Ni shule gani ya sekondari ilijengwa na wakoloni Waarabu halafu Serikali ikaitaifisha baada ya uhuru 1961?

Ni shule gani ya sekondari ilijengwa na wakoloni Waarabu halafu Serikali ikaitaifisha baada ya uhuru 1961?

Hiyo elimu uliyo/ mliyonayo haina faida kwa taifa
Nenda Oman,dubai,Qatar kuwait jibu utalipata
Ulienda shule kufanya nini kama haina faida? Hao hao wa Oman wamejaa kwenue vyuo vya UK na America wanaenda kuitafuta hiyo elimu ambayo wew mvaa kobaz wa Msanga unasema haina faida
 
Mwandishi atakua ana semea madrasa

Kuna ki madrasa cha chumba kimoja kilijenga na waarabu serikari ime kigeuza choo saivi pale mwanza

Nakaribisha wenye stress mnijibu
 
Waarabu walitawala mwaka gani? wale ni wafanyabiashara walikuwa na trade routes zao walipopita ndo waliacha tamaduni zao...
Zanzibar ilikuwa ndiyo Dola kuu hadi ndani ya Afrika ya Mashariki.Zanzibar ikawa chini y waarabu qa Oman kuanzia 1698 hadi anachukua madaraka Seyyid Bin Said Al sultan Bhusaid mwaka 1804.Hapo kabla 1741 familia ya Mazalia au Mazrui pale Mombasa ilijitangazia uhuru lakini baadaye ilipigwa na kurejeshwa chini ya Oman.1840 sultan anahamia Zanzibar,maeneo karibu yote ya yalitawaliwa na watawala watiifu kwa sultan wa Zanzibar.
 
Mwarabu na shule wapi na wapi?

Yeye anakitabu chake kimoja ukishakikariri tayari kimekamilika na itakuwa umeeleea hesabu zote kuanzia hisabati, mathematics, additional mathematics, basic applied mathematics,pure mathematics, physic,chemistry, biology , finance, law , engineering nk. Hawahitaji madrasa ya kawaida Wala viti vya kukaa
Mohamed Said jibu hili ili tuone kama Sykes wako alijenga shule au la!
Kolola...
Ikiwa ndugu yangu nia yako ni kufanya ugomvi na kuwakejeli wazee wangu mimi nitaacha mjadala na wewe.

Mimi naeleza historia ya wazee wangu vipi walivyoanza harakati mwaka wa 1929 hadi kufikia Tanganyika kupata uhuru wake mwaka wa 1961.

Kitabu kipo na kinasomwa sasa mwaka wa 25.
Sasa hii fedhuli ya nini ndugu yangu?

Naam Kleist Sykes na wenzake kama Mzee bin Sudi, Ali Jumbe Kiro na wengineo akiwemo babu yangu Salum Abdallah wakiwa ndani ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) walijenga shule mwaka wa 1933.

Majengo ya shule hii yapo Mtaa wa Max Mbwana na Lumumba Avenue.

Baba yangu alisoma shule hii Al Jamiatul Islamiyya Muslim School darasa moja na Abdul Sykes.

1672978872516.jpeg
 
View attachment 2470488
Matango Pori yako na Sykes wako yanazidi mipaka. Unadhani hatumjui sie
 
Shule ijengwe na colonial rulers halafu iwe owned na African chief daughters!!?..inaingia akilini,boys imeanza 1922,miaka minne baada ya world war 1 chapu mwingereza ajenge shule ndani magharibi mwa east Africa asijenge pwani!?
Mbona historia hiyo haijasema ilikua owned na African chief daughters? Nilivyoelewa mimi hiyo shule ilijengwa kwaajili ya kusoma watoto wa kike wa machief na baadae watoto wote wakike wakawa wanaruhusiwa kusoma.
 
Zanzibar ilikuwa ndiyo Dola kuu hadi ndani ya Afrika ya Mashariki.Zanzibar ikawa chini y waarabu qa Oman kuanzia 1698 hadi anachukua madaraka Seyyid Bin Said Al sultan Bhusaid mwaka 1804.Hapo kabla 1741 familia ya Mazalia au Mazrui pale Mombasa ilijitangazia uhuru lakini baadaye ilipigwa na kurejeshwa chini ya Oman.1840 sultan anahamia Zanzibar,maeneo karibu yote ya yalitawaliwa na watawala watiifu kwa sultan wa Zanzibar.
Asante
 
Tanganyika ilipata uhuru wake mwaka 1961 toka kwa mkoloni Muingereza

Zanzibar ilipata uhuru wake mwaka 1963 toka kwa mkoloni Muingereza na baadae yakafanyika Mapinduzi 'matukufu' mwaka 1964.

Mleta mada, huko shule ulienda kusomea ujinga..?!

Hakuna historia ya mkoloni mwarabu nchi hii!
 
Hadi leo ukipita njia ya kibiti Misikiti ni mingi kuliko shule
 
Mwarabu na elimu wapi na wapi, ukikariri kile kitabu chao umeelimika tosha.
MK254,
Ninachokiona hapa ni uchache wa elimu.
Uislam umeingia Pwani ya Afrika ya Mashariki zaidi ya miaka 1000 iliyopita.

Uislam uliingiza katika pwani hii zile zinaitwa 3Rs yaani ''Reading,'' ''Writing,'' na ''Arithmetic.''

Waislam wakawa watu wa kwanza kujua kusoma, kuandika na kufanya hesabu na kote katika nchi hizi za Pwani ya Afrika ya Mashariki elimu hii ikitolewa kwa maandishi ya Kiarabu.

Mmeshionari Johann Krapf alipofika Vuga kwa Chief Kimweri alistaajabu sana kumkuta Kimweri na watoto wake wote hadi wa kike wakijua kusoma, kuandika na kuhesabu.

Chanzo cha elimu hii yote ilikuwa madras.

Krapf alidhani Afrika ni ''Bara la Kiza,'' lakini akastaajabu kuwakuta watu Usambaani wamestaarabika na ni Waislam.

Hii ilitia choyo na hasad katika nyoyo zao.

Wajerumani walipofika Afrika ya Mashariki baada ya Berlin Conference na kuanza kutawala waliwaajiri Waislam katika serikali yao kwa kuwa walikuwa wameelimika.

Walipoondoka Wajerumani na kuingia Waingereza wao wakapiga marufuku matumizi ya hati za Kiarabu.

Ikawa sasa mtu aliyekuwa anajua kusoma na kuandika kwa sheria hiyo ya kikoloni ghafla akawa mtu aiyejua kusoma na kuandika.

Ujenzi wa shule kuchukua nafasi ya madras ukaanza na elimu ikiwa mikononi mwa Wamishionari na serikali na ikiwa mtoto anataka kuingizwa shule kusoma ilibidi abatizwe awe Mkristo.

Hiki kikawa kikwazo kikubwa kwa Waislam kupata elimu.

Hassan Omar Makunganya shujaa aliyepigana na Wajerumani na wakamnyonga Kilwa ameacha hazina kubwa ya maandishi aliyokuwa akiandika kwa hati za Kiarabu wakati wa harakati dhidi ya utawala wa Kiarabu.

Nyaraka hizi zipo Zentrum Moderner Orient, Berlin.

Halikadhalika Mtwa Abdallah Mkwawa wa Uhehe ameacha barua zake alizokuwa akiandika kwa hati za Kiarabu.

Barua hizi zipo Mkwawa Museum Kalenga.

Babu yangu Sheikh Muhammad Mvamila alikuwa akiandika siku zote kwa herufu za Kiarabu hadi anakufa.

Ndugu zangu ikiwa tutaacha mihemko na kejeli hapa tunaweza tukafanya mijadala ya manufaa kwa jamii yetu na tukaelimishana mengi.

Umeitaja Qur'an kwa dharua ''kitabu chao'' lakini umegusa kitu kimoja cha maana sana nacho ni ''hifdh'' yaani kuihifadhi.

Kuhifadhi Qur'an ni moja ya vipimo vya uwezo wa akili ya mtu.
Si uungwana kukashifu dini ya mwenzio.

Siamini kama Bwana Yesu haya ndiyo mafunzo yake.

1672980490790.jpeg

Moja ya barua ya Mtwa Mkwawa katika Mkwawa Museum​
 
Zanzibar ilikuwa ndiyo Dola kuu hadi ndani ya Afrika ya Mashariki.Zanzibar ikawa chini y waarabu qa Oman kuanzia 1698 hadi anachukua madaraka Seyyid Bin Said Al sultan Bhusaid mwaka 1804.Hapo kabla 1741 familia ya Mazalia au Mazrui pale Mombasa ilijitangazia uhuru lakini baadaye ilipigwa na kurejeshwa chini ya Oman.1840 sultan anahamia Zanzibar,maeneo karibu yote ya yalitawaliwa na watawala watiifu kwa sultan wa Zanzibar.

kwa hiyo ndio shule mliyojenga
 
Watakwambia waliacha ustaarabu ukiuliza ni ustaarabu gani huo walioacha eti kutawaza yani kunawa matako baada ya kujisaidia ni kitu wanajivunia sana toka kwa waarabu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nachekaga sana hawa ndg zetu

Waarabu na wafuasi wake ni moja kati ya wanadamu wapumbafu sana. Huyo mwarabu asingepewa mafuta angekua ndio bogaz kabisa
 
Back
Top Bottom