Ni siku gani kubeti kulitaka kukutoa uhai?

Ni siku gani kubeti kulitaka kukutoa uhai?

Tatizo wengi tunabeti mpira wa miguu na direct win cha msingi ni kubadili michezo au kucheza throw in ,foul ,shots au corner
Kuna option za magoli hasa over 0.5 ni mara chache sana kutotoa japo sio timu zote, kwa sasahivi naona timu nyingi hazitoi draw ya 0-0 yani kagoli kamoja lazima kapatikane hasa ligi ya japan na blazil ila hizo direct win ni hatari kwa afya
 
Oioioi mi kanji kashachukua Sana akiba zangu na nimetumia skills zangu nyingi za Kubet kwa ajili yake sasa safari hii nacheza na odds 1.40 kushuka chini yani hapo wenye mtaji mnifate tumnyooshe kanji
FB_IMG_16655625888103657.jpg
 
Juventus 0 - 1 Empoli.

Nilikosa usingizi mwezi mzima na bodaboda yangu niliiona chungu mwezi mzima nilikuwa natoa deiwaka tu!.

Niliweka mkeka sportpesa wenye mechi 38(behewa)ambao endapo ningeshinda nilikuwa najikamatia 22 Milioni point something na niliweka buku 2 tu.Sitakaa nisahau aisee!.

Mechi zote nikafanikiwa kushinda na ikawa Imebaki mechi ya Juventus vs Empoli,ilikuwa mwanzo kabisa wa ligi na nakumbuka ndiyo Ronaldo amemaliza kuhama Juventus!,hakuna siku niliomba,kufunga na kusali kama wakati naisubiri hiyo mechi!.Kibaya zaidi nilimpa Juventus direct win na kibaya zaidi saaaaaana hiyo hela nishaanza kuipangia bajeti!.

Aisee baada ya ile mechi nilizima simu wiki nzima na sikupata usingizi takribani mwezi kila nikikumbuka!.

Omba yasikukute mkuu!.
 
Game ya Juzi

Atletico Madrid - Rayo Vallecano

Nilimpa Atletico Madrid nikawa nasubiria mpira uishe nile pesa yangu sasa angalia kilichotokea

View attachment 2392517
Unaambiwaje direct optns ni hatari kwa afya yako,hapo A.Madrid alikua yupo kwake.A.Madrid ni timu yenye nguvu zaidi ya mpinzani wake,ungetupia 1×.
japo kua hata timu yenye nguvu inaweza kubamizwa na timu dhaifu.
 
sitosahau mwaka 2017 mkamalia mwenzangu alivyoaga dunia tukiwa kwenye gari tunampeleka hospital..story ilikuwa ni ivi jamaa alibeti timu 11 premier betting akatia 250k ikawa inatoka 110m mechi 6 zilikuwa zinacheza jumamosi, 4 jumapili na moja jumatatu ..zikatoa zote ikawa imebaki moja inacheza jumatatu LIlle vs PSG ..jamaa alishajipa uhakika mazima kuwa PSG anashinda akaenda mpaka kutafuta kiwanja cha kuanza kuje ga ..siku ya mechi PSG kafa 4-2 tukamuona mtu anaishiwa nguvu mara pumzi inatoka kwa shida kumuaisha hospital akafia njian.
 
Juzi Udinese vs Atalanta, nimebet live, halftime Atalanta anaongoza 2-0, nikawaamini wazee wa kipindi cha pili, nikamuwekea Udi ashinde...hadi 90' ni 2-2 na game ikaisha hivyo. 250k ikapotea hivyo, ila wangeshinda ilikuwa nichukue 1.5m coz Udi baada ya kupigwa mbili odds zilishoot hatari. Ila siachi ng'o!
 
Unaambiwaje direct optns ni hatari kwa afya yako,hapo A.Madrid alikua yupo kwake.A.Madrid ni timu yenye nguvu zaidi ya mpinzani wake,ungetupia 1×.
japo kua hata timu yenye nguvu inaweza kubamizwa na timu dhaifu.
Hio direct ilikua na odds 1.52 na 1× ilikua na odds 1.02 sasa ningeweka 1× hakuna ningepata maana lengo ni kupata faida
 
Back
Top Bottom