Of course maendeleo ya USA, Ulaya, Uarabuni yameletwa na ukatili mkubwa na wa ajabu. Red Indians kutokomezwa karibu America nzima. Biashara ya utumwa Watumwa kuwatumikisha mamilioni kwa mamilioni ya kwa zaidi ya miaka 600 wazungu, 1300 waarabu.
Wametuachia souvernir ya dini, udini, ukabila tutsi, hutu tuendelee kutengana na kupigana.
Miaka ya zamani kabla ya uwepo wa mashine za kufanya kazi, Watumwa ndio ilikua njia pekee ya kurahisisha ufanyaji kazi.
Sasa kwa jamii ya watu wanyonge, Lazima wange geuzwa watumwa.
Waafrika walikuwa wanyonge, Wajinga na Hawana umoja tangu zamani, Ndio maana ilikuwa rahisi kwa wazungu na waarabu kuwalaghai machifu kwa kuwapa vizawadi kisha wao waka patiwa watumwa.
Yaani, Chifu aliona ni sawa kabisa kuwauza raia wake utumwani ili tu yeye apewe zawadi na fedha.
Sasa unaona ni namna gani waafrika walikuwa wajinga tangu zamani.
Ukiangalia nchi kama Norway, Denmark,Finland, Sweden, Haziku tawala nchi yeyote ya Afrika lakini leo hii zina Maendeleo makubwa.
Pia nchi kama Singapore, Korea, Qatar, UAE, India nazo zilitawaliwa pia lakini wamefanikiwa kujikwamua kiuchumi na kupata maendeleo.
Waafrika tu, ndio tumeshindwa kujiongoza na kujitawala bado tunarudi kwa wakoloni walewale kuwa omba misaada na mikopo.
Viongozi wa Afrika wanadhani mikopo na misaada ya nje ndio itawaletea maendeleo.
Wanasahau kwamba, There is no free lunch. Kwamba hakuna cha bure bure dunia hii.