Ulichokiandika ni sawa kwa kadiri ya unavyotaka tupokee.Lakini,ni ajabu wewe hupendi wala hautaki kuambiwa usiyoyataka na wengine.Tatizo lilikuwa wapi muda ule?Ukiulizwa jina lako unaitwa nani,chimbuko la wazazi wako nk,si unatakiwa ujibu tu?Unadodoswa,mtu anapotea.Unapewa changamoto za uongozi,unahutubia umma.Baada ya dakika tano mtu aliyekupa changamoto ananyukwa risasi nyingi mwilini.Tukuweke kundi gani?Tukufikiriaje?Unatuondoleaje fikra hasi juu yako?.Hapo bado kuna ya akina mchungaji Mwingira na wanasiasa wengine waliowekwa under-pressure(blackmail) ili waunge juhudi zisizoeleweka.