#COVID19 Ni sahihi Humphrey Polepole kuonesha Msimamo wake wa kutochanjwa?

#COVID19 Ni sahihi Humphrey Polepole kuonesha Msimamo wake wa kutochanjwa?

Tumeona Viongozi mbalimbali wakitumia hiari yao kuhamasisha watu wakachanjwe na wengine wamekua sehemu ya kuchanjwa kama kuonesha mfano.

Polepole Naye yupo na msimamo wake wa kutochanjwa na ameenda mbali akihimiza watu wazingatie vyakula na vilevile kahoji kwanini hii chanjo haioneshi muda sahihi wa kufanya kazi tofauti na chanjo zingine.

Polepole yupo sahihi, ikionesha tayari wakubwa zake ambao ni Rais na mwenyekit wake wanaipigia chapuo chanjo?View attachment 1883817

View attachment 1883818
Hivi huyu nae bado anawasumbua? Naona sasa kaamua kufufua kale kataasisi kake pale makumbusho atakatishe kipato.
 
Anaposema usichanje anatoa mbinu mbadala namna ya kujikinga na ugonjwa huu. Anasema punguza kula vyakula visivyo na virutubisho, fuata masharti mengine kama kunawa mikono. Upotoshaji upi anafanya!?
Hana ruhusa ya kupinga amri ya serikali,anaweza eleza hayo watoto wake kimya kimya vinginevyo watu kama yeye ingekuwa china angekuwa kasagwa zamani sana.
 
Hana ruhusa ya kupinga amri ya serikali,anaweza eleza hayo watoto wake kimya kimya vinginevyo watu kama yeye ingekuwa china angekuwa kasagwa zamani sana.
TBC kila siku wanatwambia chanjo ni hiari tena wanatumia hata wasanii kutushawishi juu ya hili. Hakuna mahali TBC ( Televisheni ya Taifa chini ya serikali ya Mama Samia) inatangaza kuwa chanjo ni amri!

Muacheni Mheshimiwa H Polepole afurahie demokrasia na haki yake aliyonayo kwenye chama cha CCM na serikali ya sasa ya Mama Samia.

Asubuhi njema.
 
Poleole hana moral authority ya kushawishi mtu leo!!
Alipokuw mwanaharakati tulikuwa tunamsikiliza kwani alikuwa na akili.
Kwa sasa hivi baada ya kuwa mtu wa mwendazake kwa miaka 6 hana thamani tena kwa wapenda ukweli na haki!!!
Kigeugeu huyo!!!!’
Kumbuka alisema nini alipokuwa katika kamati ya Rasimu ya katiba na alisema nini kuhusu katika alipokuwa na mwendazake!!!!!!!!!
Kaa mbali na watu kama hao!!!
 
Wewe hebujaribu kumuona dactari naona kama unamsongo wa mawazo.

Serikali imesema chanjo ni hiyari then kila mmoja anahaki ya kusema kwanini anachanja na kwa nini hachanji sasa mambo ya vyama yanahusika nini hapo.

Mimi mwenyewe ni daktari na hapa nilipo najiona. Ni hivi Polepole aache unafiki afuate kila kitu kama alivyokuwa anafanya kipindi cha yule kiongozi muovu.
 
Ni kweli, ila yeye alikuwa kwenye serikali ya dhalimu ya kutoheshimu hiyari ya watu. Wakati wapinzani wakihamasisha kuwepo kwa chanjo, kutolewa taarifa za ugonjwa, alikuwa akieneza upotoshaji kuwa wapinzani ni mawakala wa mabeberu. Leo hii serikali iliyopo imekubali chanjo anataka iwe hiyari kwenye misimamo!? Toka lini amekuwa muumini wa hiari? Au unafika ndio nguzo yake?
We nae unapiga kelele tu humu, sasa kuna mwanasiasa asiyekuwa mnafki?
 
Tumeona Viongozi mbalimbali wakitumia hiari yao kuhamasisha watu wakachanjwe na wengine wamekua sehemu ya kuchanjwa kama kuonesha mfano.

Polepole Naye yupo na msimamo wake wa kutochanjwa na ameenda mbali akihimiza watu wazingatie vyakula na vilevile kahoji kwanini hii chanjo haioneshi muda sahihi wa kufanya kazi tofauti na chanjo zingine.

Polepole yupo sahihi, ikionesha tayari wakubwa zake ambao ni Rais na mwenyekit wake wanaipigia chapuo chanjo?View attachment 1883817

View attachment 1883818

Hivi waliopururwa na hili gonjwa walikuwa na matatizo ya lishe? Kwamba lile jiwe kumbe halikuwa jiwe?

IMG_20210720_114420_251.jpg

Pana wodi pale mwananyamala SSH alitimua mbio. Anaonaje pole pole akiwa anakwenda hata kuwasalimia salimia wale wagonjwa na kuwapa ndogo ndogo za mambo ya lishe?
 
Mimi mwenyewe ni daktari na hapa nilipo najiona. Ni hivi Polepole aache unafiki afuate kila kitu kama alivyokuwa anafanya kipindi cha yule kiongozi muovu.

Mkuu huyu mburula Liwagu anakushauri kujiona mwenyewe.

Pata kioo mkuu.
 
Huyu anajisahau Sana anajua kwa kusema hachanji ni watu wangapi amewabadilsha msimamo, na anawaka kwenye risk ya Corona? Polepole kama hujachanji Kaa kimnya usiwabadili walio dhaifu
Kama ni hivyo basi isingekuwa hiari hizo chanjo ingekuwa lazima ili kuwaondoa watu kwenye risk ya corona.
 
Kama anaheshimu hiyari asingekuwa sehemu ya ule uchaguzi wa kishenzi chini ya dhalimu, maana watu kuchagua mgombea wa chama fulani ilikuwa ni hiyari yao.
Huo uchaguzi unaolilia utafikiri huko nyuma kulikuwa na uchaguzi wa haki, wengine tulishaacha masuala ya uchaguzi bongo kabla hata ya huo uchaguzi unaouongelea ila mwenzetu sijui huo uchaguzi ndio mara yako ya kwanza kushiriki uchaguzi bongo.
 
Tumeona Viongozi mbalimbali wakitumia hiari yao kuhamasisha watu wakachanjwe na wengine wamekua sehemu ya kuchanjwa kama kuonesha mfano.

Polepole Naye yupo na msimamo wake wa kutochanjwa na ameenda mbali akihimiza watu wazingatie vyakula na vilevile kahoji kwanini hii chanjo haioneshi muda sahihi wa kufanya kazi tofauti na chanjo zingine.

Polepole yupo sahihi, ikionesha tayari wakubwa zake ambao ni Rais na mwenyekit wake wanaipigia chapuo chanjo?View attachment 1883817

View attachment 1883818
Hivi wenye magonjwa makubwa kama kisukari, ngoma wakichanjwa haileti madhara?

Kwani kwa wale wansosafiri kabla ya kuchanjwa homa ya manjano unaulizwa kama una magonjwa hayo ili usichanjwe.
 
Huo uchaguzi unaolilia utafikiri huko nyuma kulikuwa na uchaguzi wa haki, wengine tulishaacha masuala ya uchaguzi bongo kabla hata ya huo uchaguzi unaouongelea ila mwenzetu sijui huo uchaguzi ndio mara yako ya kwanza kushiriki uchaguzi bongo.

Wizi unafahamika, sio ushenzi. Ule haukuwa wizi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Nina uhakika ile 2015 kama Lissu angekuwa na hiari asingekubali kula matapishi yake ila ndio hivyo tena.

Na huo unafiki wao tuliusema wakati ule, na hata sasa tumeendelea kuwaambia kuwa kumpokea Lowassa ilikuwa ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
 
Wizi unafahamika, sio ushenzi. Ule haukuwa wizi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Huo wizi unaofahamika ndio unaofanya ccm iwe madarakani kipindi chote hiki halafu wewe unaona ni kitu kidogo et ni wizi unaofahamika, sasa kama hilo umeweza kulikubali na kuliona dogo sasa hilo kubwa unalolishangaa hapa lipi wakati hata iweje ccm ilikuwa lazima tu iendelee kukaa madarakani kivyovyote vile.
 
Back
Top Bottom