Mwarabu na elimu wapi na wapi, ukikariri kile kitabu chao umeelimika tosha.
MK254,
Ninachokiona hapa ni uchache wa elimu.
Uislam umeingia Pwani ya Afrika ya Mashariki zaidi ya miaka 1000 iliyopita.
Uislam uliingiza katika pwani hii zile zinaitwa 3Rs yaani ''Reading,'' ''Writing,'' na ''Arithmetic.''
Waislam wakawa watu wa kwanza kujua kusoma, kuandika na kufanya hesabu na kote katika nchi hizi za Pwani ya Afrika ya Mashariki elimu hii ikitolewa kwa maandishi ya Kiarabu.
Mmeshionari Johann Krapf alipofika Vuga kwa Chief Kimweri alistaajabu sana kumkuta Kimweri na watoto wake wote hadi wa kike wakijua kusoma, kuandika na kuhesabu.
Chanzo cha elimu hii yote ilikuwa madras.
Krapf alidhani Afrika ni ''Bara la Kiza,'' lakini akastaajabu kuwakuta watu Usambaani wamestaarabika na ni Waislam.
Hii ilitia choyo na hasad katika nyoyo zao.
Wajerumani walipofika Afrika ya Mashariki baada ya Berlin Conference na kuanza kutawala waliwaajiri Waislam katika serikali yao kwa kuwa walikuwa wameelimika.
Walipoondoka Wajerumani na kuingia Waingereza wao wakapiga marufuku matumizi ya hati za Kiarabu.
Ikawa sasa mtu aliyekuwa anajua kusoma na kuandika kwa sheria hiyo ya kikoloni ghafla akawa mtu aiyejua kusoma na kuandika.
Ujenzi wa shule kuchukua nafasi ya madras ukaanza na elimu ikiwa mikononi mwa Wamishionari na serikali na ikiwa mtoto anataka kuingizwa shule kusoma ilibidi abatizwe awe Mkristo.
Hiki kikawa kikwazo kikubwa kwa Waislam kupata elimu.
Hassan Omar Makunganya shujaa aliyepigana na Wajerumani na wakamnyonga Kilwa ameacha hazina kubwa ya maandishi aliyokuwa akiandika kwa hati za Kiarabu wakati wa harakati dhidi ya utawala wa Kiarabu.
Nyaraka hizi zipo Zentrum Moderner Orient, Berlin.
Halikadhalika Mtwa Abdallah Mkwawa wa Uhehe ameacha barua zake alizokuwa akiandika kwa hati za Kiarabu.
Barua hizi zipo Mkwawa Museum Kalenga.
Babu yangu Sheikh Muhammad Mvamila alikuwa akiandika siku zote kwa herufu za Kiarabu hadi anakufa.
Ndugu zangu ikiwa tutaacha mihemko na kejeli hapa tunaweza tukafanya mijadala ya manufaa kwa jamii yetu na tukaelimishana mengi.
Umeitaja Qur'an kwa dharua ''kitabu chao'' lakini umegusa kitu kimoja cha maana sana nacho ni ''hifdh'' yaani kuihifadhi.
Kuhifadhi Qur'an ni moja ya vipimo vya uwezo wa akili ya mtu.
Si uungwana kukashifu dini ya mwenzio.
Siamini kama Bwana Yesu haya ndiyo mafunzo yake.
Moja ya barua ya Mtwa Mkwawa katika Mkwawa Museum