Ni suala la muda tu ila Sauli na New Force mabasi yanayoelekea Tunduma na Mbeya yatamaliza watu

Ni suala la muda tu ila Sauli na New Force mabasi yanayoelekea Tunduma na Mbeya yatamaliza watu

Hapana kwasasa madereva hawakimbii kabisa hivi enzi zile Dar- Mbeya masaa 9 tu ungesemaje? Au Dar- Arusha masaa 7( Ngolika vs Buffalo), Mwanza-Dar masaa 13 tu (Ally's, Mombasa Raha, Colour star) au Kahama-Dar Masaa 11 na nusu au 12 ( Leina, Ally's ) [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Leina Tours[emoji28][emoji1430] Dar-Khm saa 12:30 jioni
 
Haya tuambie tokea Sauli katoa bus zake lini limepata ajali na kuleta maafa?? Kwa nini kama bus inatakiwa isizidishe speed ya km 80 kwa saa serikali isilete Sheria ya kuingiza bus zenye speed max km 80 kwa saa?? Mwisho kama hupenzi Gari yenye speed si upande Majinja au ABOOD??
Endelea kukumbatia unachoamini mkuu. Sijawahi panda hayo mabasi lakini kupitia mitandao ya jamii na video mbalimbali nachelea kusema kwamba hayo magari yanavunja sheria mbalimbali za barabarani. Mbaya zaidi ni hilo la Mwendokasi. Kutopata ajali sio kigezo kwamba hizo gari ziko sahihi na zinatii sheria. Cha msingi ni kuomba kwa Mungu yasitokee na wakati mwingine wahusika wakichukua tahadhari.
 
Tatizo sio kampuni, anayesababisha ajali ni madereva, wanatakiwa waachishwe kazi
 
Kuna hawa Wa STL masaa 3 Dodoma- Dar sijui unawazungumziaje hawa mtu anatoka Dar kabla ya saa 1 yupo Mwanza
 
Kuna wengine wa njia ya mwanza.. wanakimbia sana. Hawaongelewi sababu wanafika muda ambao tunaona ni usiku mwanza. Ila kutoka dar mwanza umbali wake ukifika saa 4 usiku maana yake umekimbia sana kuliko hizo sauli na new force za mbeya na tunduma

Bus inayofika mbeya saa 12 jioni kutokea dar spidi yake ni ndogo kuliko bus iliyofika mwanza saa 4 usiku kutokea dar pia

Dar - Mby - 900km
Dar - Mza - 1100km

200km kwa tofauti ya masaa manne unamaanisha nini kusema kwamba amewahi Mkuu?
 
Naunga mkono hoja hawa jamaa wako rafu sana barabarani hasa kwenye kutanua!
 
Dar - Mby - 900km
Dar - Mza - 1100km

200km kwa tofauti ya masaa manne unamaanisha nini kusema kwamba amewahi Mkuu?

Nani amekwambia dar mwz ni km 1100 na dar mbeya ni 900 km?

Nenda kafanye research kwanza. Tanroad wana chat ya bara bara nchi nzima na umbali wa kila mkoa kwenda mkoa mwingine. Tumja google kuitazama.

Acha stori za vijiweni ambazo hazina research

Kwa kukufunza tu Tofaut ya umbali wa dar mwanza stend ya nyegezi na dar mbeya stend ya uyole kwa kusafiri kwa bara bara ni zaidi ya km 300
 
Nani amekwambia dar mwz ni km 1100 na dar mbeya ni 900 km?

Nenda kafanye research kwanza. Tanroad wana chat ya bara bara nchi nzima na umbali wa kila mkoa kwenda mkoa mwingine. Tumja google kuitazama.

Acha stori za vijiweni ambazo hazina research
Nimekuwa nikifanya safari za Mara kwa Mara baina ya hii mikoa Mkuu.
 
Barabara zetu ndo chanzo cha ajali waweke dabo road kwani shida nn.
Mfano gari likifeli breki mlima wa mbalizi ni lzm lirudi kuchinja watu
 
Huyo ALLY's STAR Nlishaapaga sipandi tena. Lilikuwa linatoka MWZ nikapandia GAIRO... Saa 4¼ Usiku nashuka MBZ! Jamaa anaOVERTAKE pale CHALINZE km Baiskeli
Kuna watu hawajui kuna kukimbia na kuendesha rough mabus mengi haya kimbii ila rough wanaweza ku mantain hata 70 kwa hrbhasa Sauli Kwenye tuta anapita na speed 80 sabb gari zina booster mfano anaweza ku overtake sehem hatarishi lakini hajazidi ile speed waliyopangiwa hakuna ma Bus hatarishi kama Dar mwanza hawa Ally Stas Happy Nation ila hawaoni

Sent from my CPH2061 using JamiiForums mobile app
 
Uendeshaji wao ni wa hovyo kabisa na hauzingatii sheria na kanuni za barabarani.

Sauli hununua Askari wowote wawao zamu siku husika wa usalama barabarani kuanzia Igawa hadi Tunduma na hutoka mtu maalum na gari ndogo Mbeya mjini kwa ajili ya wao wanachokiita kusafisha njia.

Narudia,Sauli na New force ni janga litarajiwalo huko Kusini mwa Tanzania.
Watakubeza kuhusu hizo basi, lakini ukweli ndio huo!!!

Mamlaka tunaomba ingilieni kati kuhusu mienendo ya kampuni hizo za usafirishaji. Hii ni pamoja na mabasi mengine yasiyozingatia sheria, kanuni na utaratibu!!!
 
Nikikumbuka nilikua najifunzia kuendesha gari kwenye bus la abiria likiwa na abiria 55 ndani ya bus tena safari ndefu naendesha nusu safari chuma ina gia 8 na hata kupangua gia sijui vizuri nachoka kabisa na nilikua namwaga Moto kinoma
 
Hapana kwasasa madereva hawakimbii kabisa hivi enzi zile Dar- Mbeya masaa 9 tu ungesemaje? Au Dar- Arusha masaa 7( Ngolika vs Buffalo), Mwanza-Dar masaa 13 tu (Ally's, Mombasa Raha, Colour star) au Kahama-Dar Masaa 11 na nusu au 12 ( Leina, Ally's ) [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nimeyapanda yote hayo. Mombasa Raha walikuwa wastaarabu sana kwani nili-opt kulipanda kila mara hasa Mwz-Dsm. Ally's nilipanda mara 1 nikasarenda. Bufalo na Ngorika niliyaacha kabisaaa.

Baadae nikahamia Yutong za mwanzo (Golden Intercity Bus) kabisa kutoka Mwz-Dsm.
 
Back
Top Bottom