Ni smart TV gani 4K kwa sasa ipo vizuri sana?

usiondoke subiri finali endelea na mchujo hadi upate iliyochaguo lako
Tayari mkuu nimeshachukuwa TCL "50" na gurentee ya mwaka mmoja nilikaa nayo miezi kadhaa ikaanza kuchora mistari nikarudisha nimepewa nyingine mpya inapiga mzigo fresh.

Hizi Waranty muwe mnazitunza na mnunuwe kweñye maduka ya kueleweka, likitokea tatizo wanakubadirishia unapewa brand new.
 
Evvoli 43EV200DA Bei 650
Kwa hii bei kwa mchina mkuu naona kama ipo juu, hasa kwa vile ni FHD na haina 4K. Wachina waliochangamka kama TCL na Hisense unapata chini ya laki 6 kwa same specs.
 
Chief nipo arusha,Bei za dasilamu ni tofauti na huku
Bottom line mkuu ni warranty, hakikisha unapewa warranty ya maandishi na wana sehemu ya kutengenezea huko kwenu.

Kama mdau mwengine alivyokushauri angalia na wengine wanauzaje huko,
 
Nawashangaa sana watu wanaopuuza ubora wa Hisense au kwa kuwa inatoka china,kwangu mm ukiondoa sharp(mjapan) anayefata kwa ubora ni Hisense tena unapata kwa bei nafuu kabisa sharp Tv zake haziji sana Africa sababu ya bei yake kuwa kubwa ila Hisense kashika sana soko hadi ulaya bidhaa zao ni bora sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…