Ni smart TV gani 4K kwa sasa ipo vizuri sana?

Mo ni wakala ila sidhani kama Ana service centre.
Kuna wakala wawili wa LG Tanzania. Kuna Mo na Garnet star. Mo anapatikana posta nkurumah street oppsite na LATRA na service centre iko hapo hapo. Huyu Garnet star anapatikana Moroco na service centre iko hapo hapo. Ila pia kuna service centre ya LG inayojitegemea ipo kariakoo Nasra tower.
 
My mistake mpo sahihi HIMARS


Kuna kipindi ilikuwa ukitafuta service centre unapelekwa Nairobi, sasa hivi Website ya LG inaonesha kuna Service centre 3 tofauti, Morocco opposite Airtel, Nasra tower na Metl new Chox Nkurumah.
 
Wakala wa Sony yupi kwa Dar?
 
Wakala wa Sony yupi kwa Dar?
Wakala wa sony aliyepo ni Anisuma traders na duka lake liko mlimani city. Kwa bahati mbaya Sony kama imemzidi nguvu kusuply katika sokoni so kuna uhaba kabisa wa Tv za Sony. Nyingi zilizopo ni za watu kununua Dubai na china na kuzileta kwa jina lingine inaitwa Parallel Input au PI.
 
Duh siku hizi umasikini unapimwa kwa kuangalia brand ya TV unayoikubali?[emoji38][emoji38]
Sawa bwana, yangu macho tu[emoji23][emoji23]

Kwani hujui usiano wa purchasing power na income levels? Assuming preferences sio issue!

Ushawahi kuona maskini anakimbilia kununua iphone au BMW? Au anunue Samsung home thatre badala ya Subwoofer ya Sea Piano?

Ukumbuke global brands ni expensive, sasa nani asiyetaka hizo brand maarufu? Kikwazo ni kipato Mkuu!
 

Tafuta 3.5 mm jack kwenye tv,itumie hiyo kuhamisha sauti kwenda kwenye sabufa.kisha tumia waya huu hapa chini,sidhani kama kuna TV inakosa hilo tundu la earphone.
 
Kuna masikini kibao wananunua iPhone na kuna jamaa yangu Mzee wake ni mbunge lakini anatumia Infinix Smart 6 licha ya kuwa na nyumba ya gharama kubwa na ukizingatia ni mbunge , nilishangaa sana. Ndio nikaacha kupima uwezo wa kifedha wa mtu kwa kuangalia simu au labda TV au bidhaa yoyote anayotumia🥱🥱
 
Brand comes first

Brand matters

Tatizo tunatumia umasikini wetu kudowngrade hizo brand kubwa..kumbuka hazikufika hapo bahati mbaya

Tukubali tu…SONY,LG,SAMSUNG is the best

Quality,technology and durability and value for money
 
Lakini wabongo tuna dhana mbaya sana.

Hivi kweli mtu hata mwenye iphone 11 mtu anaona ana hela[emoji28][emoji28].

Tunashindwa kujua mtu anaweza jitia ujinga tu akauza shamba akanunua iphone.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ndio kama hapa tu, kisa watu wanatumia TV za Samsung na LG ndo wanajiona matajiri[emoji38][emoji38]
 
Brand comes first

Brand matters

Tatizo tunatumia umasikini wetu kudowngrade hizo brand kubwa..kumbuka hazikufika hapo bahati mbaya

Tukubali tu…SONY,LG,SAMSUNG is the best

Quality,technology and durability and value for money
Hakuna aliyekataa ila hapo kwenye value for money hebu nishushe kidogo[emoji2960][emoji2960]
 
Nitajie Tekno inayoweza kurekodi 8K
 
Sasa uchati whatsapp kwenye TV ili iweje? Watu wengine bana!
 
Hakuna aliyekataa ila hapo kwenye value for money hebu nishushe kidogo[emoji2960][emoji2960]

Soma vizuri line ya mwisho


—->Technologieën,Quality,durability

Hivo vitu ndo vinakupa value for money!

Nikupe mfano:mwaka 2012 nlinunua sony bravia 32’

Hii tv mpaka leo ipo haimjui fundi…ubora wake na teknolojia kwa kipindi kile ilikuwa mbele ya muda sana.
Mpaka nmeamua kununua sony Android juzi juzi

Hapa mimi sibishani wala si downgrage kampuni zingne ka hisense hapana..ila nazungumzia ubora wa kampuni fulani.

Unaweza kupata teknolojia na uzuri kwa bei rahisi lakini Ubora ni kitu kigumu sana kukipata kwa bei rahisi!!

Ubora ndo huamua bei…

(Nliwahi kutembelea nchi fulani nkakuta hizi saa za Hublot,Casio na Rolex original ni kuanzia £700 huko!

Nlishangaa kwasababu huku kwetu Rolex unapata kwa efu50 lkn ile high quality ambayo tunaona ni O.G inauza laki 3[emoji2][emoji2].

Nlichokuja kugundua kitu bora chochote ni gharama

So kwa bei ya original SONY,LG na SAMSUNG ni sawa kabisa kwa sababu ya ubora

Fid Q aliwahi kusema
“…kizuri ni kizuri lakini chenye ubora ni bora”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…