Habari wadau.
Nasikia baada ya kupata uhuru mwaka 1961 Serikali ilitaifisha shule zilizojengwa na wakoloni. Mfano shule zilizojengwa na wakoloni wazungu kama Minaki, Ilboru, Pugu, Mazengo, forodhani, etc
Je, ni shule zipi zilitaifishwa ambazo zilijengwa na wakoloni Waarabu?
Maana waarabu walitangulia kuja Tanganyika na Zanzibar kwa kwa miaka zaidi ya 500 kabla wakoloni wazungu hawajaja.
Zanzibar pia waarabu walifika mapema sana maana msikiti wa Kazimkazi ulijengwa mwaka 1006 AD, waarabu walitawala kwa miaka mingi Zanzibar na walifika mapema sana, naomba mnitajie ni shule gani ya sekondari waarabu walijenga Zanzibar, na ilijengwa mwaka gani?
Sijui ulitaka KUMAnisha nini ila kwajinsi nilivyokuelewa kwambaali ipo hivi:-
Walijenga chuo kikuu cha kwanza Afrika Mashariki, Kati na Kusini
Chuo hicho ndio ilipo Ikulu ya magogoni leo hii,
Walijenga kituo cha utafiti cha kwanza Africa mashariki, kati na Kusini
Kituo hicho ndio Hospitali ya Ocean road leo hii
Wakati huohuo kumbuka mawasiliano ya kimaandishi yalifanywa kwa lugha ya kiswahili kwa kutumia herufi za Kiarabu
Ukitaka kuthibitisha hilo, kaangalie sanamu ya askari pale posta kuna sehemu imeandikwa kwa kiswahili kutumia herufi za Kiarabu
Hii inaonyesha hata wakati wa koloni la ujerumani bado mawasilano ya kimaandishi miongoni mwa jamii katika kupashana habari za maendeleo yalikua yanafanywa kwa kutumia maandishi ya kiarabu
Kwa muktadha huo wasomi wa kwanza kabisa wa nchi hii ambao walikua wamebobea katika elimu mbalimbali hasa tiba, sheria na ujenzi kabla ya kuja mkolini wa ulaya walikua waislamu na waarabu
Miongoni mwa wanazuoni hao wapo waliobobea katika falsafa za fani mbalimbali kwenye sayansi mbalimbali za jamii, uchumi na siasa, na katika wao wamerithishana elemu kwa vizazi kadhaa jambo linalo thibitisha kuwa elimu hiyo ilikuwepo kwa muda mrefu tu
Lakini pia miongoni mwao wapo walio shiriki kikamilifu katika ulezi wa juhududi na muongozo wa harakati za kupigiania Uhuru wa inchi hii. Mwl. Nyerere amewataja miongoni mwao kwa majina na wasifu wao pia. Kumbuka hawakua mbumbu walikua wanataaluma zao walizozipata katika madarasa yao kwa mfumo wa elimu zao wakiti huo.
Unachopaswa kuelewa wazungu walipokuja walikuja na mfumo wa elimu tofauti kabisa na elimu iliyo kuwepo, kibaya zaidi elimu zote hizi zilikua na msingi wa imani kwanza ndio uelimike jambo ambalo wazee wengi waliokua na elimu ya mfumo uliowajenga kiimani walikataa kupokea elimu mpya Kwa sababu ilikua ni vigumu sana kwa wao kubadilisha imani zao