya dizain hiyo Yako vizuri kiukweli hat kutoa rangi ni nadra lakin Sasa huwez kuvaa shiffon kilasiku shida ndo huanzia hapo
 
Nachojua kila nguo inakuwaga na maelekezo yake namna ya kuitumia ili ikae mda mrefu
Mfano kuna ambazo hutakiwi kutumia sabuni kali hutakiwi kuanika kwenye mwanga mkali wa jua etc
Ni wachache sana wanaosoma Label za kwenye nguo na kufuata maelekezo yake ,Mtu nguo kwenye Label imeandikwa "Tumble Dry" hata haelewi maana yake nini🤣🤣🤣
 
Ni kweli lakini nyingi ziko vizuri ila Magauni ya dizain hiyo Yako vizuri kiukweli hat kutoa rangi ni nadra lakin Sasa huwez kuvaa shiffon kilasiku shida ndo huanzia hapo
Kuna vigauni vimejaa town vya shiffon ni vizuri. Dizain mbali mbali. Sema nahisi we nguo fupi huvai 😂 maana tule tupo magotini
 
Sio wewe peke yako jinzi mimi miaka yote sifulii sabuni na tishirt na mashati nafulia sabuni ya kipande nguo zangu hudumu sana , na mara moja moja jinzi nikiona imezidi uchafu naanza kufua mashati na tishet halafu lile povu lake lisilo na nguvu ndio napitishia suruali humo nafua then nasuuza na sipaki sabuni hata ya kipande, jinzi hadi naiacha inakua na muonekano mzuri na rangi yake ile ile na ukiweza usianike nguo kwenye jua
Ila Sasa inategemea na shughuli zako mwingine anashughuli zinahusisha vumbi ni ngumu kufua hivo nguo
 
Kuna vigauni vimejaa town vya shiffon ni vizuri. Dizain mbali mbali. Sema nahisi we nguo fupi huvai 😂 maana tule tupo magotini
😂Huwa nanunua ndefu ila zile fupi ni nzuri sana na hat Bei zake ni nzuri pia
 
95% ya nguo zinazouzwa Madukani Bongo ni Fake au Reject za Viwandani ambazo wafanyabiashara wakienda China au Uturuki wanazinunua kwa Bei poa na wakileta huku wanapata faida zaidi ya 100%. Ni wabongo wachache sana wanaoweza kumudu kuvaa nguo OG.
Na kwa Bongo kuipata nguo OG utaikuta kwenye Mtumba iliyokwisha jambiwa na wazungu huko ilikotoka.
 
Back
Top Bottom