Reuben Challe
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 2,940
- 5,511
Umesomeka bossSoma vizuri line ya mwisho
—->Technologieën,Quality,durability
Hivo vitu ndo vinakupa value for money!
Nikupe mfano:mwaka 2012 nlinunua sony bravia 32’
Hii tv mpaka leo ipo haimjui fundi…ubora wake na teknolojia kwa kipindi kile ilikuwa mbele ya muda sana.
Mpaka nmeamua kununua sony Android juzi juzi
Hapa mimi sibishani wala si downgrage kampuni zingne ka hisense hapana..ila nazungumzia ubora wa kampuni fulani.
Unaweza kupata teknolojia na uzuri kwa bei rahisi lakini Ubora ni kitu kigumu sana kukipata kwa bei rahisi!!
Ubora ndo huamua bei…
(Nliwahi kutembelea nchi fulani nkakuta hizi saa za Hublot,Casio na Rolex original ni kuanzia £700 huko!
Nlishangaa kwasababu huku kwetu Rolex unapata kwa efu50 lkn ile high quality ambayo tunaona ni O.G inauza laki 3[emoji2][emoji2].
Nlichokuja kugundua kitu bora chochote ni gharama
So kwa bei ya original SONY,LG na SAMSUNG ni sawa kabisa kwa sababu ya ubora
Fid Q aliwahi kusema
“…kizuri ni kizuri lakini chenye ubora ni bora”