Ni sawa kuweka nyimbo za injili kwenye mabasi ya mikoani?

muziki unafariji, unaponya mjuba, hili nalo hujui faida za muziki? Ishu ya maudhui ni kitu kingine
 
Ipi ivi yale ni matakwa ya dereva na konda wake kutokana na moods zinazomzunguka na mara chache sana kua matakwa ya mtu binafsi mf mm mara myingi nimepanda mabas ya abood kwenye tv kukaoneshwa nyimbo za injiri,bolingo,kaswida na hata movies zisizokua na maadili,pia mara nyingi ata mabas ya wakristo kama bm,esta huweka kaswida kwa uchache na hata movies ambazo wengine atupendi
 
Ni kweli kama tungekuwa jamii tunayojitambua vizuri na kujiweza kiuchumi safarini ingekuwa sehemu ya kusoma vitabu na kujifanyia mambo mengine ila usafiri wa bus Tanzania ni mgumu sana usio comfortable kuweza kufanya mambo ya maana kwa hiyo TVs zinapunguza tabu kidogo.
 
muziki unafariji, unaponya mjuba, hili nalo hujui faida za muziki? Ishu ya maudhui ni kitu kingine
Kuna watu hawaruhusiwi kusikiliza muziki kimatibabu kabisa , na wengine hawapendi mziki wa aina yoyote
 
Kuna sheria inakataza? Asubuhi wanaomba kabla ya safari, mbona hutoki nje. Mimi Azana za kuniamsha kila siku wakati si dini yangu wakati si dini yangu ndo kero. Yule shehe wa Azana anajua nimelala saa ngapi? Hizi dini zataka kuvumiliana kuvumiliana, vinginevyo wakisema tusisikilize ambavyo hatutaki kusikia hapatakalika.
 
"Hiyo ndio Tanzania" hapo unakuta walikuwekea mabongo flavour na mamovie yenye mambo ya hovyo hovyo huku ndani ya bus kukiwa na watoto. Mimi Mkristo ninae jitambua nitavumilia mahubiri ya kiislamu ndani ya bus kuliko mabongo flavour na ma movie maana mengi yanakuwa ya hovyo,kuna siku wakati wanabadili nyimbo waliwahi kweka video ya ngono,mpaka kuitoa watu wote ndani ya basi walikuwa wameona. Kama huweki nyimbo za kikristo au kiislamu basi ni bora kupiga kimya tu
 
Waweke haina shida ,kwani tatizo liko wapi...Mimi hata movie siwezi kufuatilia hizi za kwenye mabasi ..Njimbo hizo hazina tatizo ,mbona hata zile za wakaa uchi wanapigan.
 
Mimi nikikutana na comedy has za mkojani, ndaro na Stivu mweusi pamoja na bongo movies safari tayari imeharibika.
Hawa bado sijawajua mkuu ,nawajua matujo , kingwendu bambo joti na mpoki😁
 
Nadhani huwa hawajui kuwa zile TV ni kwa ajili ya abiria na sio wao makonda na madereva..

Lakini pia sometimes kwa safari ndefu. Kheri waweke tu hizo destructions japo sauti wakicontrol itakuwa sawa zaidi kwa watu wasio interested..
Distraction sio Destruction
 
Kiufupi wewe ukipanda bus mshukuru mungu umefika salama bin salmin maana ndio lengo kukuu kwa 100% na kuhusu huduma zitolewazo kwenye usafiri haziwez kuwafurahisha abilia wote 60 kwa utofauti wenu wa kiiman,kitikadi ata kimaumbie na mbaya zaidi akuna bus ata v.i.p apa afrika lenye uwezo wa kumkonga moyo kila abilia kutokana na utofauti wa iman,itikad na maumbile
 
Bimafsi nadhani ni heri kusikiliza muziki wa injili kuliko zile nyimbo ambazo zimejaa matusi! Au labda kuna madhara yoyote au kadhia ulikumbana nayo kutokana na hilo!?
 
Balance story yako kwani kuna mengine yanaweka kaswida.
 
Kwani ukisikia wimbo wa injili unapata shida gani
 
Hayo nafikiri ni maamuzi binafsi ya mwenye usafiri kama unaona ni kero kwako unaweza kutafuta usafiri utakaokuwa na maudhui uyapendayo
Sasa mtu atajuaje hili bus lina maudhui fulani ndani yake ilhali ni mpaka lianze safari ndiyo wanaweka!!

Waweke angalizo huko kwenye tovuti zao kwamba wao ni kwaya safari nzima au ni kaswida!!
 
Ni mziki gan tunaweza kujali ili tukipiga kila mtu afurahie ndani ya gari?
Kupiga miziki kwenye gari ni kupigiana kelele na kero kwa wengine.
Mle kwenye gari kuna watu ambao afya zao hazina urafiki na makelele lakini utakuta watu wameweka mamiziki tena kwa sauti ya juu.

Suruhisho ni kutoliza mziki wowote kwenye gari za uma kama mtu anataka kusikiliza mziki atumie simu yake kusikiliza mziki anao utaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…