Ni rahisi sana Afrika (Tanzania) kurudi utumwani

Ni rahisi sana Afrika (Tanzania) kurudi utumwani

Kwani ni lini Afrika ilipata Uhuru! Bado tuko utumwani.
Tuanze harakati za kujikomboa.
Kwa Mikataba hii ya madini na bandari unadhani Sisi ni watu huru? Aibu sana

Tulipata uhuru wa bendera. Hatuna uhuru wa kiuchumi, kiutamaduni, kifrikra, kisiasa.

Unaona waliojaribu kupinga huu mkataba, polisi inawasakama na wabunge kama mpina walivyofanywa wakitetea maslahi ya Taifa.
 
Tukijitambua sawa tutakuwa baraka, kwa sasa ni shamba la bibi mzigo kwa dunia.
Tungekuwa hatuna kitu, maskini,

Hao matajiri wezi wa magharibi na Mashariki wangefuata nini Africa?

Africa ni Tajiri, na itabaki hivyo.

Africa ni Baraka Kwa Dunia nzima. Hata vita na chokochoko zote xinazoendelea Africa, waanzilishi ni Kutoka nje ya Africa, Magharibi na Mashariki.

Adui wa Africa ni Hao Kutoka mataifa nje ya Africa.

Africa umebarikiwa sana 👍🙏🙏
 
Hata Mangungo asingeuza Mali ya urithi bila kulaghaiwa na wageni.

Adui yetu anatoka nje alitumia pesa kidogo kulaghai viongozi wetu.

Africa umebarikiwa sana.

Africa inaponzwa na utajiri wake.
 
Umesema sahihi kabisa
Now it's either of the two
1.Tujifunze namna ya kuishi utumwani
2.Tutafute mbinu zitakazotusaidia tusiingie utumwani, kwa shari au amani.
 
Wangefuata Ardhi, watumwa.

Ndio Afrika ni utajiri ila utajiri wake unawanufaisha genge dogo, viongozi wachache na chawa wao na mataifa ya nnje.

Wanaishi kama watumwa kwenye nchi zao. Chakula, afya, elimu, biashara, makazi, umeme, maji, barabara, uhuru wa kujieleza, siasa, kuanzisha vyama mbadala wa CCM, vyote changamoto.

Ndio utumwa wenyewe Utumwa sio lazima chains, minyororo tena huu uliopo sasa ndio utumwa mgumu kujikomboa. Sababu wengi hawajui wako utumwani.
 
Kabla ya kupata Uhuru tulipigania tujitawale lakini kuna watu hawakuwa radhi mkoloni aondoke Africa
Kuna mataifa jirani walimkumbatia mzungu kwa mda na walibadili mambo mengi kuhusu utawala na wakafaidika kwa baadhi ya mambo hata nidhamu tu

Leo sisi na wengine kama sisi ambao tuliwafukuza na kuanza kuhujumu mali zao tuko wapi?

Kusini mwa Africa hali ni mbaya sana maana kuna wengine walifikia mpaka kuwauwa kabisa wazungu

Hawakuishia hapo maana ukishakula nyama ya mtu huwezi kuacha
Wakaanza kupigana wao kwa wao na mwisho wakawa wanauwa mpaka waafrika wenzao kisa wameingia nchini kwao

Mtu mweusi ni Bara letu ni kama tumewekwa tuishi na wanyama tu

Wazungu wameiba sana na bado wakachukua wanyama wetu na kufungua zoos kila miji na wakaiba mpaka historia zetu kama vito vya zamani walivyochonga babu zetu wakapeleka kwenye museum zao na kusema eti huku ulaya ndio safe zaidi na watu wataona vizazi na vizazi ila kwa upumbavu wetu hatujui kuwa wao ndio wanafaidika kwa kupata viingilio kila leo na ni mradi endelevu

Mwafrika ameshindwa kujenga nchi yake na kila kiongozi anayeingia analazimika awe mwizi na akubali wizi atake asitake

Sijui kwenye vipengele vya kuwa kiongozi huwa wanaambiwa funga mdomo?

Inauma kwa kweli
Sasa haya majizi na matapeli yanashirikiana na wazungu na mataifa mengine kuiba rasilimali zetu in return wanapewa na kitu
Wanachukua mikopo wakijua hata mjukuu wake hatalipa bali watakuwa wanarudisha riba tu na sio mkopo, kwa hiyo hawajali wataendelea kukopa na nusu miradi nusu mifukoni

Tusilaumu sana ni upumbavu wetu wenyewe
 
Unaona ktk uono hafifu!!

1. Madini yote,yanatoka Africa,

2. Malighafi zote hutoka Africa, ambazo hutumika kuzalisha bidhaa na vifaa vyote adimu.

3. Hata kabla ya mashine kugunduliwa, watumwa walitoka Africa kwenda kuzijenga Nchi maskini za ulaya na kuzitajirisha.

4. Mali asili ,misitu mizuri na Kila fursa zipo Africa.

5. Ni bara pekee ambapo unaweza kufanya KILIMO msimu mzima, mabara mengine ni barafu ktk baadhi ya misimu.

Narudia kusema Bila Africa, mabara mengine yasingekuwa yalivyo Leo, hivyo Africa ni BARAKA.

Hao unaowaona wamebarikiwa ndo chanzo Cha Umaskini wa Africa.

Naipenda Africa, Najivunia Kuzaliwa Africa,

Naipenda Nchi yangu nzuri TANZANIA, pia Najivunia Kuzaliwa Tanzania.

Aamen.
So what.sasa kama una vitu vyote hivyo alafu havikunufaishi kama huna laana ni nini?.
 
Unaona ktk uono hafifu!!

1. Madini yote,yanatoka Africa,

2. Malighafi zote hutoka Africa, ambazo hutumika kuzalisha bidhaa na vifaa vyote adimu.

3. Hata kabla ya mashine kugunduliwa, watumwa walitoka Africa kwenda kuzijenga Nchi maskini za ulaya na kuzitajirisha.

4. Mali asili ,misitu mizuri na Kila fursa zipo Africa.

5. Ni bara pekee ambapo unaweza kufanya KILIMO msimu mzima, mabara mengine ni barafu ktk baadhi ya misimu.

Narudia kusema Bila Africa, mabara mengine yasingekuwa yalivyo Leo, hivyo Africa ni BARAKA.

Hao unaowaona wamebarikiwa ndo chanzo Cha Umaskini wa Africa.

Naipenda Africa, Najivunia Kuzaliwa Africa,

Naipenda Nchi yangu nzuri TANZANIA, pia Najivunia Kuzaliwa Tanzania.

Aamen.
Changamoto ni watu wanavyofikiria.
Ardhi, anga na vyote viijazavyo ni baraka tele.
 
Hata Mangungo asingeuza Mali ya urithi bila kulaghaiwa na wageni.

Adui yetu anatoka nje alitumia pesa kidogo kulaghai viongozi wetu.

Africa umebarikiwa sana.

Africa inaponzwa na utajiri wake.
Baraka namba moja ni kua na akili.kama huna akili umelaaniwa.Kubali huu ukweli ili tujikomboe kuitafuta akili kwa vizazi vyetu vijavyo badala ya kujifariji.
 
Baraka namba moja ni kua na akili.kama huna akili umelaaniwa.Kubali huu ukweli ili tujikomboe kuitafuta akili kwa vizazi vyetu vijavyo badala ya kujifariji.
Akili ni kumtafuta, kumjua Mungu, kuwa na HOFU ya Mungu.

Africa ndiyo inakwenda kuinuka juu sana katika Kila kitu, kiuchumi, kimaarifa kisiasa nk nk.

Sababu kuu ni Mungu anatafutwa sana na Waafrica na wanamkubali.

Mabara mengine yanakwenda kufifia Ili Afrika ipae zaidi.

Usipoyaona Leo, panda mabegani mwa watoto na vitukuu uyachungulie nikuambiayo Kisha moyo wako ujae furaha tele.

Amen
 
Anaye kuambia kuwa mwafrica umelaaniwa, mrudie na kumwelewesha jinsi ULIVYOBARIKIWA baada ya kusoma HEKIMA za MUNGU Kupitia Kwa Rabbon.

Amen
 
Baraka namba moja ni kua na akili.kama huna akili umelaaniwa.Kubali huu ukweli ili tujikomboe kuitafuta akili kwa vizazi vyetu vijavyo badala ya kujifariji.
Yep tungeanza na katiba mpya, elimu ya kuwajenga watoto wao kuchambua vitu na kufanya maamuzi sahihi. Walimu wetu waheshimike na kulipwa vyema wawe proud na kazi zao. Mitaala izingatie mazingira yetu.

Afrika inabidi iwe kama au juu zaidi kimaendeleo ya UAE, Singapore, South Korea, Ulaya, USA, South Amerika, Canada zaidi ya hao wote.

Tuna kila kitu kasoro akili za kusimamia rasimali zetu, kupambana mazingira yetu, kupata viongozi sahihi.
 
Akili ni kumtafuta, kumjua Mungu, kuwa na HOFU ya Mungu.

Africa ndiyo inakwenda kuinuka juu sana katika Kila kitu, kiuchumi, kimaarifa kisiasa nk nk.

Sababu kuu ni Mungu anatafutwa sana na Waafrica na wanamkubali.

Mabara mengine yanakwenda kufifia Ili Afrika ipae zaidi.

Usipoyaona Leo, panda mabegani mwa watoto na vitukuu uyachungulie nikuambiayo Kisha moyo wako ujae furaha tele.

Amen
Huyo Mungu anatafutwa kwani amejificha?

Anacho jifichia ni nini? Hadi atafutwe?

Kwamba kigezo cha bara au taifa fulani kufanikiwa ni kuwa na hofu ya Mungu?

Je Ulaya na America walikuwa na hofu ya Mungu, ndicho kilicho wafanya wafanikiwe?

Una elezea nadharia zisizo na uhusiano wowote wala mantiki kwenye mafanikio ya Taifa.

HAKUNA uhusiano wowote wa Taifa kumjua Mungu na kufanikiwa.
 
Ukiweza kula na kunywa na kufurahi ndio utajiri wenyewe.

Mengine ya ziada ni UBATILI mtupu na kujilisha Upepo.
Watanzania wangapi wanaweza kula, kunywa na kufurahi.

School ya mtoto, ukiumwa, kodi, tozo, bei za chakula, mafuta, kazi, mazingira ya biashara, umeme, maji safi na salama vyote vigumu unavipata kwa mbinde.

Kwenye mazingira kama haya unapataje furaha? Lazima umtegemee Mungu kuendelea kuishi na uishi katika imani.
 
Mwarabu anataka kurudi enzi za babu zao wanatawala ukanda huu. Project yake ya mwanzo anayoanza nayo ni kutawala kiuchumi, ndiyo haya ya bandari. Baadaye atatanua wingo na kujiingiza kwenye siasa za nchi akitumia hawahawa machawa aliowapata. Upande wa dini hana shida sana tayari huko ana majuha ya kutosha yaliyomeza dini yao ikawa ni sehemu ya maisha yao huwaambii kitu hapo. Kutawaliwa kiuchumi na kitamaduni kumeanza kushika kasi. Kuna kitabu kinaitwa kwaheri uhuru karibu utumwa, mwandishi wake aliona mbali
 
Huyo Mungu anatafutwa kwani amejificha?

Anacho jifichia ni nini? Hadi atafutwe?

Kwamba kigezo cha bara au taifa fulani kufanikiwa ni kuwa na hofu ya Mungu?

Je Ulaya na America walikuwa na hofu ya Mungu, ndicho kilicho wafanya wafanikiwe?

Una elezea nadharia zisizo na uhusiano wowote wala mantiki kwenye mafanikio ya Taifa.

HAKUNA uhusiano wowote wa Taifa kumjua Mungu na kufanikiwa.
Hukusoma kuwa,

Kumcha Mungu ni chanzo Cha HEKIMA na MAARIFA?
 
Back
Top Bottom