Ni sababu zipi zinazofanya kupotea kwa Ben Rabiu Saanane lionekane ni jambo dogo mbele ya vyombo vya dola?

Ni sababu zipi zinazofanya kupotea kwa Ben Rabiu Saanane lionekane ni jambo dogo mbele ya vyombo vya dola?

Ulichokiandika ni sawa kwa kadiri ya unavyotaka tupokee.Lakini,ni ajabu wewe hupendi wala hautaki kuambiwa usiyoyataka na wengine.Tatizo lilikuwa wapi muda ule?Ukiulizwa jina lako unaitwa nani,chimbuko la wazazi wako nk,si unatakiwa ujibu tu?Unadodoswa,mtu anapotea.Unapewa changamoto za uongozi,unahutubia umma.Baada ya dakika tano mtu aliyekupa changamoto ananyukwa risasi nyingi mwilini.Tukuweke kundi gani?Tukufikiriaje?Unatuondoleaje fikra hasi juu yako?.Hapo bado kuna ya akina mchungaji Mwingira na wanasiasa wengine waliowekwa under-pressure(blackmail) ili waunge juhudi zisizoeleweka.
Nimeongelea elimu yake sijaongelea hulka yake binafsi. Hata Samia amekuwa wazi kwamba maoni ni haki ya raia, muda wote yanawekwa wazi ili jamii iweze kuyasikia.

Tatizo ni kutumia huo uhuru vibaya kwa kujisahau kuwa uhuru unakwenda sambamba na wajibu binafsi wa huyo anayekuwa nao. Samia baada ya kuwapa uhuru mwingi kina Mdude na wengine akakumbusha juu ya wajibu wao kwenye jamii.

Uhuru unapozidi sana kwenye jamii unazaa ujinga, unazaa tabia ya kutowajibika kwani kila anachoambiwa mtu anaona furaha kukihoji na kuja na hoja hasi juu yake.
 
Nimeongelea elimu yake sijaongelea hulka yake binafsi. Hata Samia amekuwa wazi kwamba maoni ni haki ya raia, muda wote yanawekwa wazi ili jamii iweze kuyasikia.

Tatizo ni kutumia huo uhuru vibaya kwa kujisahau kuwa uhuru unakwenda sambamba na wajibu binafsi wa huyo anayekuwa nao. Samia baada ya kuwapa uhuru mwingi kina Mdude na wengine akakumbusha juu ya wajibu wao kwenye jamii.

Uhuru unapozidi sana kwenye jamii unazaa ujinga, unazaa tabia ya kutowajibika kwani kila anachoambiwa mtu anaona furaha kukihoji na kuja na hoja hasi juu yake.
Bado unazunguka tu.Unajichosha.Umeeleza kuhusu yeye kujiendeleza kielimu,sawa.Na ni hapo palipo leta shida.Angeonesha uhalali wa alichoulizwa halafu muulizaji (umma)aridhike kulikuwa na shida gani?Hofu na makasiriko ya nini?Alilewa mamlaka,akasahau maadili ya dini yake kuhusu kusamehe 7×70,uvumilivu,upole na kiasi kisicho na kipimo?Angeosha mikono yake na kujiweka kando tu.
 
Magufuli maisha yake yote alikuwa mwalimu na alijiendeleza baada ya kupata Masters na ushahidi wa picha siku anapata hiyo shahada upo mitandaoni akiwa amekaa pembeni ya Mama yake.

JPM alichukiwa kwa sababu ya misimamo yake ya kutotaka ujinga huko serikalini. Alikuwa na maadui wengi hivyo haikuwa ajabu kumtengenezea hizo habari zikiwa ni sehemu ya chuki.
PhD Thesis yake inapatikana wapi??
 
Iko hivi:

Serikali zote duniani zina damu nazo huua na kutesa watu wanaoonekana kuwa ni hatari kwao. Hata hapa Bongo awamu zote zimeua na kutesa watu - kwa viwango tofauti. Cha muhimu tu ni kuwa mwangalifu unapopambana nazo na uwe tayari kwa lo lote; maana unaweza kuishia kuteswa kama Dr. Ulimboka na hata kuuliwa kama Ben Saanane na watu unaodhani kuwa unawapigania wala wasijali.

Kuhusu Lissu ni mama huyu huyu aliyetoa kauli kuwa waliojaribu kumuua hawakuwa watu wa serikalini maana watu wa serikalini wasingeweza kupiga risasi zote zile na wasiue. Huyu alikuwa makamu na kauli yake hii bila shaka ililengwa kusema kwamba serikali haikuhusika katika jaribio hilo.

Labda ukweli utajulikana siku moja; na wahusika kushughulikiwa. Hii bila shaka itawezekana tu pale CCM itakapoondoka madarakani!
Kwamba anajua na ana uhakika,wale wauaji wa serikali wana shabaha nzuri sana?Huua kabisa?🤔🤔🤔🤔🤔
 
Hakuna tukio limewahi kuniuma kama la Ben Saanane.
Mbaya zaidi nyakati zake za mwisho hapa JF tulitokea kuwa marafiki wakubwa, akifurahia sana ubuyu wangu kule celebrities forum.

Kupotea kwake kulinifanya nimchukie sana bwana yule! Ila, Mungu anajua zaidi.
Nami pia ndio maana ule moto ni wa makaa ya mawe uliochanganywa na LGP,yaani kila mara nikifikiria kuhusu family yake, hasira zinanichemka mno,ila ukweli utakuja kujulikana hadi kama itachukua miaka 100,Akwilina eti ameuawa na risasi iliyotoka juu na mashetani haya bado yanakwenda kwenye nyumba za ibada, ipo siku familia zao zitajibia haya,familia ya Akwilina haijapata closure kuhusu kuuliwa kwa mpendwa wao
 
Huko kutaka kunyoosha tu watu hata kwa minor issues hakutofautiani na akili za cave-men!Akili za medieval times ziachwe.Mujarabu wa swali ni jibu.Siyo kununa na kutumia bunduki au mabavu.Dunia yote ikiwa hivyo itakuwaje mustakabali wake?
Aisee duniani huko kunatisha sana Bora yetu sisi hapa.
Angalia tu assassinations Kwa majirani zetu ndi utajua sisi bado
 
Back
Top Bottom