Ni sahihi kulea mtoto wa Kambo?

Sioni kama kuna shida,vitu vingi, wanaume ambsvyo wanaona ni matatizo, husababishwa na ukosefu wa pesa, ukiwa na fedha, hata kusomesha watoto kumi wa kambo sio tatizo, laiti ungeuliza je ni sawa kugawanya mkate wa watoto wangu wa damu na kumpa wa kambo? Au nitoe mtoto wangu English medium, nimpeleke kayumba, ili nibaki na mkwanja nisomeshe mtoto wa kambo, hiyo sio sawa kabisa,
 
Mtoto wa kambo nimtoto wako kwasababu nimtoto wa mkeo

Na iwapo utashindwa kumlea Kama mwanao Basi mlee Kama mtanzania mwenzio au mwafrica mwenzio
 
Unapenda boga pekeeua unamuachia nani
 
Uzi umeishia hapa
 
Atamkuta akiwa na watoto wengine wa3, kuna ubaya gani na mitoto mibichi imejaa kibao? Kung'ang'ania mwanamke ni tatizo la saikolojia.
Lakini tayari ushapoteza muda na pesa kulea mtoto asiye wako
 
Mkuu umeeleza kwa ufasaha sana, na akimesap hapo familia itaparanganyika, na alifanya kosa sana mwamba kuuoa singo mama
 
Kwani ni mwanao
Kama uwezo upo, na nina ufahamu sio kwamba nimebambikiwa, nikimlea asiyetoka kwenye viuno vyangu kuna tatizo gani?
mabinti wabichi wamejaa wewe unahangaika
Kila nikiwasoma hoja zenu zinaangukia sehemu moja tu, hofu ya kugongewa ambayo kwangu mm haina mashiko. Malaya atagongwa tu hata kama ulimchukua bikira. Asiye malaya atatunza heshima yake hata kama alishaichafua kabla.
 
Kuna mazingira ukimtazama baba mzazi unaona kabisa hana madhara.

Mfano Mtu anashinda kwenye baa za pombe kali za kienyeji kalewa chaka chaka 24/7 kachoka mara aokotwe mitaroni una hofu nae wa nini na mzazi mwenzie umempa watoto na maisha mazuri?
Nimemis madini kama haya kwenye ule Uzi wetu.., respect πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Jadiliana na mkeo! Soon atakuzalia mwingine na huyo ex wake!
 
1. Kama NI Mtoto WA Kike mchukue umlee hata Leo hii. Hapa Hakuna masharti

2. Kama NI Mtoto WA kiume Hapo wekeni makubaliano kadiri utakavyoona.

3. Kama Mkeo anakazi ya kuzalisha kipato Lea.

4. Kama Mkeo anakutii Lea.

Lakini napata shida kuhusu kuvunjwa Kwa makubaliano Yenu tangu mwanzo.

Kama Mtoto anasema anateseka, ustawi WA jamii upo
 
Mpaka uwe na roho nzuri au ni Mchamungu! Kama wewe una roho nzuri au ni Mchamungu unaweza kumlea ili mradi baba yake awe analeta matunzo!
Lakini kama una roho mbaya,toa pesa ya matunzo ya mtoto tu lakini usioe!

Mungu mwenyewe mwenye Roho nzuri atawachoma Watoto wa Kambo(Watoto WA Shetani)

Mnapenda kumpa Sifa Ambazo Hana.

Mungu NI nature.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…