Ni sababu ipi muhimu sisi wazazi tunakuwa na mtoto zaidi ya mmoja?

Ni sababu ipi muhimu sisi wazazi tunakuwa na mtoto zaidi ya mmoja?

Kila mtu ana wajibu wa kuitunza dunia ili si tu iendelee kuwapo kwa vizazi vijavyo, bali pia iwe na mazingira bora. Pengine hata mazingira bora zaidi ya yaliyopo sasa.

Kama mimi nilivyoikuta dunia haijaharibiwa na walioniachia, na mimi nataka niwaachie wengine dunia ambayo sijachangia kuiharibu sana. It's only reasonable for any person who is not overly selfish.

Ni kama vile nimepewa switch ya kuchangia kuilipua dunia kwa kiasi fulani kidogo, nikaambiwa unaweza kuibonyeza switch hii na kupata personal glory ya kuwa na watoto wengi, ukaiharibu dunia kwa watoto wa watoto wa watoto wa watoto wao, au unaweza ukakataa kubonyeza switch hiyo, na kuwa na mtoto mmoja.

Uamuzi wangu wa kuwa na mtoto mmoja umekuwa rahisi zaidi kwa sababu mimi, kinyume na watu wengi, sioni kuwa na watoto wengi kuwa ni jambo la fahari.

I am more about quality of life ninayompa mtoto mmoja kuliko quantity of life ya kuwa na watoto wengi.

Na pia, kwa watu ambao tunatoka familia ambazo tayari zina utamaduni wa kuzaa watoto wengi, kuna watoto wengi sana wa familia wanahitaji kulelewa, na watoto hao wanakua kwenye umasikini na kuwa watu wazima tegemezi, tunaweza kuanza kusaidiana kuumaliza au kuupunguza umasikini kwa watu waliopo kwanza, kabla ya kuongeza watu wengine wengi tu ambao tunaweza ku struggle kuwapa maisha mazuri.
Hii last paragraph imekuwa bora sana.
 
Hii last paragraph imekuwa bora sana.

Ndiyo hivyo mkuu.

Mimi nina mtoto mmoja wa kuzalisha mimi mwenyewe, lakini ninalipia ada watoto zaidi kwenye familia, watoto ambao wazazi wao hawana uwezo.

Hivyo bado nina watoto wengi ninaowalea kwa jinsi yangu katika familia, licha ya kuwa na mtoto mmoja wa kuzalisha mimi mwenyewe.

Sasa hapo napo bado niongeze watoto tu?

Yani hawa waliopo tu kwenye familia zetu kuwasomesha wote vizuri naona kuna mgogoro, bado tufyatue zaidi tu?
 
Moyo wa kujitolea ni mdogo sana. Na hiki ni kikwazo kikubwa cha mafanikio.

Kifupi, kwa Waafrika wengi ukimwambia chagua wewe na ndugu zako wote mzaliwe katika ulimwengu wenye umasikini mkubwa, au wewe usizaliwe, na ndugu zako waishi maisha mazuri sana, wengi watachagua wazaliwe halafu wote wagawane umasikini.

Ndiyo tafsiri ya mtoto wa tisa wa Afrika kusononeka kwenye maongezi haya hapo.
 
Ni kweli, sisi tumezaliwa wawili tuu, mama yangu kilasiku anasema anajuta kuzaa watoto wachache, hua naona watoto wa mama mdogo wengi wanavyosaidiana na kupendana
Shida hapo ni umaskini, sio uchache wa idadi yenu.
 
Moyo wa kujitolea ni mdogo sana. Na hiki ni kikwazo kikubwa cha mafanikio.

Kifupi, kwa Waafrika wengi ukimwambia chagua wewe na ndugu zako wote mzaliwe katika ulimwengu wenye umasikini mkubwa, au wewe usizaliwe, na ndugu zako waishi maisha mazuri sana, wengi watachagua wazaliwe halafu wote wagawane umasikini.

Ndiyo tafsiri ya mtoto wa tisa wa Afrika kusononeka kwenye maongezi haya hapo.
I see!
 
Dream Queen, I used to think we share similar perspectives. Here we differ.
Tatizo watu wanapenda kua serious muda wote, ile comment ya mwanzo kabisa kabla hicho kibabu hakijaja kunivamia ilikua ya kichokozi tu,

Btw, kwenye suala la watoto wengi tupo pamoja, it's not good kua na msururu wa watoto halafu huduma sifuri, elimu duni, afya mgogoro, yaan mzazi badala ya kuzaa ili amuwezeshe mtoto yeye anazaa ili mtoto aje amuwezeshe yeye bila kumuandalia mazingira wezeshi.
 
Tatizo watu wanapenda kua serious muda wote, ile comment ya mwanzo kabisa kabla hicho kibabu hakijaja kunivamia ilikua ya kichokozi tu,

Btw, kwenye suala la watoto wengi tupo pamoja, it's not good kua na msururu wa watoto halafu huduma sifuri, elimu duni, afya mgogoro, yaan mzazi badala ya kuzaa ili amuwezeshe mtoto yeye anazaa ili mtoto aje amuwezeshe yeye bila kumuandalia mazingira wezeshi.
Thank you, thank you. That is The Dream Queen I know, I am proud of you.
 
Hapa tatizo ni umaskini wa wazazi wala sio idadi chache ya watoto. Matajiri hata wasio na watoto wanaweza kuhudumiwa kwa huduma bora kabisa katika

Hapa tatizo ni umaskini wa wazazi wala sio idadi chache ya watoto. Matajiri hata wasio na watoto wanaweza kuhudumiwa kwa huduma bora kabisa katika wakati wowote na hali yoyote.
Nakubaliana na ww kwa asilimia kadhaa tu, ila ukweli HELA SIO suluhisho la kila jambo. Hiyo mifano niliyotoa hapo juu shida haikua pesa bali ni issue ya utu, ubinadamu, upndo, ukaribu watu wanataka uwepo wako etc etc ambavyo havijengwi ktk misingi ya pesa.
 
Habari za muda huu ndugu zangu. Nimekaa, nikafikiria, Mimi ni mzazi wa mtoto mmoja wa kike.

Sasa issue kubwa nataka kufahamu nimeona kama nimeridhika au sina sababu maalumu ya kuongeza mtoto. Najiweza sana kiuchumi, mimi kijana mdogo ila mwanangu yupo anaishi na mama yake Uingereza (Mama mtanzania age 27) nilimpeleka mwenyewe. Anajiweza. Na pia sipo nae kimahusiano kwa sasa ila nina mtunza huyu binti.

(Nia nikutoa point za uchumi na uhusiano). Sasa sina Wazo lolote la kuongeza mtoto, yaani nina mapenzi yaliyopitiliza kwa huyu niliye nae.

Wazee sababu ipi inafanya mtu awe na watoto zaidi ya mmoja au wengine kupitiliza hadi watano. Nini sababu?

Au huwaga ni bahati mbaya tu, mimba hiyo?


Utoto raha sana
 
Suala la kuzaa watoto wangapi, au kutozaa kabisa, ni la utashi wa mtu binafsi. Ni haki ya mtu binafsi. Hapo hakuna mwanya wa haki hiyo kuingiliwa bila kuvunja haki za kikatiba na za kibinadamu za huyo mtu.

Ila.

Kuzaa kwa hesabu zozote za watoto kuja kukusaidia kwa namna yoyote baadaye ni aina fulani ya biashara, tena biashara ya utumwa.

Watu wanatakiwa wazae bila mategemeo yoyote ya kulipwa fadhila yoyote na watoto, hata ya kutunzwa uzeeni. Wajiwekee mipango yao wenyewe.

Kwa sababu.

Kwanza mtu hawezi kujua kwamba mtoto wake ataishi maisha marefu kumpita yeye. Inawezekana mtoto akafariki awali.

Pili, si maadili mema kuzaa kwa lengo la kibiashara. Kwamba mimi namzaa mtoto namtunza ili naye aje anitunze. Hiyo si familia, hiyo ni biashara ya kutunzana.

Vipi kama mtoto hana interest yoyote ya kutunza wazazi, yeye anataka kuishi kwa uhuru wake akae mbali akiendesha maisha yake? Hiyo ni haki yake. Utataka aache maisha yake amtunze mzazi?

Hiyo ni sababu moja ya kibinafsi kabisa ya kuzaa watoto.

Sisemi kwamba kumtunza mzazi ni kitu kibaya, nasema kwamba, mzazi kuweka mahesabu kwamba nazaa watoto wengi waje kunitunza vizuri baadaye ni kama kuwafanya wale watoto ni watumwa wake, kazaa watumwa wengi waje kumtumikia, kawekeza kibiashara, hajazaa kifamilia.
Ndo maana watu wa siku hizi wamekosa baraka mpaka wanafikia kuwa viongozi ilihali wanavaa suruali tobovu tena kwa makusudi.

Kwa nini mzazi asitarajie chochote kutoka kwa mtoto aliyemzaa?

Punguzeni umagharibi na usasa mtazikwa na vihereni.
 
Italy wamepunguza population tena wana mpango wa kupungua zaidi.

Watu wengi wameshtuka dunia sio salama ,kuzaa watoto wachache hata kuchelewa kuzaa na wapo ambao hawazai kabisa.

Zamani mtoto kuishi ni rahisi ila sasa lazima uwe vizuri kiuchumi la sivyo utajuta
.
Uchumi uchumi, mna overate sana mambo.
 
Ndo maana watu wa siku hizi wamekosa baraka mpaka wanafikia kuwa viongozi ilihali wanavaa suruali tobovu tena kwa makusudi.

Kwa nini mzazi asitarajie chochote kutoka kwa mtoto aliyemzaa?

Punguzeni umagharibi na usasa mtazikwa na vihereni.
Mzazi akizaa huku akitarajia chochote kwa mtoto anazaa kwa biashara, ya kutunza mtoto na kutarajia kulipwa.

Kulea mtoto si biashara, ni wajibu wa kifamilia tu.
 
Back
Top Bottom