kweyamba_dave
JF-Expert Member
- Oct 2, 2012
- 961
- 483
Mkuu, ikiwa lengo la uzi ni kujifunza basi nikujulishe tu kuwa zipo shule kadhaa zilizojengwa na muarabu tena si serikali bali mtu ama watu binafsi.Habari wadau.
Nasikia baada ya kupata uhuru mwaka 1961 Serikali ilitaifisha shule zilizojengwa na wakoloni
Mfano shule zilizojengwa na wakoloni wazungu kama Minaki, Ilboru, Pugu, Mazengo, forodhani, etc
Je ni shule zipi zilitaifishwa ambazo zilijengwa na wakoloni waarabu?
Maana waarabu walitangulia kuja Tanganyika na Zanzibar kwa kwa miaka zaidi ya 500 kabla wakoloni wazungu hawajaja.
Zanzibar pia waarabu walifika mapema sana maana msikiti wa Kazimkazi ulijengwa mwaka 1006 AD, waarabu walitawala kwa miaka mingi Zanzibar na walifika mapema sana, naomba mnitajie ni shule gani ya sekondari waarabu walijenga Zanzibar, na ilijengwa mwaka gani?
Tofauti na wazungu muarabu hakuwahi kuwa mtawala wa Tanganyika bali visiwani na baadhi ya sehemu ya bara ambayo ilikuwa kama strip ili afanye biashara zake na aweze kusafiri bila bughuza.
Mwaka 1882 Sewa Haji Paroo aligawa jengo la ghorofa tatu kuwa shule ya kwanza ya watu mchanganyiko Tanganyika. Shule hii ipo hata sasa ninavyoandika kwenye tarafa ya mwambao kata ya Dunda Bagamoyo. I grew up next to the school na I can say nimeona legacy ya mwarabu.
Binafsi ni muhusudu wazungu kweli na nimepita na kusoma kwenye shule za wazungu lakini nikiri sijaona mzungu mwenye roho ya utu kama aliyokuwa nayo Sewa Haji Paroo. Nimepita Ilboru naifahamu historia ya shule tangu ikiwa Lushoto mpaka kuhamia Arusha na kutaifishwa. Unlike Mwambao ambayo iliruhusu mtu wa dini na rangi yeyote kupata elimu you cant Say the same kwa shule nyingi za wazungu.
Kwenye swali lako umeuliza kwanini hakuna shule iliyotaifishwa ni kwasababu waarabu waliamini kwenye sadaka na hawakuhodhi shule yeyote kama mali yao.
Mwisho sijapata kuona uzi ulioanzishwa kwa minajili ya chuki kama huu.