Intelligent businessman
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 31,913
- 65,514
Asante, ila muda mwingine tv inajibonyeza, au kuwasha kitaa chake pasipo Mimi kufanya hivyoHizo 'rimoti' zake itakuwa zimeingia maji au kama una watoto watakuwa wamezijaza mate...
Jaribu kufungua uzikague...
Pia watu wafanyabiashara hawakupeleki Samsung sababu ya Margin ni ndogo hasa maneno yenye competition.
Mfano tv ya kichina ni 250,000 wanaweza wakauza 450,000 margin kubwa, ila Samsung wanapata 550,000 wanauza 600,000.
Samsung wapo official kabisa Tanzania, sidhani kama kutoa mstari ni issue, ukiwa na warranty na unajielewa wataitengeneza bure.
LG hawana Qled... Qled ni technology ya Samsung.Hizi ndio shule nilikuwa nahitaji mpaka kufunguwa huu Uzi.
Mkuu kwa kunisaidia nimebaini LG wako vizuri ingawa hawakuwa mawazoni kwangu kabisa, Sasa nataka nijilipuwe na LG.
Kwa Sasa LG hiyo Qled ya inch 43 inakwenda kwa bei gani na authorized agent au dealer anapatikana wapi?
We jamaa Xiaomi naye anazo simu expensive. Watu wengi wanaojaribu kuelezea hii mada kupitia reference ya simu naona wanaboronga. Hata Samsung ana A series ambazo ni simu za chini na kati ndio kama hizo TV zao za laki sita. Kama bajeti ni laki sita na nusu nunua Hisense
Hama kwanza unapokaa kama ni Nyumba ya kupanga la sivyo utaibiwa Tena. Kama ni Nyumba Yako boresha ondoa mazingira yote yanayotoa gepu Kwa wezi na pia ongeza ulinzi. Ukishindwa kufanya hayo hiyo mpya utayonunua au hata hiyo 32 itaibwa tenaWadau nilikuwa na smart TV 4 K nchi 50 wale wajaa laana wakasepa nayo.
Nina Samsung Hd nchi 32 ilikuwa chumbani ndio nimeileta sebuleni yani tofauti ni kubwa sana.
Sasa nimeokota pochi la mzungu nataka ninunue TV ya kweli nirudi kwenye modern life.
Karibuni kwa ushauri.
Apple tv ndo tv gani hiyo?..Ni bajeti yako tu mkuu
Wale wachovu wenzangu wanakwenda na Boss, StarX
Hizi ni sawa na watumiaji wa simu wa Tecno, Itel, infinix
Wale wa uchumi wa kati wanakwenda na Hisense, TLC
Hizi ni sawa na watumiaji wa simu za Oppo Xiaomi nk
Wale wanaojiweza wanakwenda na Sony LG Samsung Apple Tv
Hizi ni sawa na watumiaji wa simu za Samsung iPhone nk
Watu wanajiropokea tu.."Sony kali,sony kali..bila hata kusema ni type ya sony.Humu naona watu wana bwabwaja tu wala hawatoi jibu la kueleweka. Hawa TV manufacturers wote wana TV za level mbali mbali kwa budget mbali mbali. Mfano LG zipo za kawaida, nanocell, QNED,OLED etc! sasa wewe unapomwambia mtu nunua LG/samsung/Sony/Hisense ndio bora! Ni LG ipi? na ni bora kuliko hisense ipi? Maana hisense wana za kawaida, ULED (QLED/ Mini LED) etc! Mshauri mtu kwa specific model kutokana na budget yake lakini si kulinganisha the whole brand
Apple tv ndo tv gani hiyo?..
Apple walichonacho sio tv box tu?
Watu wanajiropokea tu.."Sony kali,sony kali..bila hata kusema ni type ya sony.
Hitachi na TCL Mbona hamna uhusiano wowote?Nilipoanza kununua flat TV nilianza na LG ya LED 43" ila aliporudi mbabe wa kioo bwana Hitachi kwa jina la TCL sikujishauri kuvuta smart TV ya 55" kwao, kutokana na durability ya product zao. Nna imani hiki kioo kitapiga kazi kwa hadi miaka 15 mbele bila tatizo (kuna tv ya Hitachi ya 21" ilinunuliwa na dingi 1998 na mpaka sasa inapiga kazi, imekuwa inahama vyumba tu pale home na kwa sasa iko ghetto la msaidizi wa kazi wa home ikiwa haijachora hata mstari mmoja)
Ameshadanganywa na wauza tvHitachi na TCL Mbona hamna uhusiano wowote?
Nikweli Samsungu zinazo kuja Tanzania siyo zinazo kwenda Ulaya, we jaribu kutafuta Samsung ya Ulaya na Ya Tanzania utaona utofauti kwenye Menu, Samsung zaki bongo hazina mambo mengi yani ata mshamba anaweza kuichezea na akiifahamu kwa harakaMkuu nimejibu kulingana na ubora wa bidhaa tunazozipata zaidi Tz
Najua kama zipo Xiaomi kali
Hizo TLC na Hisense zinazo kuja bongo ni za kichovu kama Xiaomi zinazopatikana kwa wingi huku
Jamaa wana product zinacompete na wakina LG, Sony Philips nk
Haya Samsung tv nyingi zinazokuja huku sio zile zenyewe ni za quality ya chini
Nilinunua remote ya LG Home Theater (watoto waliharibu) kwa bei ya kawaida kabisa pale Kariakoo, labda hizo za Tvs zinaweza kuwa juu. Ukipata latest tech ya LG nadhani utafurahia hata kuangalia TV yako.Ukianzia Mwanzo wa thread mpaka hapa tayari jibu unalo na tofauti ya hizi tech sijui HD, Qled, 4K Dolby sijui nini nini kwenye upande wa TV tayari una muongozo nzuri ujilipuwe wapi.
Binafsi naona nilijilipuwe na LG ila kuna mdau kanitisha hapo anadai remoti ya LG ikiharibika inauzwa laki mbili, huu nao ni mtihani kwa sisi wenye Watoto ambao bado watundu.
Ukianzia Mwanzo wa thread mpaka hapa tayari jibu unalo na tofauti ya hizi tech sijui HD, Qled, 4K Dolby sijui nini nini kwenye upande wa TV tayari una muongozo nzuri ujilipuwe wapi.
Binafsi naona nilijilipuwe na LG ila kuna mdau kanitisha hapo anadai remoti ya LG ikiharibika inauzwa laki mbili, huu nao ni mtihani kwa sisi wenye Watoto ambao bado watundu.