Ni sahihi kuachana na mwanamke uliyemzalisha watoto wawili?

Ni sahihi kuachana na mwanamke uliyemzalisha watoto wawili?

Yaani mwanamke anaondoka kwako na watoto wako toka mwezi uliopita na huangaiki kupiga simu kwa ndugu zake kumjulia hali au kujua alipo serious..

Wewe humpendi huyo mwanamke basi penda watoto wako.

Kwanza fanya juhudi kujua alipo wapi nenda kawasalimie watoto na upeleke mahitaji siku hizi maisha magumu usiwaachie majukumu yako wakwe zako..

Kama unampenda bado omba msamaha huko warudi nyumbani muendelee na maisha kama himpendi kwa sasa basi fuata utaratibu mzuri wa kujua namna ya kutunza watoto wako.
Msamaha niliomba akasema kanisamehe,ila hayuko tayari kuendelea kuishi hapa nyumbani kwangu,anataka akapumzike kwanza
 
Ninaamini ikipatikana nafasi ya mkeo kusema aliyokuwa anayavumilia toka kwako naamini ni mengi mno pia..!!

katika viumbe wavumilivu ni wanawake, tena hata habari za uchepuzi hana maskiini dada wa watu, vuta kidosho nyingine uje kutuomba ushauri wa kuruka ruka kwake kama popcorn tukushauri tena..!!

Waonee huruma wanao, wanaenda kuishi maisha ya aina gani bila Baba yao, hata kama Mama yao angekuwa na kazi ya kueleweka ila bado 'Presence' ya Baba na malezi yako ni muhimu mno kwenye mustakabali mzima wa maisha yao..!!

Sidhani kama kuna kitu kinashindwa kuzungumzika na 'kusolvika' baina yako wewe na mwenzio, wanaokushauri wengi humu na wenyewe wana changamoto zao nyingi kuliko hata zako, hivyo mtu isipomfaa akili yake basi utamdhuru ujinga wake..!!
 
Rudianeni mkuu , huyo ni shetani kapita kwa ninavyoona bado unampenda !!
Mbona umewaza kuachana kabla ya kitu chochote ?
Ugomvi ukitokea kila mtu anapokua ana hasira huwa ana maamuzi magumu ambayo hashirikishi ubongo wake vizuri kwa hiyo yeye kuondoka ni hasira lakini bado mnahitajiana.
Muite omba msamaha kwa sababu huenda wewe ndo una kosa maana ulikua katika hali ya ulevi naamini atakuelewa wanawake kidogo wana moyo wa kusamehe ! Mpeti peti muulize hiyo hali ya kununa inasababishwa na nini ? Ataeleza kama liko ndani ya uwezo wako litatue mapema !
Kuoa mke mwingine ni kujiongezea tu mzigo wa watoto pia uanze kujenga tena tabia zake maana hakuna uhakika kama utampata mwenye tabia njema kuliko mkeo wa mwanzo !! Kila mtu ana vipengele vyake 😂

Rudisha mamaa nyumbani mzee !! Tatueni itakusaidia wewe , pamoja na saikolojia ya watoto !!
 
Mnapiga kama mnapiga ngoma eeeh ?
Mwanaume wa kupiga hafai, siku atakutia ulemavu
 
Ninamini ikipatikana nafasi ya mkeo kusema aliyokuwa anayavumilia toka kwako naamini ni mengi mno pia..!!

katika viumbe wavumilivu ni wanawake, tena hata habari za uchepuzi hana maskiini dada wa watu, vuta kidosho nyingine uje kutuomba ushauri wa kuruka ruka kwake kama popcorn tukushauri tena..!!

Waonee huruma wanao, wanaenda kuishi maisha ya aina gani bila Baba yao, hata kama Mama yao angekuwa na kazi ya kueleweka ila bado 'Presence' ya Baba na malezi yako ni muhimu mno kwenye mustakabali mzima wa maisha yao..!!

Sidhani kama kuna kitu kinashindwa kuzungumzika na 'kusolvika' baina yako wewe na mwenzio, wanaokushauri wengi humu na wenyewe wana changamoto zao nyingi kuliko hata zako, hivyo mtu isipomfaa akili yake basi utamdhuru ujinga wake..!!
Sawa mkuu,nimekupata vyema kabisa
 
Mkuu,
Nenda uchukue mke wako!
Kumshushia mke kipondo kwa sababu eti ulikuwa tungi hiyo haikubaliki.....kubali umekosa na uombe radhi.
Kama umeshakaa na mwanamke miaka zaidi ya 5 na mmepata watoto 2 huyo ni mke tayari....na umesema hujawahi kuhisi usaliti wowote hiyo inampa thamani zaidi huyo mwanamke.
 
Habari zenu wakuu?
Kwa wale wakatoliki poleni sana kwa msiba wa papa Francis.
Issue yangu iko hivi,kuna mwanamke nilikua naishi nae,huu ni mwaka wa 7 au 8 kama sikosei,tumebahatika kupata watoto wawili.hatuna ndoa but nilitaka mwaka huu tubariki.
Huyu mwanamke kwa suala la uaminifu sina shaka nae kabisa,kwani sijawahi kumhisi kwa lolote baya.
Sasa mwaka huu haujaanza vizuri kwa upande wetu,tumekua nin watu wa kununiana sana kwa mambo madogo madogo tu.
Sasa last month kuna siku nimerudi home niko tungi,sijui alinisemesha kitu gani kwa kweli nilimkungu'uta sio poa,usiku huo huo akakimbilia kwa ndugu zake,kesho yake akarudi nyumbani na kirikuu akachukua kila kilicho chake akasepa kwao kukaa pamoja na watoto .
Nilimsihi sana asiondoke ila akasema amechoka na maisha tunayoishi na kanivumilia sana.
Basi akaondoka na watoto,so huko aliko sijui wanakula nini wala sijui kama wanaenda shule yani niko sina taarifa zao,hakuna ndugu yake hata mmoja aliyenipigia kuniuliza imekuaje binti yao karudi nyumbani mpaka leo.
So mimi wasiwasi wangu ni hao watoto sijui kama wanapata huduma sahihi kwani mama yao hana kazi ya kueleweka.
Sasa wakuu,tusaidiane mawazo,ntakua sahihi kumuacha huyu mwanamke ambae tayari nimemzalisha watoto wawili?if not,nitumie mbinu gani kuyajenga nae ili arudi nyumbani?
Note:sikua tayari kuzaa na wanawake tofauti na huyu katka maisha yangu,but kwa scenario hii naona kuna dalili nikatafuta kidosho mwingine tukazaa tena.
Naomba maoni yenu yenye busara hapa,matusi pia yanakaribishwa kwa mikono miwili.
LEA WATOTO WAKO.
 
Mkuu,
Nenda uchukue mke wako!
Kumshushia mke kipondo kwa sababu eti ulikuwa tungi hiyo haikubaliki.....kubali umekosa na uombe radhi.
Kama umeshakaa na mwanamke miaka zaidi ya 5 na mmepata watoto 2 huyo ni mke tayari....na umesema hujawahi kuhisi usaliti wowote hiyo inampa thamani zaidi huyo mwanamke.
Sawa mkuu,nimekupata vizuri
 
Achana na pombe, huziwezi, kupiga mwanamke ni kutojiamini.

Na kama umemchoka mkeo tafuta namna muachane kwa amani, wewe ubaki kulea wanao akiwa mbali.
 
Rudianeni mkuu , huyo ni shetani kapita kwa ninavyoona bado unampenda !!
Mbona umewaza kuachana kabla ya kitu chochote ?
Ugomvi ukitokea kila mtu anapokua ana hasira huwa ana maamuzi magumu ambayo hashirikishi ubongo wake vizuri kwa hiyo yeye kuondoka ni hasira lakini bado mnahitajiana.
Muite omba msamaha kwa sababu huenda wewe ndo una kosa maana ulikua katika hali ya ulevi naamini atakuelewa wanawake kidogo wana moyo wa kusamehe ! Mpeti peti muulize hiyo hali ya kununa inasababishwa na nini ? Ataeleza kama liko ndani ya uwezo wako litatue mapema !
Kuoa mke mwingine ni kujiongezea tu mzigo wa watoto pia uanze kujenga tena tabia zake maana hakuna uhakika kama utampata mwenye tabia njema kuliko mkeo wa mwanzo !! Kila mtu ana vipengele vyake 😂

Rudisha mamaa nyumbani mzee !! Tatueni itakusaidia wewe , pamoja na saikolojia ya watoto !!
Sawa mkuu umesomeka vyema
 
Sema neno boss
Naomba jipe muda mtafute mkeo jishushe omba msamaha kuwa hautampiga tena na pia chukua wanao na mkeo mkaendelew na maisha .
Acha mara moja kuwaza upumbavu eti kugombana mara moja muachane wewe unayajua maisha ya kumuacha mwanamke mwenye watoto wako ? Usijaribu mdogo wangu naomba kayamalize na mkeo wanao wanakuhitaji wewe na mkeo .

Akigoma nitaomba uniamini nipe walau hata simu ya mzazi wa kiume wa mkeo nitakuwa tayari kumrudisha kwa gharama zangu .

Kauchana ni vibaya ,ni donda dumu ,ni mwanzo wa maisha ya ujinga na utahir hasa ngono zisizo na staha naongea haya kama muathirika wa haya unayojaribu kuyaonja kwa ulimi .

Nikuombe unielewe tu ,wewe ni mnywaji na yawezekana ni mlevi mwenzangu ila kwa hili hapana usifike huko bado unahitaji kuijenga familia yako
 
Back
Top Bottom