Ni sahihi Rais Traore kukutana na maraisi huko Russia akiwa na bastola kibindoni?

Ungetuwekea ushahidi wa haya unayoyaandika ingekuwa bora zaidi.
Mkuu kama hukubaliani na nilichoandika ni kazi yako kupinga kwa kuonyesha ushahidi, sio kazi yangu kujiwekea ushahidi mwenyewe kwa sababu sijipingi.
 
Hana lolote huyo dogo. Umaarufu wake ni zao la social media tu.

Habari nyingi sana kumhusu yeye ni za uongo uongo au zilizotiwa chumvi nyingi.

Tuliambiwa eti alikataa mwaliko wa Trump kuhudhuria uapisho wake 🀣. Na watu wakaamini tu bila kujua kwamba hilo ni rahisi sana kulithibitisha.

Sasa hivi kwenye mitandao kuna videos zikimwonyesha akiongea Kiingereza.

Sina uhakika sana kama ni yeye. Nadhani ni video za kutengenezwa.

Sidhani kama yuko fluent kivile kwenye Kiingereza.

Kawachota akili wajinga na wapumbavu ambao wanaamini kila kitu kuhusu yeye.

Ana cult following ya wajinga, wapumbavu, na majuha.

Anazunguka na hicho kibastola chake huku kavaa magwanda utadhani ni mlinzi wa getini.

Naye watampindua tu kwa staili ile ile aliyoingia nayo madarakani.

Hizi zama zama social media zina wajinga na wapumbavu wengi sana.

Wao wakiona kitu chochote tu mtandaoni, basi wanakiamini mazima.

He is a hype job!
 
Hahaaa

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo hata tukikwambia siyo sahihi itakusaidia nini? We endelea kukamua mawese huko kazuramimba
 
Hiki kiswahili kimekaa Kama AI generated πŸ˜€
 
Wenyeji wake wanasemaje?
 
Self diffenceπŸͺ
 
Yeye Iko wazi inaonekana, ila zipo njemba ambazo nchi zao ziko na falsafa kama za Russia chuma ziko ndani ya Makoti tena double double Hadi magotini hahh
 
Kama mataifa ya Afrika yakijielewa siku moja, labda tunaweza kufika mahali
Huyu ni mmoja katika nchi zaidi ya 50.
Mjitafakari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…