Ni smart TV gani 4K kwa sasa ipo vizuri sana?

Na mimi nataka niijaribu mkuu ila nchi 43 smart
 
Nipe link ya samsung tanzania tuone inakaaje
 
Hii TV niliyonayo ni Samsung HD inch 32, nilinunua laki saba wakati ndio zinatoka, imeshawahi kupigwa chini kwenye domestic violence lakini iko vilevile na Ina miaka zaidi ya 10, je Samsung bado watakuwa na bidhaa imara kiasi hiki kwa miaka hii?
Nina Samsung 5 series 32"

Me sio mpnz mtazamaji Ni mpenzi msikilizaji I spend more kwenye sound kuliko TV's Ila hio tv sijaona shida yake hata ipo njema Sana miaka kadhaa sasa
 

Hiyo Hisense unayoipigia debe kwana
1. Haina “Play Store”
2. HDMI port moja ndio ina support kifaa cha 4K kama PS5 zingine zote ni hdmi za kawaida
3. Ukiweka flash yenye movie ya 4k yenye file la MKV au MP4 haichezi

Kwa kifupi Hisense ina support 4k kwenye Youtube tu.

Sony
Sumsang
LG

Zilikuwepo na zitabaki kuwepo ni sawa na useme mwenye iphone na infinix zote ni sawa unapiga na kupokea.
 
Software ya hisense ni ya kiboya sana kusema kweli. Ninayo Hisense moja hapa, mpaka uconect na Desktop ucalibrate na Nvidia Gpu ndio unapata Quality nzuri.

Ila Vidaa unapata Quality mbovu na kama Kama huna ujuzi utaangalia picha mchele mchele maisha yako yote.
 
Mkuu samahani natoka nje ya mada kidogo.
.nataka kuchukua simu ya g.pixel mojawapo kati ya 3a xl au 4a 5g kwakua zina betri kubwa.kwakua 4a 5g ina camera mbili za nyuma je inaweza kuizidi 3a xl kwa camera?
Maana naona 3a xl bei ipo chini sana kuliko 4a 5g.
 
Natumia solarmax haina hata shida inapigabkaz balaa kitu mng'ao
 
Sasa hii kwa akili yako wewe ndio inakuonyesha kuwa Hitachi ndio wanatengeneza TCL? Hii inaonyesha kuwa anayetoa warranty anatoa kwa TCL na Hitachi. Maana yake ndio anayeimpont hizi bidhaa kwa Tanzania. TCL ni kampuni ya china while Hitachi ni ya JAPAN.
 
Kwa hiyo kwa laki saba TV gani wewe unashauri ambayo Ina hizo sifa [emoji848][emoji848] Ni vizuri useme kwa faida ya wengi.
Hamna tofauti na watu wanaotaka Super AMOLED display kwenye simu za laki mbili
 
Kama priority ni charge tafuta 5A,

4a itakua nzuri kuliko 3A
 
Reactions: PYD
PS5 ili upate features zote inabidi TV yako iwe na hdmi 2.1. Matoleo mapya ya tv sana sana zile midrange to high end ndio yana HDMI 2.1 na si tv zote. PS5 pia inaconnect kwa HDMI 2.0 ila features zote hutozipata. Kama tv yako ilishindwa kuconnect na ps5 inawezekana kuna shida mahali, sababu hata cable unayotumia huwa inachangia.
Hisense zenye android kama zina play store, sasa ulitaka yenye vidaa iwe na play store? Lg wana play store? Samsung wana play store? Play store ni kwa android tv na Google tv tu
 
Nimechukua hisense u7h juzi, vyote unavyosema havina ukweli. Hisense zenye vidaa haziwezi kuwa na play store maana play store ni kwa ajili ya android/Google tv. Ina hdmi 4, Mbili ni hdmi 2.1 120hz (mojawapo ni eARC), Mbili ni hdmi 2.0,ina USB 2.0 NA USB 3.0 na nimechomeka hdd hakuna file lolote lililogoma. Sasa sijui wewe umetumia hisense ipi?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] uchumi wa chini ndo upoje mkuu yani kwa mwaka anaweza akaingiza shilingi ngapi?
Uchumi mdogo kwenye familia na tatizo la kutokujua Elimu ya bidhaa bora ilimradi kuambiwa TV flat laki mbili na nusu nchi 32 ili miradi tv iwepo ya kutazama taarifa ya habari ITV saa mbili usiku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…