Samsung zote ni OG mkuu, hao wanunua Sinsung sio Samsung.
Pili wananunua tv kwa fundi tv sio Dukani. Uliwahi kuona wapi Samsung tv inauzwa laki 2 ama laki 3. Wanapenda vya dezo halfu wanakuja kulaumu brand badala ya kujilaumu wenyewe.
Mkuu punguza ujuaji, aliekwambia Samsung zote OG nani? Kwa zaidi ya 60% Tanzania tunatumia TV za Samsung fake, mwisho wa siku nunua kitu kulingana na uelewa wako lakini kikubwa uongozwe na budget yako
Mtu unakuta ana budget ambayo yeye alipenda kupata TV smart ya inch 43 ila budget yake hawezi kununua Lg, Samsung au Sony kwahiyo asinunue sasa? Uwepo wa makampuni mengi ya bidhaa lengo ni kila mtu apate kitu kulingana na uwezo wake
Ukitaka kujua tz tunapigwa sana we agiza TV China, Unaulizwa unataka Original?high copy au end copy? Na hapo hawamaanishi kwamba hizo copy na high copy zitaandikwa sumsung wala singsung bali zote ni Samsung unazikuta na kila kitu chake kama zilizo zingine
Samsung nchini kwetu nyingi sana zinakuja fake maana washajua kuwa tunapenda Jina ila uwezo wa kununua OG hatuna kwahiyo tunapewa kile ambacho tunaweza afford
Nenda posta Samsung store na model na series alafu omba uoneshwe TV original, we kazana uoneshwe TV original yani urudie tena unataka TV original, alafu icheki na chukua bei kisha Rudi kariakoo karinganishe bei
Hiyo ni option one, option 2 tafuta mtu alie China kisha mpe model ya TV ya Samsung aende Samsung store kisha apewe bei, na huko ndio atakutana na issue ya OG,High copy na end copy alafu usikie bei zao wenyewe uone kama tutaweza nunua
Usiishi Kwa kukariri mkuu, japokuwa Heshima ya Samsung kwenye ubora wa bidhaa zake kila mtu anaujua ila ukweli ni kwamba karibia zaidi ya 70% hawatumii Samsung OG kwa sasa ila wao hawajui tu
Walionunua TV za Samsung miaka ya zamani utagundua kuwa TV zao nyingi hadi leo zinadunda fresh tu, ila njoo Kwa hawa wanaonunua hii miaka ya karibuni ni kisanga Mzee mwenzangu
The same na kampuni zingine expensive kama vile Lg saizi tunapigwa tu kisa trade name, ata Hisense pia zina OG zake na fake zake, Tanzania hivi sasa kumejaa vitu fake, wakati iPhone 14 inatoka Yani china store hakuna ila teyari Tanzania kina bilnass wanaziuza na watu wananunua kama kawaida
Nenda posta au kariakoo Kwa mafundi wakubwa wa TV alafu ulizia ni kampuni gani Kwa sasa zinaongoza Kwa kufa, hadi mwaka Juzi me nipo kariakoo ilikuwa ni Samsung ikifatiwa na LG, Samsung ilikuwa inaongoza kufa kioo na LG ilikuwa inaongeza kuunguza AC
Nasema kariakoo na posta kwa sababu huko ndio walipo wanaotumia hizi kampuni, sio uende Kwa mafundi wetu wa kigogo au Manzese zimejaa TV kampuni za hadhi yao huwezi kuta hizo Samsung na lg wala Sony na ukikuta basi inatumika kama sampo tangu mwaka 2016, utakuta BOSS,Aborder,Zunne,singsung nk