Ni sahihi kuachana na mwanamke uliyemzalisha watoto wawili?

Naomba jipe muda mtafute mkeo jishushe omba msamaha kuwa hautampiga tena na pia chukua wanao na mkeo mkaendelew na maisha .
Acha mara moja kuwaza upumbavu eti kugombana mara moja muachane wewe unayajua maisha ya kumuacha mwanamke mwenye watoto wako ? Usijaribu mdogo wangu naomba kayamalize na mkeo wanao wanakuhitaji wewe na mkeo .

Akigoma nitaomba uniamini nipe walau hata simu ya mzazi wa kiume wa mkeo nitakuwa tayari kumrudisha kwa gharama zangu .

Kauchana ni vibaya ,ni donda dumu ,ni mwanzo wa maisha ya ujinga na utahir hasa ngono zisizo na staha naongea haya kama muathirika wa haya unayojaribu kuyaonja kwa ulimi .

Nikuombe unielewe tu ,wewe ni mnywaji na yawezekana ni mlevi mwenzangu ila kwa hili hapana usifike huko bado unahitaji kuijenga familia yako
Sawa sawa mkuu,ushauri wako nimeuchukua
 
Mzee chanzo cha ujaribifu wa watoto uchangiwa na ujinga wa wazazi.

Usione kizazi kibovu kilichopo sasa ni Matokeo ya wazazi kutojitambua na kujua Wana wajibika kulea na kutengeneza watoto watakao kua baba na mama Bora.

Mkeo ni Mtu muhumu sana katika maisha yako brother.

Ukiona mwanamke Ana kurekebisha kwenye jambo Lolote jua Anakupenda na kukutakia Mema.

Mimi Niko kwenye ndoa zaidi ya Miaka 30 Nina uzoefu mkubwa juu ya Mke.

Ukitaka kupotea jufanye wewe unajua kila kitu Alafu Mdharau mkewako. Muda utaongea utaharibukiwa kila kitu.

Mimi Nakushauri Mtafute mkewako myatengeneze na ukubali Kushauriwa Brother na mkewako.

Wewe ni Mtu mzima ni lazima uwe mtu wa kutafakari mambo na kuamua kwa busara brother.

Matatizo Au changamoto haziondolewi kwa kulewa ndio unajipoteza kabisa.

Changamoto uondolewa kwa kutafakari na Kushauriana na mkewako.
 
Huyo tayari ni mke wako, ondoa kauli kuwa hamjafunga ndoa. Ndoa tayari hiyo hata kama hangekuzalia. Kurudi anaweza kurudi kama atapigwa na maisha vibaya ila akipata ka ajira ka kumpa kula na watoto wake, imetoka hiyo, ikirudi ina pancha, we nawe itabidi ujitafutie single mama uvute kama hutanasa kwa mishangazi. Kumchukulia poa huyo mkeo itakugharimu sana kama hatarudi
 
Ninamini ikipatikana nafasi ya mkeo kusema aliyokuwa anayavumilia toka kwako naamini ni mengi mno pia..!!

katika viumbe wavumilivu ni wanawake, tena hata habari za uchepuzi hana maskiini dada wa watu, vuta kidosho nyingine uje kutuomba ushauri wa kuruka ruka kwake kama popcorn tukushauri tena..!!

Waonee huruma wanao, wanaenda kuishi maisha ya aina gani bila Baba yao, hata kama Mama yao angekuwa na kazi ya kueleweka ila bado 'Presence' ya Baba na malezi yako ni muhimu mno kwenye mustakabali mzima wa maisha yao..!!

Sidhani kama kuna kitu kinashindwa kuzungumzika na 'kusolvika' baina yako wewe na mwenzio, wanaokushauri wengi humu na wenyewe wana changamoto zao nyingi kuliko hata zako, hivyo mtu isipomfaa akili yake basi utamdhuru ujinga wake..!!
Dada Carol mwanamke hawez kuondoka kwako bila plan b

I mean lazima kuna muhuni uko ktaan amemchanganya

Sasa ni bora mwanamke awe na tabia zingine ila sio kutmbewa 😎
 
Sawa mkuu,umesomeka
Ikiwa ni kuomba msamaha, inakubidi,

Kingine usiamini kuwa pombe ndo mtatuzi wa shida zako, siwezi kukuambia acha pombe, Ila pombe sio dawa ya matatizo yako,

Fuatilia wanao walipo, ona uwezekano wa kutoa sapoti

Ikiwa mke kakaza ni muda tuu atarejea kama Hana mtu anayempa kiburi huko nje,

Muda wa mapumziko anayosema binafsi isizid miezi mitatu ikipita hapo
 
Mzee chanzo cha ujaribifu wa watoto uchangiwa na ujinga wa wazazi.

Usione kizazi kibovu kilichopo sasa ni Matokeo ya wazazi kutojitambua na kujua Wana wajibika kulea na kutengeneza watoto watakao kua baba na mama Bora.

Mkeo ni Mtu muhumu sana katika maisha yako brother.

Ukiona mwanamke Ana kurekebisha kwenye jambo Lolote jua Anakupenda na kukutakia Mema.

Mimi Niko kwenye ndoa zaidi ya Miaka 30 Nina uzoefu mkubwa juu ya Mke.

Ukitaka kupotea jufanye wewe unajua kila kitu Alafu Mdharau mkewako. Muda utaongea utaharibukiwa kila kitu.

Mimi Nakushauri Mtafute mkewako myatengeneze na ukubali Kushauriwa Brother na mkewako.

Wewe ni Mtu mzima ni lazima uwe mtu wa kutafakari mambo na kuamua kwa busara brother.

Matatizo Au changamoto haziondolewi kwa kulewa ndio unajipoteza kabisa.

Changamoto uondolewa kwa kutafakari na Kushauriana na mkewako.
Sawa sawa mkuu,this is well noted
 
Huyo tayari ni mke wako, ondoa kauli kuwa hamjafunga ndoa. Ndoa tayari hiyo hata kama hangekuzalia. Kurudi anaweza kurudi kama atapigwa na maisha vibaya ila akipata ka ajira ka kumpa kula na watoto wake, imetoka hiyo, ikirudi ina pancha, we nawe itabidi ujitafutie single mama uvute kama hutanasa kwa mishangazi. Kumchukulia poa huyo mkeo itakugharimu sana kama hatarudi
Sawa mkuu
 
Miaka saba huyo ni mkeo.Jishushe chini na kumuomba msamaha kwa kumchapa.Halalisha ndoa mlee watoto pamoja.Baada ya kazi fika nyumbani acha kuzurura wanawake hudhani umetoka kufanya kamanyola
 
Ikiwa ni kuomba msamaha, inakubidi,

Kingine usiamini kuwa pombe ndo mtatuzi wa shida zako, siwezi kukuambia acha pombe, Ila pombe sio dawa ya matatizo yako,

Fuatilia wanao walipo, ona uwezekano wa kutoa sapoti

Ikiwa mke kakaza ni muda tuu atarejea kama Hana mtu anayempa kiburi huko nje,

Muda wa mapumziko anayosema binafsi isizid miezi mitatu ikipita hapo
Poa poa mkuu
 
Fahamu kuwa kuna masela huwa hawajali idadi ya watoto aliyonayo mwanamke wanabeba na watoto wake. Uko tayari kuona au kusikia watoto wako wanalelewa kwa msela mwingine? Ukute tayari mkeo kajazwa mimba na huyo msela aliyembeba
 
Yote heri tu mkuu
 
Kikubwa nakusaidia kutunza Mzee mwenzangu sema ka nyau kake kadogo sana like hajawai zaa😂
 
Back
Top Bottom