Ni sababu ipi muhimu sisi wazazi tunakuwa na mtoto zaidi ya mmoja?

Mkuu, kwa hiyo hapo, kila mwanamke atazaa watoto 2.1. Kimahesabu, hii maana yake nini? Tufafanulie!
Mkuu, hakuna mtoto 0.1 hivyo hakuna mwanamke atakayezaa watoto 2.1.

2.1 ni namba ya average ya watoto wanaotakiwa kuzaliwa ili kupata perfect replacement, hiyo ni kwa ajili ya hesabu, average.

Hii ni average.

Niliandika hivi.

Watu wanne, couples mbili, wakiwa na watoto watatu, couple moja ina watoto wawili, nyingine ina mtoto mmoja, kwa average hapo kila couple ina mtoto 1.5

Unachukua idadi ya watoto watatu, inaigawanya kwa idadi ya couples, mbili.

3/2 = 1.5.

Average ni 1.5 children per couple.

Kama kuna kitu hujaelewa hapa, naomba unishirikishe.
 
Hiyo definition si relevant period, kwa sababu ina assumption ambayo umeshindwa kui prove.

Mkuu, hakuna mtoto 0.1 hivyo hakuna mwanamke atakayezaa watoto 2.1.

2.1 ni namba ya average ya watoto wanaotakiwa kuzaliwa ili kupata perfect replacement, hiyo ni kwa ajili ya hesabu, average.

Hii ni average.

Niliandika hivi.

Watu wanne, couples mbili, wakiwa na watoto watatu, couple moja ina watoto wawili, nyingine ina mtoto mmoja, kwa average hapo kila couple ina mtoto 1.5

Unachukua idadi ya watoto watatu, inaigawanya kwa idadi ya couples, mbili.

3/2 = 1.5.

Average ni 1.5 children per couple.

Kama kuna kitu hujaelewa hapa, naomba unishirikishe.
Kwahiyo "couple moja" watazaa mtoto mmoja na nusu, unamaanisha hivyo? Najuwa unaongelea average, lakini jambo lolote lazima lireflect uhalisia hata kama ni average. Tuambie, average ya mtoto mmoja na nusu kwa kila couple, maana yake nini? Hakuna couple (mme na mke) waliowahi kuzaaa nusu mtoto, au robo mtoto, au thetuthi!
 
Ukizichukua namba nyingi, ukatafuta average ya hizo namba, average si lazima iwe namba yoyote kati ya hizo namba, average inaweza kuwa namba tofauti kabisa.

Kwa mfano, average ya 2 na 1 ni 1.5 (3/2).

Hivyo hivyo, idadi ya average watoto wanaotakiwa kufanya perfect replacement haihitaji kuwa idadi ambayo mwanamke yeyote kazaa, hii ni numerical average, si idadi ya watoto ambayo mwanamke yeyote kazaa.

Ukiwa na couples mbili, moja ina watoto 2 , nyingine ina 1, average ya watoto per couple ni 3/2, ni watoto 1.5 per couple. Hii ni average number, si actual children ambao any couple itazaa. Hakuna mtoto 0.5.

Usichoelewa ni kipi hapo?
 
Nyie zaeni kidogo, Wenetu wa Kanda ya Ziwa watajazia kwenye magap hapo.
 
Mkuu,

Mimi ni kama wewe, nilipata mmoja tu nikaridhika.

Kama unapenda dunia iendelee kuwa na watu, unatakiwa angalau kuwa na watoto wawili.

Actually kimahesabu ya takwimu tunatakiwa kuwa na average ya watoto 2.1, hii ndiyo replacement rate.

Ukiwa na mtoto mmoja wewe, na dunia nzima ikiwa na mtoto mmoja average, maana yake kizazi kinachofuata kitakuwa nusu ya kizazi hiki, na kinachokifuatia kitakuwa nusu ya hiki, mpaka kizazi kitaisha.
Kwa hiyo lengo lenu ni kumaliza uwepo wa wanadamu?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Mkuu tumepigwa bao 41-1 na mpiga bass wa "Bob Marley and the Wailers" Aston "Family Man" Barret aliyefariki February 3 2024 akiwa na miaka 77.

Jamaa alipata watoto 41 katika maisha yake.

Huyu legend hakutegeategea kazi.

Tabu Ley alikuwa na angalau 104, wanaojulikana rasmi.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo lengo lenu ni kumaliza uwepo wa wanadamu?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Mkuu,

Mimi mtu mmoja ninamaliza vipi uwepo wa hao unaowaita wanadamu?

Mimi nafanya mamuzi yangu, kwenye maisha yangu, na vizazi vyangu.

Hao unaowaita wanaadamu kwanza hata siwajui.
 
Tabu Ley alikuwa na angalau 104, wanaojulikana rasmi.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Mkuu watoto 104 hapo lazima kutakuwa na wakubambikiwa.

Tabu Ley kafariki akiwa na miaka 73. Tuseme kaanza kuzalisha akiwa na miaka 16 kama yeye rijali barubaru sana.

73 - 16 = 57.

Haya. Muondolee miaka mitatu ya uzeeni huko labda alikuwa anaumwa mzee hakuzalisha.

57 - 3 = 54.

Anabakiwa na miaka 54 ya kuzalisha.

104/ 54 = 1.92.

Karibu watoto wawili kwa mwaka kwa miaka 54.
 
Habari za muda huu ndugu zangu. Nimekaa, nikafikiria, Mimi ni mzazi wa mtoto mmoja wa kike.

Sasa issue kubwa nataka kufahamu nimeona kama nimeridhika au sina sababu maalumu ya kuongeza mtoto. Najiweza sana kiuchumi, mimi kijana mdogo ila mwanangu yupo anaishi na mama yake Uingereza (Mama mtanzania age 27) nilimpeleka mwenyewe. Anajiweza. Na pia sipo nae kimahusiano kwa sasa ila nina mtunza huyu binti.

(Nia nikutoa point za uchumi na uhusiano). Sasa sina Wazo lolote la kuongeza mtoto, yaani nina mapenzi yaliyopitiliza kwa huyu niliye nae.

Wazee sababu ipi inafanya mtu awe na watoto zaidi ya mmoja au wengine kupitiliza hadi watano. Nini sababu?

Au huwaga ni bahati mbaya tu, mimba hiyo?
Naona bado hujaota ndoto inayokuonesha kuwa huyo mmoja hakutoshi
 
Inaweza kufikia mpaka nchi kuishiwa na watu kabisa.

Hili tatizo linaonekana kama utani, ila South Korea wanalipitia sasa hivi.

Kuna kampuni ya ujenzi ya South Korea inatoa fedha kiasi cha US dollar 75,000 kwa kila mfanyakazi ambaye amepata mtoto ndani ya miaka miwili iliyopita, au atakayepata mtoto.

Hii ni kupambana na "population decline" huko South Korea.

Watu wamegoma kuzaana.

Mtihani ni kwamba, inaonekana kuwa kadiri nchi zinavyopata maendeleo ya kiuchumi na watu kuelimika, na maisha kupanda gharama, watu wanaamua kuzaa watoto wachache zaidi.

Samahani Mkuu, hivi hawa watu wa Far East wana shida gani? Maana Japan nao wana shida kama Korea Kusini. Je, ni sababu za kibayolojia au kinasaba zinazosababisha hali hii? Nchi hizo kwa sasa ndizo zinazoongoza kwa hali bora za kimaisha na hata binadamu mwenye umri mkubwa yupo maeneo hayo. Ni nini kinasababisha waogope kutungisha mimba?

Aidha, tamthilia za huko zote zina theme ya kugombea watoto au wizi wa watoto.
 
Sasa kama mtoto mwenyewe ni mmoja na keshampeleka mbali na anapoishi, hiyo attention anampatia nani? au kujichukulia sheria mkononi ndiyo mpango mzima? Zaidi ya hayo, kama suala ni attention au mahaba niuwe; huyo mtoto akikua akaolewa bado atakwenda naye huko kwa mkwewe?

Hapa kuna zaidi ya attention
 
Samahani Mkuu, hivi hawa watu wa Far East wana shida gani? Maana Japan nao wana shida kama Korea Kusini. Je, ni sababu za kibayolojia au kinasaba zinazosababisha hali hii? Nchi hizo kwa sasa ndizo zinazoongoza kwa hali bora za kimaisha na hata binadamu mwenye umri mkubwa yupo maeneo hayo. Ni nini kinasababisha waogope kutungisha mimba?

Aidha, tamthilia za huko zote zina theme ya kugombea watoto au wizi wa watoto.

Sio Far East tu, karibu nusubya dunia inaelekea kushindwa kufikisha "replacement level" ambayo ni watoto wawili.

Angalia hapa chini, nchi yyote yenye fertility rate under 2.2 bila ya immigration ina hatari ya kufutika.

Nchi nyingi bila kupata wahamiaji kutoka nje zitatoweka.

Unavyozidi kuongeza maendeleo ya kielimu na kiuchumi ndivyo unazidi kuona maisha ni pointless.

Unavyozidi kuona maendeleo ya kiuchumi na kielimu yanaonesha kuwa si tu maisha ni pointless, bali pia maendeleo yanazidisha matatizo na stress na kukosa maendeleo pia ni tatizo, unaona maisha ni trap.

Hizo jamii zimeamua kujitoa katika maisha. Zimepita level ya maisha.

Kwenye Buddhism wanasema all existence is suffering. Wao wameamua kuondoka katika existence polepole, na hivyo kuondoka katika suffering.

Mwanamuziki nguli wa Tanzania Mbaraka Mwinshehe aliwahi kuimba "Kila siku shida, shida haiishi mpaka siku ya mwisho".

Hawa watu wamekubaliana na falsafa za Mbaraka Mwinshehe. Wamekubali maisha ni shida, na wamekataa kuzalisha watu zaidi kuwaleta dunia hii yenye shida nyingi. Washaona dunia inayokuja itakuwa na matatizo mengi sana mambo ya climate change, Artificial Intelligence, chakula, mazingira etc. Wameona wawaepushe hao watoto na matatizo haya kwa kutowazaa.

Watu wasioelewa dunia inaendaje ndio wanazaana kwa mafungu bado.
 
Nakushukuru sana Mkuu kwa maelezo haya yaliyoshiba. Sasa mbona serikali zao zinapiga Kampeni za kuzaana? Ina maana serikali haioni ni vyema Taifa likafutika tuu ili kuepukana na yale yajayo?

Kumbe bado sisi weusi hatujui lolote kuhusiana na majanga yaliyopo mbele yetu!

Bado shida tunayo.
 
Wanasiasa walio kwenye madaraka wanahitaji watu wazaane iki wapate walipa kodi wa kuwa sustain, lazima wapigie debe kuzaana ili nchi zao zisifutike.
 
Back
Top Bottom